Time Travel Kwenye Ndoto

Duuh! swali gumu ni hilo sasa je, yapi ni maisha halisi?
kweli mkuu, maana ki uhalisia mtu ukiwa ndotoni ni ngumu sana kujua kama unaota(bali utaona kila kitu kipo katika uhalisia wake,kuanzia mazingira,watu,na shughuli zote zinazoendelea zipo kawaida kama haya maisha yetu ya jf,bali utofauti utakaokuwepo ni swala mda na wakati, kuhusu mda ni kwamba kila kitu kinafanyika/kutendeka papo kwa hapo, ama kufumba na kufumbua, kwa mfano ukiwa ndotoni labda ukawaza kwenda mahali tofauti na hapo ulipo utajikuta mda huohuo umefika mahali ulipokusudia, haijawahi kukutokea!? na kuhusu swala la wakati kwenye ndoto huwa halipo unaweza ukajiona umezaliwa umekua umekufa kwa wakati huohuo,ama unaweza kuishi nyakati tofauti kwa kufumba na kufumbua, ) na kama itatokea ukafanya jambo au kitu kufanyika juu yako na ukaamini 100% sio la kweli au likaleta mshangao wa kutolielewa wala kufikirika ni lazima utashituka/kuamka, kwa mfano labda unaota unakimbizwa au unataka kufa nawe ukakinzana na hiyo hali je hujikuti umeshituka ghafla usingizini!?

Kwa mtazamo na fikra zangu maisha halisi yapo katikati ya maisha haya tuliyonayo hapa jf na maisha ya ndotoni, leo usiku ukilala au kwa wakati wako wowote utakaoamua kulala ile hali itakayokuwepo katikati baada ya kuuacha huu uhalisia wa jf na kabla hujaingia ndotoni mi ndio fikra zangu zinanituma hayo ndio maisha halisi
 

Unajua mtu unaweza kuota ndoto kwa nafasi ya mtu mwingine, sasa kwa vile hujui unazani ni wewe ni mpaka utulie ndio utajua kuwa hukuwa wewe, sasa hiki ndicho ninachokiona kwako wewe, na ndio maana imekuwa rahisi kuota mwaka ambao ulikuwa bado haujazaliwa, na pia ndio maana yule mtu alisema hakujui japo wewe umjua, kwamba mwili ni wako wa sasa lakini kumbukumbu ni ya mtu mwingine.

Sasa swali la kujijluliza ni nani huyo ambaye umechukua taarifa zake na kwa nini?

Ebu jaribu kujiuliza huko kwenu huo mwaka wa 1973 kulikuwa na tukio gani? Uzuri yule mzee uliyemuona kwenye ndoto bado hupo nenda kamuulize kuna tukio gani lilitokea kipindi hiko si vibaya ukamuelezea hiyo ndoto yako.

Ila mwisho wa siku Mungu ndio mtafsiri wa kweli wa ndoto, usipopata ufumbuzi wewe muulize Mungu muumba atakujibu hata kama unazambi.
 
inawezekana kuwa kweli labda kachukua nafasi ya kaka/dada,baba/mama,mjomba/shangazi,babu/bibi, kama si je rafiki basi ni adui, swali ni kwamba ktka hii ndoto yeye uhusika wake ni upi!? maana kufikia hatua ya yeye kuota ndoto hiyo inawezekana anahusika pia au kuna bond fulani kupitia fulani katika hiyo ndoto, je ni kwanini yeye aote hiyo ndoto na sie mhusika mwenyewe!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…