Timbwili la JKT

Mkuu pamoja na hili nafikiri kuna umuhimu wa kushauri vijana wetu kuachana na vyakula kama chipsi maana madogo siku hizi ni nyolonyolo mon!

unajua wakati ule tuliposoma sekondari sisi masikini tuliamini kula mihogo ni ushujaa na tuliwaponda sana watoto wa kishua kula chips mayai , kumbe ilikuwa ni ulofa wetu tu !
 
Isije kuwa mtambo wa kuzalisha vikundi vya uasi kama M23

Ni suala la kuweka vipaumbele tu na kuhakikisha wanakuwa absorbed na sectors za uzalishaji, vyuo vya kati viongezwe, riba zipunguzwe,ajira ziwepo kwa wenye uwezo bila nepotism, na vyombo vya ulinzi na usalama viimarishwe zaid ili kuwa na mkono mrefu,pua safi, masikio makubwa na ngozi safi na yenye afya ili kuhisi kwa haraka!!!!

Rasilimali zifaidishe wengi na mfumuko wa bei udhibitiwe!!!!

Umetoa angalizo zuri sana, semi trained are more dangerous when it comes to bad moods!!!!
 
Mkuu sasa chanzo cha vifo vinavyotangazwa ni nini, au ni uzushi tu?

mkuu kwa suala la vifo mara nyingi hua ni magonjwa ya kawaida kama ilivyo kwa vifo vingine, na ndio maana ukiangalia OP:MIAKA 50 YA JKT interk ya pili (july-sept) kambi iliyoongoza kwa mazoezi makali ni 824 KJ kanembwa jkt KIBONDO-KIGOMA lakini hakuna aliyekufa hata mmoja,, mimi niwasihi watanzania wenzangu kwamba vijana wako salama na wanaendelea vizuri, nilichogundua ni kuwa watu wanakuwa na wasi wasi juu ya usalama wao kwa sababu hakuna mawasiliano. tuwaombee vijana warudi salama
 
Niambieni nia hasa ya JKT. Ajira, nidhamu, jeshi la akiba, mshikamano, afya bora au nini??? Na je Ni nani ndo wahudhurie? Kuna mambo mengi sana ya kujiuliza. Au la sivyo Ni kupoteza muda tuu. Mantiki ya Hilo zoezi siioni.
 
View attachment 169905
Wana JF, inasemekana hii ni moja ya picha ioneshayo mazoezi katika kambi za JKT. Je, hii inaweza kuwa chanzo cha malalamiko ya watu kuhusu maafa yanaosadikika kutokea huko au ni siasa za watu tu!

Hapo bado hajapigwa 45 minutes extra drill ! jeshi lazima ugangamale !
Bahati nbaya humiu wazazi wengi wenye miaka kati ya 35 mapaka 42 hawajapita jeshini, na hao ndio mabingwa wa majungu !
Tafuta movie moja inaitwa Full Metal Jacket uone drills humo !
 
Yaani hilo ndo jeshi... Jeshini hiyo ni kawaida sana...
 
Haya Ni mazoezi ya wiki ya kwanza,hamna kitu hapo.Acha kuwalea watoto kimayai mayai,nyie ndo mnatuharibia nchi.
 
mbona hawa kama wanapiga picha za kutupia whatsup na fesibuku
 
Sasa nyie mlifikiri Jeshini wanaenda wanachat.?
 
Wapi huko majasiri wanatolewa posa? Madogo mkisia JKT uharo mtupu,alafu mnashabikia vita na majirani!!
Ngoja wakikutolea posa wewe ndio utajua wapi.

JKT na vita wapi na wapi?je kila nchi duniani ina JKT?

Kama wanataka ku-recruit wanajeshi ili kujiandaa kwajili ya vita basi watangaze ajira,uone jinsi gani wengi watakavyoenda kwa ihari.

Kama wanataka watu wafunzwe ukakamavu basi kiwekwe kiwango cha mafunzo kama ilivyo kwenye elimu na mafunzo mengine.

Ni ujinga kujiumiza kwa kung'ang'ania mambo ya mwaka 47 wakati mambo ya leo ni marahisi na yanaepusha hatari za maisha.JKT ni ushenzi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…