KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 35,747
- 86,378
Assalam alyeikum mabibi na mabwana..?
Bila kuwachosa njoga niwape kisa hichi kilichonikuta, waswahili wanasema ujana maji ya moto sasa mimi nilikutana na moto wenyewe!.
Ilikuwa ni usiku tulivu nikiwa nimejituliza baada ya mihangaiko ya hapa na pale, punde mlango ukabishwa nikamkaribisha mgeni wangu, alikuwa ni jamaa anakaa jirani na ndio kwanza alikuwa amekuja kunihabarisha kuwa kuna jambo linanihusu na mimi ndo naonekana kuwa mtatuzi!.
Alikuwa ni kijana wa umri kama wangu baada ya salamu swali la kwanza aliloniuliza lilinistaajabisha!, "unamahusiano na Hanifa..?" ambae huyo hanifa ni mdogo wake!, nilistaajabu kwa yeye kuniuliza swali kama hilo, pili sikuwahi kuwa namahusiano na mdogo wake huyo!.
nikamjibu hapana na hapohapo nikamuuliza kwanini...?
Akavuta pumzi halafu akanitazama kwa tuo!, kisha akawa kama anataka kusema kitu akasita!!.
Mimi hapo nikaanza kuwaza "tayari wahuni wamesha mmimba hanifa wa watu!" sasa mimi hapo naingiaje!.
wakati nawaza hivyo kaka mtu akaendelea..
Leo mchana hanifa alipandisha maruhani!!, na maruhani yenyewe yalikuwa yanakutaja wewe!, yanasema kwamba yamevutiwa na wewe!.. tokea hiyo mchana mpaka sasahivi huko nyumbani hapakaliki ni yanashuka nakupanda, navyokuambia sasahivi yameamka tena na wazee wameniambia nikufuate!.
baada yakusikia hivyo nilimeza mate yakawa hayamezeki!, nikijiuliza mimi na maruhani wapi na wapi, hapohapo nikamfikiria huyo hanifa mwenyewe, alikuwa ni binti fulani hivi black beauty wa alfu mbili.. sura ya mdoli na sauti ya Abby!.
Sauti yakaka mtu ikanigutua tena
vipi nasubiri jibu lako!..
Nilisita kwa tuo kwanza, ye mwenyewe akaona sijaafiki kwenda!. aliusoma uoga wangu ulionekana dhahiri namimi nilimuangalia nikaona uso wake ukiwa na huzuni!. na huyo ndo alikuwa mdogo wake pekee maana walizaliwa wawili tu!.
kwa mara nyengine akaniomba walau niende hata nikamuone uenda hayo maruhani yakatulia!.
Kwa shingo upande nikajivuta hapo yeye akiwa ameshatangulia nje, nikatungua tisheti nikajivika maana nilikuwa kifua wazi huyo mguu wake mguu wangu na hapakuwa mbali ni umbali wa mita kama 50 tu toka ninapokaa!.
Nikaingia ndani sebuleni nikawakuta wazee wake wakiwa wamesawajika hoi taabani kwa kuyatuliza majini!, nikawasalimia nakuwapa pole ila alieitikia alikuwa na mama, mzee alionyesha sura ya makasiriko ni kama vile hakuwa na namna!, akaniangalia juu mpaka chini na asinimalize!.
Hawakutaka kuzungumza sana wakainuka nakushika korido iliyokuwa ikielekea kwenye vyumba!, mlango wakwanza tukapita wapili pia, watatu mama mtu akawa wakwanza kuufungua na ndipo wakanikaribisha!.
picha yakwanza niliyoiona ilikuwa ni kitanda ambacho juu yake alikuwa ameketi hanifa kwa kunyoosha miguu!, huku akiwa ameinamisha kichwa na kutikisatikisa kichwa!, ile naingia nilipokelewa na harufu ya udi nikajisemea moyoni "Leo namba itasomeka tu!".
kwa mandhari chumba kile kilionekana kutokuwa kwenye mpangilio maana yake kulikuwa na purukushani, nikawaza wao watatu hivi mimi mmoja nitayaweza...? nilijiuliza!.
wakati nikishanga baba mtu akanivuta kwa nyuma nakuniuliza swali lilelile aliloniuliza mwanae hapo awali..!
"unahakika huna mahusiano na mwanangu..?".
Nikamjibu kwa ku nod kichwa mara mbili!. mzee akaniachia wakati sielewi hili wala lile mama mtu akaniambia "mwanangu keti hapo kitandani!!..
Nilitamani niseme "toba!" lakini nikaona nitaharibu!, taratibu na kwa umakini nikaketi huku nikimuangalia hanifa ambae mpaka wakati huo alikuwa bado ameinamisha kichwa!..
punde kidogo mama mtu akamuita "hanifa..?" hakuitika "hanifa..?" hakuitika tena ila taratibu akainua kichwa chake!.
nywele zake nzuri zilikuwa ktk rafu, na hata macho yake yalikuwa mekundu kiasi japo hayakufanikiwa kuufunika ule uzuri wake ambao ulilandana na uzuri wa mama yake!.
Mama aliendelea..
"Tumewaletea mtu wenu!"
Nilitamani niseme sii mimi lakini mdomo ulikuwa mzito!, hapo mapigo ya moyo yalikuwa yakienda mrama maana hanifa alikuwa amenikazia macho kiasi chakuogopesha!.
sote tulikaa kimya tukimuangalia ila tofauti wenzangu walimuangalia mtu ambae hawaangalii, ila mimi macho yake yote pasipo kupwesa yalikuwa kodo kwangu!..
ilipita dakika kama tatu akinitazama!, kisha akainua mkono wake wakulia nakuanza kuusogeza kwangu akiuendea mkono wangu wakushoto!.. alipoufikia aliushika nakuanza kuniminyaminya taratibu kwa vidole vyake!.
Niliogopa ila mama yake akaniambia usiogope mwanangu!, nikajisawazisha kama mtu naetafuta pozi zuri la comfortability!.
akiendelea kuupikicha mkono wangu dakika hiyohiyo machozi yakaanza kumtoka!.
Nikaona hii sasa mbona inataka kuwa filamu ya kifilipino!, nikaanza kuona kama mchezo fulani hivi hii familia wanataka kunichezea wanipe jiko bila ridhaa yangu!..😂
punde hanifa akaanza kuongea kwa kuita jina langu ila sauti yake haikuwa ile niliyoizoea!, ilikuwa ni sauti yenye mikwaruzo fulani hivi!..
ile hajamaliza nikashangaa kwa spidi ya hatari akinikwida!, hapo sasa nikajua tayari namezwa sasa!..
nikawa namsukuma aniachie mama yake nae akaingilia kati huku baba mtu na kaka mtu nao wakaingilia wakinivuta kuniondosha!..
kusema kweli lile picha lilibadirika kwa mara moja pasipo kutarajia!, watu tuliokuwa tumeketi kwa amani sasa ilikuwa imetangazwa vita!, vita ambayo binafsi sikujua nani jambazi na ni nani sterling!.
Mnyukuano ulikuwa ni wa haja binti na maruhani yake alikuwa ananguvu mithiri ya mpiganaji mieleka!..
si baba, mama wala kaka yake wote walionekana kuelemewa ktk kuninasua!, alianza mpaka kuinuka! hivyo mimi nikawa naenda chini yeye anakuja juu!.
hapo ndipo nilijua "binadamu hadaa ulimwengu shujaa!".
Sasa katikati ya hali kama hiyo likajitokeza jambo ambalo walahi nalilaani mpaka leo!. imagine katika mnyukano kama ule na viumbe ambao sijui hata wanatoka sayari gani, wale mabwana wenye usemi "tunayaangaza maisha yako!" wakaamua kuuchukua mwangaza wao!, hivyo disko likawa limeingiliwa na wamasai!. lile giza sio tu lilinihadaa mimi hata waliokuwa wananisaidia nikaona wamezuzuka!, ila kwa maruhani ilikuwa kama ni sherehe maana yalianza kutoa ukelele mkali huku yakiongeza nguvu yakunikandamiza!.
ile hali iliwatisha wasaidizi wangu hivyo kila mmoja alikuwa akikiacha chumba kile ktk namna ambayo nilikuwa nikisikia vishindo tu!, punde nilibaki mimi hanifa na viumbe vilivyokuwa ndani ya hanifa!!.
nilitamani kutoa chozi lakini nani angeniona na lile giza..?
nilimshika mikono kujihami nikajipepesa mara ya kwanza akakaza!, mara ya pili pia akakaza mara yatatu ikabidi nijiviringishe!, hivyo nikatahamaki nashuka nae kwenye kitanda mzima mzima mara puu!, tukaanguka kwenye sakafu kama furushi la mihogo!, hapohapo akawa ameniachia uzuri mimi ndo nilikuwa karibu na mlango japo nilikuwa siuoni!, ile najivuta niuendee mguu wangu ukashikwa!.
nikapush kama napiga teke kwa nyuma!, mguu ukaachiwa si nikajua nimewin kumbe ulipoachiwa huo ukashikwa mwengine!, mpaka nikajiuliza "anaonaje huyu na hili giza..?!"..😂
akawa kama amenisoma akajua na wenyewe nitapush kama wa awali na kweli nika push akauacha kumbe mara hii amenisogelea zaidi alivyouachia mguu nikasikia napapaswa kiuno!, kusema kweli hapo niliachia welelo ambao sijui ulitoka wapi! bahati nzuri alikuwa ameshikilia pensi niliyokuwa nimevaa nikaona hapa afe kipa ama beki mimi nayeya!.
ile pensi ilikuwa ni nyepesi namimi mikono ilikuwa imeshafikia mlango hivyo nikajivuta kwanguvu nikasikia tu "chaaaaa" pensi likitatuka na huo ndo ukawa uhuru wangu japo ndani sikuwa nimevaa boxer lakini haikuwa tabu nilimuachia li pensi lake limliwaze huko!.. hiyo ndo ilikuwa bahati ya mkenge niliponyoka nikiwa uchi!!.
ile nafika sebuleni na umeme nao ukawaka hapo ndo kizaizai chengine kikaonekana!, mgeni nilikuwa nakiwasha nduki huku malighafi zikiwa on air!, majirani kadhaa waliokuwa karibu walishuhudia soko langu la hisa la mbele likinepanepa huku mimi nikiwa sina habari mpk nilipofika ninapokaa nikiwa hoi!.. japo asubuhi nilivyokuwa naenda kazini kuna dogo wa kama miaka mitano hivi sikupenda swali lake ati "anko kwanini wewe unakitovu kikubwa..?!" sikumjibu nilitabasamu tu huku nikimuahidi nitamletea pipi!.
kufupisha stori kumbe familia yake ndo walichanganya!, yale maruhani walikuwa wanamuhitaji mpenzi wake na hanifa ambae wao walikuwa hawamjui ila jina lake lilikuwa linafanana na langu!, so wao wakajua ni mimi na ndio maana yalinibadilikia ila yote kwa yote niliamua kusamehe bure japo nilidharirika sana!.