Tigray: Chakula cha Misaada kuisha wiki hii

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) limeonya hatari ya kuisha kwa chakula cha misaada kuanzia wiki hii katika eneo la mapigano la Tigray nchini Ethiopia.

Zaidi ya watu 900,000 wapo katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa ikiwa ni kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miezi tisa ya mapigano kwa taasisi za kibinadamu kuishiwa na chakula cha misaada. USAID imesema kuwa uhaba huo wa chakula hausababishwi na kukosekana kwa chakula, lakini ni kutokana na serikali ya Ethiopia kuzuia chakula cha misaada kufika katika eneo la mapigano.

Mapigano katika eneo hilo baina ya vikosi vya serikali ya Ethiopia na Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) yamesababisha vifo vya maelfu ya watu huku zaidi ya watu milioni 500 wapo katika uhitaji wa misaada ya kibinadamu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ametaka kusitishwa kwa mapigano katika eneo hilo, akionya kuwa zaidi ya watoto 100,000 wanaweza kufariki kwa njaa.

Ili kufikia mahitaji ya watu katika eneo la Tigray, malori 100 yenye chakula na misaada muhimu yanatakiwa kufika kila siku katika eneo hilo, lakini ni malori 320 tu yamefika ndani ya siku chache zilizopita, ikiwa ni chini ya 7% ya mahitaji yote ya eneo hilo, kwa mujibu wa USAID.

Msemaji wa Serikali ya Ethiopia amepuuzia madai hayo ya USAID akisema serikali yake inaangalia zaidi suala la usalama katika eneo hilo.

Chanzo: Reuters

1629703491270.png
 
Back
Top Bottom