Tigo cheap is expensive

Tigo cheap is expensive

french

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2017
Posts
3,636
Reaction score
3,834
Wakuu huu msemo wa cheap is expensive ndio umedhihirika na hii kampuni ya tigo. juzi j'2 nilinunua GB 15 kwa shilingi elfu kumi nikijua nitamaliza nalo wiki bila ya stess.

Cha ajabu mpaka leo hii ni GB moja tu ndio nimetumia. Mtandao ni mbovu sana network hamna almost masaa 22 kwa siku.

Network inakuja na kuondoka. Dah inshort hela yangu imeliwa bure sidhani hata kama nitamaliza GB3 mpaka Jumapili. Nimekoma sinunui tena kifurushi cha hela nyingi mtandao wowote ule.
 
Mbaya zaidi wanashindwa hata kutuma msg kwa wateja kuwaeleza kama kuna tatizo lakini message za mmbet wanatuma
 
We uko wapi, mm nimehamia tigo sina stress hata kidogo. Natumia elf 15 napata 100min all net, na 7 gb mwezi mzima
 
Mimi lilinikuta kwa halotel hatakufungua page inachukua muda, halafu baada ya masaa kadhaa wananitumia msg kuwa bundle limeisha, nilibaski nashngaa. Nikaona isiwe tabu nikarudi nyumbani voda japo vifurushi vyao bei ila bora nlipe pesa nipate huduma nzuri.
 
kweli mkuu wakati mwengine bora ulipe hela nyingi lakini upate huduma bora. tigo kwa sasa wanadhindwa hata na ttcl
Mimi lilinikuta kwa halotel hatakufungua page inachukua muda, halafu baada ya masaa kadhaa wananitumia msg kuwa bundle limeisha, nilibaski nashngaa. Nikaona isiwe tabu nikarudi nyumbani voda japo vifurushi vyao bei ila bora nlipe pesa nipate huduma nzuri.
 
Hiyo inakuwa Limited Speed. Yaani wanakupangia wao.
Hata Voda wana hiyo tabia ukinunua lile bando la elfu 20 Gb 20 unakutana na Limited Speed ila ukinunua bando la saa 24 Speed iko vizuri mno.
 
Tigo wamekuwa wa ovyo sana. WAHAME.
INTERNET OVYOOO
 
Mtandao unakuwa na kasi kutokana na eneo ulipo mara nyingi,sehemu nyingine kunakuwa na mnara wa mtandao husika hivyo network yake inakuwa strong lakini eneo hilo hilo mtandao wa simu nyingine unaweza kuwa dhaifu.

Pili ni aina ya simu unayotumia ni Original au fake au inatumia caverage mwisho 2G au 4G.

Lakin kiukweli mtandao wenye coverage nzuri ya internet na speed kwa hapa Tanzania ni vodacom na ikifuatiwa na Halotel au TTCl,hii mitandao iliyobaki ni mitihani tu
 
Mi sio mtoto boss muda mwingi natafuta hela kwa ajili ya familia yangu. Nyie mnaoshinda utube na whatsap ndo haziwatoshi
Usiseme hivyo mkuu, wengine ni mafundi simu upande wa software, binafsi natumia kima cha chini kabisa GB 5 kwa siku, na hapo ndo mtandao hauna spidi
 
Hiyo inakuwa Limited Speed. Yaani wanakupangia wao.
Hata Voda wana hiyo tabia ukinunua lile bando la elfu 20 Gb 20 unakutana na Limited Speed ila ukinunua bando la saa 24 Speed iko vizuri mno.
duh. kunbe ndio hivyo mkuu. lakini inakata kabisa,sometimes
 
Airtel 2.5GB zinanitosha kwa siku kama tano. Tigo hapa ina speed kubwa na inakula data kwa kasi. Voda siwezi logwa kwa bundle zake. Halotel speed yake hapa ndogo. Ttcl hakuna kitu.
 
Back
Top Bottom