Tii Sheria bila Shurti ifundishwe Shuleni!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kama kuna jambo ambalo nampongeza Mkuu wa Polisi aliyepita S. Mwema ni kwenye hii kauli mbiu ya utii wa sheria bila ya shurti sina uhakika kama ni ya kwake au ilikuwepo na yeye akaamua tu kuitumia lkn ni kauli ambayo ni muhimu sana kwa ustawi wa jamii yoyote ile hapa Duniani!

Moja kati ya changamoto tulizonazo kama jamii ni swala la utii wa sheria, tunapata matatizo mengi kwa kutokutii sheria bila ya shurti kwa mfano mtu anasababisha ajali halafu anakimbia, hata huyu boda boda aliyefariki leo hii kama angeelewa maana ya kutii sheria bila ya shurti si ajabu mauti yasingemkuta kwani angetii Amri ya askari wetu, hivyo napendekeza hili liingizwe kwenye mitaala yetu shuleni ili watoto wafundishwe tangu wadogo maana ya kutii sheria itatusaidia sana!


Hata watu wanaojenga pasiporuhusiwa moja ya sababu ni kutokuuelewa utii wa sheria bila ya shurti, Mafisadi wengi pia kutokuelewa utii wa Sheria bila ya shurti, hata Wabunge wa chadema kama wangefundishwa tangu watoto jinsi ya kutii sheria bila shurti kungekuwa hamna haja ya kuleta askari wetu Bungeni kwani wangemuelewa Mkuu wa Bunge na kutii aliyosema hivyo kwangu mimi shida kubwa nchini mwetu yetu kama jamii iko hapa, kwenye kutii sheria bila ya Shurti!!
 
Back
Top Bottom