'Tigo' wasababisha Ajali Kariakoo na kuua

'Tigo' wasababisha Ajali Kariakoo na kuua

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,096
Habari ya kusikitisha..

MTU mmoja amefariki dunia asubuhi hii baada ya kugongwa na Lori kichwani maeneo ya Kariakoo jijini Dar es salaam.

Chanzo cha ajali hiyo ni Polisi wa doria barabarani (maarufu kwa jina la 'tigo') walipokuwa wakijaribu kuwafukuza Madereva wa Pikipiki (Bodaboda) ambao nao walimsukuma kijana mmoja mtembea kwa baiskeli hadi barabani na kugongwa na Lori hilo.

Picha za tukio ninazo nyingi, ila zinatisha sana (Hazifai kuwekwa humu).

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema!

R.i.p, baada ya yule jamaa colman kimaryo kukamatwa na kufikishwa lupango" saizi watu hawatukani polisi ovyo, wameshika adabu yao,
 
badilisha kichwa cha habari yako tumia neno tigo kwenye mabano..
 
Waliosababisha ni tigo au bodaboda!!!!!!!.

Kwani polisi wanatisha kiasi gani mpaka unakimbia hata huangalii mbele!!!R.I.P kijana mpita njia.

Hivi hata wangekufa hao bodaboda ungesema tigo ndio wamesababisha!!!!????
 
Interest

Usiziweke tafadhali mkuu.
Watu wenye roho nyepesi tupo wengi sana.
RIP aliegongwa na gari.
 
Last edited by a moderator:
Hivi inakuwaje unaanza piga picha za habari
 
Habari ya kusikitisha..

MTU mmoja amefariki dunia asubuhi hii baada ya kugongwa na Lori kichwani maeneo ya Kariakoo jijini Dar es salaam.

Chanzo cha ajali hiyo ni Polisi wa doria barabarani (maarufu kwa jina la 'tigo') walipokuwa wakijaribu kuwafukuza Madereva wa Pikipiki (Bodaboda) ambao nao walimsukuma kijana mmoja mtembea kwa baiskeli hadi barabani na kugongwa na Lori hilo.

Picha za tukio ninazo nyingi, ila zinatisha sana (Hazifai kuwekwa humu).

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema!

Ziweke bana
 
Back
Top Bottom