Ticha amchinja mwanafunzi

Ticha amchinja mwanafunzi

20PROFF

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
8,217
Reaction score
7,255
Mwalimu wa madrasa ya Ali Munawar, ustaadhi Mohamed Ngulanjwa (36) wa Mbagala Mianzini jijini Dar es Salaam, ameuawa baada ya kumchinja mwanafunzi wake.



Ustaadhi huyo aliyekuwa mwalimu wa madrasa na shule ya awali ya Ali Munawar, alimchinja mwanafunzi huyo saa 12.10 jioni kwenye eneo la madrasa baada ya kutenganisha kichwa na kiwiliwili

(hudugu)

-


Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Jonathan Shana, akizungumzia mauaji hayo , alisema tukio hilo la kinyama, lilishuhudiwa na wananchi waliomuua ustadhi huyo.

Alisema baada ya mwalimu kumuua mwanafunzi wake wa kiume alichukua kisu alichotumia pamoja na msahafu na kukimbia.-

"Ilidaiwa kuwa alimchukua mtoto huyo , kumlaza chini kisha kumchinja kwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili na kutelekeza vipande vya mwili wake kwenye varanda," alisema Kamanda Shana.

Baada ya mauaji hayo mtuhumiwa alianza kukimbia lakini wananchi walimvamia na kumshambulia kwa mawe na kila silaha iliyokuwa karibu na kumuua papo hapo.-

Shana alieleza kuwa polisi walifika eneo la tukio na kuchukua maiti hizo na kuzipeleka hospitali ya Temeke.-
-Hata hivyo alisema jina la mtoto huyo mwenye umri kati ya miaka 10- 12 halikufahamika na polisi inaendelea na uchunguzi.



Read more:-http://www.vitukovyamtaanews.com/2014/02/inasikitishamwalimu-aliyemchinja.html#ixzz2u7Buda2I
 
Too sad nimeiona hii habari ila natamani kujua zaidi hata toka kwa wanufunzi waliokuwepo ilikuwaje dah huyu ni pepo na ukiuwa kwa upanga nawe utauliwa kwa upanga. Na kuna picha niliona baba kashikwa na askari kupewa msaada wa kutembea kashika vitabu analia kwa uchungu nahic na mzazi wa mtoto alieuwawa, wananchi nilitamani wangezungumza angalau wasomaji tupate mwanga wa tukio lilikuwaje dah poleni wahusika
 
loh it is so sad tunaelekea wapi kama walimu wa dini tunaowategemea kuzionya jamii zitu kimaadili wanafanya matukio ya kinyama namna hii RIP mwanafunzi wa madrasa
 
Maskini upo nyumbani, una hamu ya kukuona kitoto chako ukishatoka kazini kumbe kameshajifia.

So so sad.
 
Ah! Walimu wa Madrasa wanavituko sana!
Kwa sababu gani alimchinja mwanafunzi wake?
Anaejua plz!
 
Inasikitisha san mtt kaenda tafuta elimu ya kumjua mungu, kakutana na ukatili huo. Ss naomba ifikie mahali hawa watu wanaotembea na visu, panga au fimbo pasipo sababu ipatikane sheria ya kuwabana hata kupitia shiria ndg ndg za serekali za mitaa maana tunakaa nao tunawaona na wengine tunawafaham.
 
Taarifa haijakamilika, hebu tuambie ilikuwaje mpaka huyo ustadhi akafanye, hebu tujuze zaidi
 
Bangi zinakusumbua na upuuzi wako we nawe wale wale shame on u kufa wewe basi?

Nadhani hujamuelewa, nilivyoelewa mimi ni kuwa iwe retaliation kwa mzazi wa mtoto kumchinja huyo ustadhi (huenda uchungu wa baba kwa mwana ungepungua). Hope ndio alinamaanisha
 
Back
Top Bottom