Tido aundiwa zengwe lingine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tido aundiwa zengwe lingine

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 31, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,231
  Trophy Points: 280
  na Mwandishi wetu

  BAADA ya kung'olewa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando amekumbwa na msukosuko mwingine kutokana na baadhi ya wanachama wa Chama cha Maendeleo Muheza (MDTF) kutaka sekretarieti ya chama hicho kujiuzulu. sasa.

  Wanachama hao wametaka sekretarieti hiyo ing'oke kutokana na kudaiwa kushindwa kuleta maendeleo katika kipindi cha miaka miwili, hivyo kuhatarisha uhai wa chama hicho.


  Kwa mujibu wa kundi hilo, wanachotaka ni uongozi wote wa sasa kujiuzulu, kwani uongozi uliopita ulifanikiwa kuleta maendeleo ikiwamo ujenzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Muheza, ujenzi wa visima vya maji na Shule ya Sekondari Kelenge.


  Walisema kasi ya ukuaji wa chama haionekani tangu kuingia madarakai sekretarieti mpya.


  Akizungumzia suala hilo jana jijini Dar es Salaam, msemaji wa chama hicho, Ramadhan Semtawa, alikiri kuwapo kwa mpango huo wa mapinduzi.


  "Ni kweli huo mpango wa mapinduzi nimeusikia. Jana nimezungumza na mkurugenzi anasema Tido yuko Uingireza na amepanga tukutane karibuni.


  "Ninachosema sekretarieti haijashindwa kazi na sioni sababu ya kujiuzulu. Tunaomba utulivu kwani mipango inatekelezeka. Saccos tayari iko chini ya Mama Semainda ambaye alikuwa Mkurugenzi wa BoT, tawi la Mwanza.


  "Tatizo mwaka jana kulikuwa na mambo ya uchaguzi, ila tutajitahidi na Balozi Adad Rajabu yupo kwa sasa atatupa mbinu," alisema.


  Katika sekretarieti cha chama hicho, Tido ni Mwenyekiti, Mary Chipungahelo (Makamu Mwenyekiti), Nehemia Mchechu (Mhazini), Albert Semng'idu (Katibu), Clement Mang'enya (Mkurugenzi Mtendaji) na Ramadhan Semtawa (Katibu Mwenezi).


  Sekretarieti hiyo iliingia madarakani baada ya kuondoka uongozi chini ya uenyekiti wa Balozi Adad.

  Hata hivyo, Semtawa kwa upande wake, alisema kama shinikizo hilo litaongezeka atajiuzulu kabla ya kutokea kwa mapinduzi.

  "Shikinizo likiongezeka nitajiuzulu kabla ya mapinduzi," alisema Semtawa.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,231
  Trophy Points: 280
  Sera za CCM ni use and dump..................so we should not be surprised with whatever had befallen TIDO.........................
   
 3. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #3
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Loh! hii use and dump mbaya sana. We jiulize wako wapi kina Mngula phillip, ndo ujue ni noma. Tuombe Mungu.
   
 4. m

  mahonjero New Member

  #4
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  hii ni hatari,tukipewa vyeo vingine tuwe tunavikataa jamani.
   
 5. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  Duh, pole sana mzee Tido, ndio maisha lamuhimu amtumainie mungu kwa kila jambo
   
 6. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Wanatumiana kama kondom, baada ya kazi hata kuishika kinyaa; kabla ya kazi very important.
   
Loading...