Tigo Tanzania Haithamini Wateja

Sita Sita

JF-Expert Member
Aug 25, 2008
1,397
519
Uongozi wa Tigo

Naomba kuweka wazi kwamba ninasikitika sana kwa jinsi mnavyotatua kero za wateja wenu. Nimekua mteja kwa zaidi ya miaka 10 lakini kila mara nikipata tatizo na kuongea na watu wa huduma kwa wateja nashikwa na hasira sana. Hao watu wenu wa back office wanaohusika na kutatua kero zetu wana matatizo na ni vyema mkawatumbua jipu.

Sitaweka wazi yaliyonikuta ila nitaendelea kuwachafua mpaka mshike adabu yenu. Bila wateja nyie tigo si lolote na bila kututhamini tutawaacha na milingoti yenu.

Nimepiga simu customer care kwa siku 4 mfululizo na kila siku naambiwa tatizo lako litashughulikiwa in 24 hours. wapuuzi wakubwa xxuuuu.

Kama hamuwezi kutatua msitoe ahadi za maudhi alaf baadae mnaishia kuomba msamaha. Mi naingia hasara na kuonekana si mwaminifu kwa sababu ya uzembe wenu. Tuheshimiane nyie watu.

Ikifika j3 naenda TCRA kupata muongozo wa kudai fidia na lazima nihakikishe back office wanatumbuliwa.

# TigoMnaudhi
 
Laini yako ulisajili kwa vitambulisho vyako?
Kama ulipiga namba 100 kueleza tatizo lako hebu piga namba 150.
Ahsante kwa kuchagua tigo Endelea kutumia huduma za tigo.
 
Jamani tigo badilikeni basi mimi leo toka asubuhi hamtaki kuniunganisha 4G na kusababisha kukosekana hewani siku nzima ofisi za Mwanza wanasema makao makuu hamtaki kufungua access!
 
Back
Top Bottom