Tigo iwaheshimu wateja wao

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Kitendo cha mtandao wa tigo kuwa na matatizo makubwa siku hizi (hasa Morogor), kuwa ukipiga simu haziendi, ukituma msg haziendi kwa wakati, ukiingiza vocha hazikubali, na matatizo mengine kibao ni vya muda mrefu. Cha kusikitisha siku zote hizo sijamuona Mfuru akijitokeza na kuomba radhi, na kusema tatizo litaisha lini. Huku ni kuwadharau wateja wake...
 
Hamia huku kwetu...........
 
express yourself
mdhamini wa chochote kile unachokipenda
kugawana ni kujali
usiache mbacho kwa msala upitao
 
Hamia huku kwetu...........

Tatizo ni kuwa gharama za kuhama ni kubwa kwani namab niliyo nayo inafahamika na watu wengi, na nimeiaddress sehemu nyingi. Hata hivyo, uwepo wa simu za kichina siku hizi unatusaidia kwani nakuwa na line 2, hii nyingine ndiyo ninayotumia mimi nikitaka kuwasiliana, ingawa nighali kwani watu wengi nina namba zao za tigo tu...
 
Huku Dar ndo kabisaaaa, ukitaka kupiga kwa line ya TiGo basi ujaribu kama mara 30 hivi ndo utafanikiwa, halafu inakata wala haikwambii kama simu iko busy au mtandao uko busy wala nini
 
Huna haja ya kulalamika wewe hama halafu wataarifu watu taratibu kuwa unatumia namba mpya. Mitandao mbona mingi kwa nini upate shida bwana?
 
hili tatio naona ni kubwa, hata huku sisi tulipo ni shida tupu...... na shoga yake zain pia mambo ni hayo hayo
 
Yaani imenikera hakuna mfano, mbaya zaidi nikituma meseji hazitoki halafu inakula hela more than normal rates yaani t's over 100Tsh na meseji inabaki kwenye outbox ambapo simu inastruggle to resend, kila ikiresend inakula hela. Nilikuwa na more than 2000 ikaisha bila kujua ndipo niliposhtukia!!! Aaaaarrrrrgggggg.... tigo mambo gani haya tena na ukipiga customer care haikubali vilevile. Itawacost wasipojirekebisha
 
Back
Top Bottom