Tigo pesa wamehold pesa yangu zaidi ya masaa 48

naisha nasri

Member
Apr 25, 2016
67
64
Ladies and gentlemen

Naombeni msaada wa kisheria;Tarehe kumi na nne nilienda kwa wakala kutoa pesa kwenye akaunt yangu ya Tigo pesa.Nilipofika kwa wakala nikaendelea na mchakato mzima wa kutoa kahela kangu nilikobakiza kwenye akaunti yangu.Kuzingatia hali ya uchumi ilivyokua nikajaribu kuwa makini sana ilinisikosee kumbe ndo nakosea kweli kuingiza numba ya wakala nilipoenda kutoa pesa,nikakosea kuingiza numba ya mwisho.

Baada ya kugundua kukosea numba,muhudumu akanielekeza kupiga numba 100 kuwambia tigo kisa changu,Tigo bila kupoteza muda wakasema wamehold hiyo hela na nikaambiwa itarudi ndani ya masaa 24,baada ya masaa ishirini na nne pesa haikurudi ilibidi niwapigie tena na tena nikaambiwa nisubiri masaa 24.Pesa yangu leo hii bado haijarudi,nimewapigia Tigo wadada wananiambia swala langu bado ninashughulikiwa,nisubiri tena masaa 24.

Nisaidieni nifanyeje tigo wananizungusha kunirudishia hela yangu (hard earned money under this gvt)
Tigo are they doing business kweli?kwa nini wananisumbua?
 
Hahahahahaha Nenda na hizo numba za wakala kwenye ofisi za tigo
 
Ilishawahi kunitokea. Siyo jambo la ajabu sana pesa kukaa zaidi ya saa 24. Ya kwangu ilikaa zaidi ya siku 14 lakini nilirudishiwa (ingawa siyo justification ya hela yako kukaa muda mtefu).

Kwa uzoefu huo wangu, tatizo kama hilo linapotokea, TIGO lazima wawasiliane na wakala ambaye hela yako imeenda. Sasa kwa kuwa matukio kama hayo yapo mengi kwa siku, huwa inachukua muda mrefu kuhakikisha kuwa ni kweli hiyo hela imeenda kwa wakala wa pili kimakosa. Uharaka wa hela yako kurudi itategemea na ushiriakiano atakaoutoa huyo wakala wa 2. Wakala mwenye nia mbaya atafanya makusudi kutokupokea simu na hapo ndipo ucheleweshaji hutokea.

Kitu ninachoweza kukuhakikishia ni kuwa pesa yako iko kwenye mikono salama as long as umeshawasiliana na Customer Care. Lakini kama unaona inachukua muda mrefu jaribu kuwasiliana na ukurasa wa TIGO wa FACEBOOK. Kwa maelezo niliyoyapata kutoka kwa watu, njia hii inasemekana ni nyepesi zaidi kuliko ya kupiga simu, ambapo kila unapopiga simu anapokea mhudumu mwingine na hivyo inakubidi uanze kutoa maelezo upya kabisa.

Mwisho nikupe pole kwa tatizo lililokutokea, lakini nirudie kukuhakikishia kuwa pesa zako ziko kwenye mikono salama. Utazipata in due time.
 
Back
Top Bottom