Mkuu tpaul yawezekana ulipiga kuangalia salio kabla hata hujaanza kutumia dakika zako ulizozawadiwa. Ilikuwaje Mkuu? Pole lakini
Jana nimenunua laini ya simu ya mtandao wa tiGO, baada ya kuisajili nikatumiwa SMS ifuatayo:
Hongera! Umezawadiwa Dk 14 Tigo-Tigo, Dk 6 kwenda mitandao yote TZ, SMS 450 na MB 125 kwa kununua line ya Tigo. Tumia ndani ya masaa 24. Kwa salio piga *102*01#
Nilipopiga *102*01# nikapata ujumbe huu hapa:
Una sek 960 mitandao yote TZ, SMS 450 & 90MB hadi 12/07/2014.
KERO YANGU
Kupitia SMS hizi, mnaweza kushuhudia jinsi tiGO wanavyowatapeli wateja wao kwa kuwaahidi ahadi feki ambazo hazilingani na matangazo wanayoyatoa:
1. Mteja hudanganywa kwamba amepewa MB 125 kumbe amewekewa MB 90 tu! Huu ni wizi, uhuni na utapeli!
2. Mteja hudanganywa kwamba dk za ofa zimegawanywa, kumbe si kweli! Matokeo yake mtu akipiga simu analiwa fedha zake. tiGO acheni uti-GO wenu. Msiwafanye wateja wenu mafala kihivyo!
mkuu, ni baada ya kupokea SMS hii kutoka tiGO, hata kabla sijaanza kutumia yao, ndipo nikakutana na mauzauza hayo. yaani hawa tiGO ni matapeli usipime! najua wapo humu, naomba wajitokeze watupe ufafanuzi kuhusu uhuni huu wanaowafanyia wateja wao. halafu hata mtu ukipiga customer care hawapokei simu.
Kiboko ni smart park. Ukijiunga huko mara moja hata ukijitoa wanaendelea kukata 30000 kila mwezi. Nimeamini siweki tena salio linalozidi kiasi hicho kwani watakiiba hapo hapo
Kwa nini lakini umuandikie mwenzio hivi?Kosa gani katika thread yake ambalo limekukera kiasi hiki?Kama hao tiGo wanakuletea u-tiGo hadi unakuja kulia mitandaoni basi wewe ndiye mwenye u-tiGo kuliko hao tiGo wenyewe.
Jana nimenunua laini ya simu ya mtandao wa tiGO, baada ya kuisajili nikatumiwa SMS ifuatayo:
Hongera! Umezawadiwa Dk 14 Tigo-Tigo, Dk 6 kwenda mitandao yote TZ, SMS 450 na MB 125 kwa kununua line ya Tigo. Tumia ndani ya masaa 24. Kwa salio piga *102*01#
Nilipopiga *102*01# nikapata ujumbe huu hapa:
Una sek 960 mitandao yote TZ, SMS 450 & 90MB hadi 12/07/2014.
KERO YANGU
Kupitia SMS hizi, mnaweza kushuhudia jinsi tiGO wanavyowatapeli wateja wao kwa kuwaahidi ahadi feki ambazo hazilingani na matangazo wanayoyatoa:
1. Mteja hudanganywa kwamba amepewa MB 125 kumbe amewekewa MB 90 tu! Huu ni wizi, uhuni na utapeli!
2. Mteja hudanganywa kwamba dk za ofa zimegawanywa, kumbe si kweli! Matokeo yake mtu akipiga simu analiwa fedha zake. tiGO acheni uti-GO wenu. Msiwafanye wateja wenu mafala kihivyo!
Tigo humu JF wana tangazo tu la 'go crazy'. Hawana muda wa kujibu kero za wateja - nawashangaa ile mbaya!mkuu, ni baada ya kupokea SMS hii kutoka tiGO, hata kabla sijaanza kutumia yao, ndipo nikakutana na mauzauza hayo. yaani hawa tiGO ni matapeli usipime! najua wapo humu, naomba wajitokeze watupe ufafanuzi kuhusu uhuni huu wanaowafanyia wateja wao. halafu hata mtu ukipiga customer care hawapokei simu.