Timbwilitimbwili la uwakilishi Zanzibar na tuhuma za uchawi

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
20,057
23,510
13015375_774091929393603_2231463446600311603_n.jpg



CUF wameturoga.

Kuna usiri mkubwa ndani ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Lakini pamoja na usiri huo leokuna jambo lililokuwa limefichwaMwenyezi Mungu amelileta hadharani. Kumbe wawakilishi wanaoaminishwa kuwa ni halali ,wana madhila yanawapata barazani huko.

Leo Mwakilishi wa viti Maalum wanawake bibi Mwanaidi Kassim Mussa alipelekwa uwanja wa ndege Zanzibar kwa ajili yakusafirishwa kwenda Dar es Salaam kwa matibabu. Njia nzima alikuwa akipiga kelele kwamba, "CUFwameturoga, CUF wameturoga,kila siku tafrani barazani, juzi wenzangu wawili wamepandisha shetani na baadae kuanguka, leo mimi hali ndio hii,CUF wachawi siutaki tena uwakilishi" alimalizia.

Alipoingizwa ndani uwanja wa ndege hapohapo akazimia. Amesafirishwa saa nane mchana huu kuelekea Dar kwandege ya "AURIC AIR".Mungu amjaalie apone arudi kuwatumikia waliomtuma.
 
Sasa wasubiri tetemeko la uzani wa 9.99..kila wawapo kwenye ukumbi wa baraza la uwakilishi.
 
Yaani waache kuroga wahusika wawaroge wawakilishi wa kuteuliwa? Aache mawenge huyo.
 
Back
Top Bottom