Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 36,007
- 108,554
(Picha ikionyesha Warmhole na Nyota mbalimbali)
Salute Comrades.
Kwa references ya vitabu vya imani za dini mbalimbali zinasema kua hapo zamani Mungu aliumba ulimwengu, akaumba vyote vilivyomo ndani ya siku sita. Upande wa tafiti za kisayansi zinasema kua hapo zamani miaka billion kadhaa iliyopita kulitokea mlipuko mkubwa huko angani ambao wanauita The big Bang, mlipuko huo ulipelekea kutengenezwa kwa sayari na kuleta uhai wa viumbe mbalimbali kwenye sayari hizo (Earth) kupitia Evolution. Mimi ni muamini sio mwanasayansi, hivyo mada yangu itaegemea kwenye imani kwa kiasi Fulani.
Inasemekana Mungu aliumba kila kitu ndani ya siku sita tu na kukabidhi yote aliyoyaumba mikononi mwa mawanadamu (Kiumbe wake pendwa zaidi). Moja kati ya vitu ambavyo vitabu vya imani havielezi kama viliumbwa na Mungu ni MUDA, hakuna sehemu yoyote utakuta wameeleza muda uliumbwa, lakini logically muda uliumbwa.
Fundamental physical quantinty inasema kwamba SI-unit ya muda ni Second, minute,year,months etc. Ili muda uwepo inatakiwa kuwe na solar system, katika soler system sayari zinazunguka jua..zinapozunguka jua tunapata matokeo ya musiku na mchana. Katika usiku na mchana huo ndio tunaweza hesabu sekunde,dakika mwezi au mwaka. Jua ndio linasababisha ruweze kuhesabu muda au tuseme kwamba ndio inafanya existence ya muda. Since jua likizima basi muda utapotea pia uhai wa viumbe vilivyopo kwenye dunia unaweza kuwa extincted/toweka. Jua limepewa dhamana ya kushikilia uhai wa viumbe vilivyopo kwenye sayari hizi (Earth), ndio maana baadhi ya jamii huabudu Jua wakiamini ni Mungu,wengine huenda mbali zaidi wakisema kua hallo ambazo zimechorwa kwenye picha ya yesu ni jua..Hallo ni dura ambalo lipo juu ya kichwa cha picha ya yesu ikimaanisha “Aliye mtakatifu”
Time Apocalypse
Ushajiuliza inakuaje hasa mpaka mtu anakufa?ushajiuliza kwanini wanasema muda utatuambia?au time is a healer? Ipo hivi. Kuna vitu vikuu vitatu ambavyo ndio huleta athari either chanya au hasi katika maisha ya mwanadamu vitu hivyo ni Nature,subconscious mind na Time. Subconcious mind ni shemu kuu ya mind ya mwanadamu ambayo inaratibu taarifa zote zinazohusu mtu husika katika nafsi/soul yake, nature ni mazingira haya tunayaishi, na muda sasa ndio husimama kama hakimu katika kufanikisha mambo yaliyoratibiwa na subconscious mind na mind, hivi vitu vitatu vinafanya kazi simultaneously.
Kwa mfano Moja ya Law of nature ni kua Kila binaadamu lazima afe, so mtu anapokaribia kufa muda ndio huwasiliana na subconscious mind, kisha S mind inaiambia nature kua muda umefika wa mtu huyu kuondoka..nature sasa itakachofanya itachagua aina ya kifo anachotaka muhusika aondoke nacho kutokana na mazingira /hali i/aliyopo. Watu husema muda utatuambia/muda utatupa majibu tuwe na subira kwakua wenyewe ndio hua amua ni wakati gani kitu Fulani kilichoombwa kitokee.
Kuna watu hua wanajiuliza kwamba je unapomuomba Mungu mambi yako yeye huyajibu moja kwa moja au lah? Ukweli upo hivi kuna mambo amabayo Mungu hushughulika moja moja lakini pia yapo mengi sana amabayo huyashughulikia bila yeye kuhusika nayo directly. Mungu alichofanya aliweka kanuni zake amabazo huratibu kila maombi na matakwa yetu yote. Subconscious mind,Nature na Time ndio vitu vinavyoratibu matakwa yetu mengi vikiwa vimewezeshwa na Mungu. Iko hivi unapohitaji kitu mind inakipeleka kitu kile kwa Time, Muda sasa ndio unaamua kitu kile kikufikie kwa wakati gani.
Kwa mantiki hiyo kila kitu kinachotokea maishani mwako ni muda unakua umeamua kitu hicho kikutokee kwa wakti gani. Vile vile kitu pekee ambacho kinafanya kila binaadamu afariki ni muda, muda ndio chanzo cha kifo tukiweza kuudhibiti muda basi tunaweza kudhibiti kifo. Kuna wengine husema kua miaka 1000 duniani ni sawa na siku 1 hapa duniani, hicho kitu ni uongo uliotuka mbinguni hakuna Muda. Muda ili uwepo inatakiwa kuwe kuna sayari zinazunguka jua, mbinguni Mungu hua anawasha taa ikifika usiku kisa giza limeingia?hapana. Kwa Mungu hakuna muda, kama kuna muda basi Mungu atakufa malaika atakufa. In eternal dimension muda haupo ndio maana viumbe walioko huko huwa vile vile maisha yao yote, ndio maana ukifa leo ukafufuka baada ya miaka 50 utajua ulikua umefumba macho nano second kadhaa zilizopita maana kule hakuna muda. Kila kitu kipo Present hakuna future wala past ndio maana vitu vinaishi milele…ndio maana tunaambiwa tutachomeka motobi milele bila kufa maana hakuna muda kule…..So Muda ndio Controller wa hatima ya maisha yetu akiwa amepewa access hiyo na mwenyezi.
Time Heist
Wanasayansi na wanafalsafa wengi kama Einstein,Hawking,Tesla,Newton wamekua wakifanya tafiti juu ya nadharia za muda waone kama wanaweza kwenda beyond a time, wakagundua kwamba muda ni mwendo kasi (Speed) hivyo basi kama wataweza kuwa na speed kubwa basi wanaweza kuutawala Muda. Inasemekana kitu chenye speed zaidi duniani ni mwangu, hivyo kama tukiweza kutengeneza kitu chenye mwendo kasi zaidi ya mwanga tunaweza kuumiliki muda (bending/manipulate). Hapa sasa ndipo linakuja suala la time Traveling
Einstein- Rosen Bridge(warmhole)Hili ni tundu lenye muundo wa kipande cha pipe chenye pande mbili ambazo zinatenganisha muda. Mfano pande/point A inaweza ikawa ipo Tanzania ambayo kwenye point hiyo inaonyesha ni mwaka 2020 halafu pande B inaeza kua Kenya ambapo muda wake unaweza kua ni 2015 au pande hizo zinaweza kua sehemu moja au zikawa na muda unaofanana. Warmholeinaeza kuunganisha vitu vilivyo umbali mrefu kama miaka billion ya mwanga/light years , umbali mfupi au universe moja na nyingine ndani ya muda mfupi tu. Labda unasafiri sehemu yenye umbali wa miaka 500 ndani ya dakika kadhaa, ndio maana ukirudi kule ulikotoka utawakuta wale uliowaacha wamezeeka au wamekufa. Humu kuna masuala mengi ya kisayansi ambayo nikielezea nitawachanganya mliosoma General relativity theory mnaelewa Einstein Field Equation (EFE) mambo ya Gab = KTab Au Cosmological constant Gab + Agab = KTab (tumia Web ndio zitaonekana vizuri)
Kwakua kifo kinasababishwa na muda na muda unaathiriwa na Speed basi ili tukidhibiti kifo inabidi tuuudhibiti muda kwa speed,Hapo ndipo Time travelling inakuja kuchukua nafasi yake. Ili Time traveling (kwenda mbele ya muda au kurudi nyuma ya muda) ikamilike inahitaji chombo cha kusafiria ambacho ni Time Machine. Time machine ili ifanye kazi inabidi kuwe na warmhole, hapo sasa ndio wanasayansi wanaumiza vichwa ni kwa namna gani wataweza kutengeneza Warmhole ili ku-power up time machine.Time traveling inaweza kufanyika spiritually, physically au mentally. Wengi wetu hapa hua tunafanya mental time travelling na baadhi hufanya mental time travel, si ulishawahi kwenda sehemu ukahisi labda hilo eneo ushafika kila tendo linalotendeka unaona kama liliwahi tokea..Hapo unakua ulifanya spiritual time travel bila kujijua roho yako iliwahi kufika bila wewe kujijua, nyie mnaita Dejavu.
Kitu kinachoumiza kichwa ni jinsi gani watafanikisha physical time travelling mtu aweze kwenda zake mwaka 2025 huko akwepe Corona,au arudi 2015 huko. Tukifanikisha timetravellingi itakua ni mwendo wa kukwepa incident zinazopelekea watu kufa..Mtu akifa unaswitch muda unarudi nyuma Yule mtu aliyekufa unamuepusha na ile incident iliyopelekea kufa.
Wanasayansi wengi hasa Stephen Hawking wanasema time travelling haiwezekani, na watu humu JF wanaamini kabisa hua naona wanaongea hivo. Wanasahau kua ubongo wa mwanadamu ni Infinity yaani hauna ukomo, ukomo wa bongo wa mwanadamu upo kwenye baadhi ya vitu Fulani umekua disabled kuweza kungamua vitu hivyo kama Usingizi,maisha mtu akifa,Mungu yupoje na mengineyo. Mwanadamu ana uungu ndani yake kutokana na pumzi aliyowekewa kutoka kwa muumba wake ndio maana anaweza kufanya big invetions kama zote hizi tunazoziona duniani. Kama Stephen hawking alihjaribu akashindwa basi haiamanishi kua Time travelling haiwezekani, yeye hakua mwanadamu pekee na wa mwisho ambao wanaakili kuliko wengine. Ipo siku natumani atatokea giant mwingine katika kufikiria aje approve wrong maneno ya wanasayansi walioshindwa time travelling (Naweza kua hata mimi nikipewa nafasi)
Mimi fikra zanituma kua hichi kitu ni real na inawezekana kuna watu wanafanya hii mambo kwa manufaa yao wenyewe ndio maana mtu anaweza kutabiri vitu tata vitakavyokuja mwaka Fulani, au wanafanya Dark Prophesying? Inawezekana wanasubiri muda watakaoona unafaa waje wailete kwetu nasi tuitumie. Kama tutaweza maana hata 4G tumeshindwa kuimudu ipasavyo.
-Unworthy, Useless
~Da’Vinci
