Tigopesa,Airtel money na Mpesa

Dhwahiri

Member
Jun 20, 2016
16
5
Naomba ufafanuzi namna ya kupata line hizo Na faida zinakuwa vipi kwa mfano ukiwa unamtaji wa 1,000,000 Na Unao wateja wakawaida wakutoa Na kuweka kwa mwezi commission unaweza pata kiasi gani?.
 
Hizo laini zinapatikana bure,
Unatakiwa uwe na Kitambulisho, passport size 2, leseni ya biashara na TIN no.
Nenda tigo shop, airtel shop, vodashop au halotel shop.
Utasajiliwa laini na utatengenezewa TILL hapo hapo,
Fuata taratibu ili upate vitu halali,
Hii pia ni kwa usalama wa pesa zako!!
Kumbuka kutumia laini za "magumashi" ni hatari kwa usalama wa pesa zako. Mwenue details za usajili anaweza kwenda shop akaswap hizo laini zako na usiwe na mahali pa kulalamikia..
 
Kuhusu faida inategemea na mzunguko wa wateja, ukifanya kazi sana utapata faida kubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom