Tibaijuka: Wanaoniita mwizi wataisoma namba

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
tibaijuka.jpg

Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka jana alikuwa mkali bungeni akisema yeye si mwizi na kuwabeza wanaomuita hivyo kuwa wataisoma namba.

Profesa Tibaijuka alifikia hatua hiyo baada ya kuhamaki kutokana na baadhi ya wabunge wa upinzani kupaza sauti na kumuita mwizi wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria.

Profesa Tibaijuka alianza kwa kuwataka wabunge wamuunge mkono Rais John Magufuli kwa kuwa amechaguliwa na wananchi.

“Wenzetu ambao kazi yao ni kuja kutusimamia sisi (upinzani) wana haki ya kusema wanayoyasema, lakini hata sisi tuna haki ya kuyaweka vizuri ili yaeleweke kwa wananchi,” alisema.

Profesa Tibaijuka alisema upinzani ukifilisika utabaki kukemea kwa sababu ni lazima tu useme kitu, Bunge linageuka kijiwe na bungeni si mahali pa kupeleka hoja za vijiweni.

Kauli hiyo iliwakera wabunge wa upinzani ambao walianza kupaza sauti zao dhidi yake, hali iliyoonekana kumchanganya.

Akirejea hotuba ya msemaji wa kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu kuwa Tanganyika inainyonya Zanzibar na kuifanya koloni lake, Profesa Tibaijuka alihoji: “Tanganyika inainyonya Zanzibar katika lipi? Hili ni jambo la kujiuliza. Nimejiuliza mimi kama mchumi. Kazi yangu ya kwanza nyinyi mnanijua nilikuwa kwenye shirika la makazi duniani, hamjui kwamba nilikuwa kwenye Shirika la Biashara la Dunia?” alihoji.

Kutokana na zomeazomea kuendelea, Spika wa Bunge, Job Ndugai aliingilia kati: “Waheshimiwa wabunge namlinda mzungumzaji, naomba muwe wavumilivu. Mheshimiwa Profesa endelea.

“Kwa wale wanaosema nimeiba mtaisoma namba, mimi si mtu wa kutishwa na vitu vya ovyoovyo. Mimi sitishwi na hoja za ovyoovyo, huyo (mtu) akaisome namba. Nasimama hapa kwa sababu nataka nitetee vitu. Mtu anapopotosha anaweza kuleta hatari. Tanganyika kwa mtizamo wa kiuchumi haiwezi kuinyonya Zanzibar.

“Katika Dunia ya ustaarabu unasikia hoja. Lissu hapa angeweza kuzomewa, lakini wastaarabu wakamsikiliza wamekomaa kisiasa,” alisema huku baadhi ya wabunge wakiendelea kumzomea.

Tibaijuka aliwahi kuwa waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati wa utawala wa Rais Jakaya Kikwete na aliondolewa baada ya kutuhumiwa kupata mgawo wa fedha za Tegeta Escrow.
 
Akichangia bungeni juzi proff tibaijuka amesema " si vyema mgawanyo wa rasilimali katika wilaya uwe sawa!!" Kikubwa ni kuangalia population na ukubwa wa eneo.

AKITOLEA Mfano wilaya ya muleba hususani jimbo lake la muleba kusini lenye kata 25!!!JIMBO Ambalo naamini kwa sasa ndio jimbo lenye kata nyingi kuliko majimbo yote ya uchaguzi tanzania bara!!!!

Bado akaongeza kuiomba serikali izidi kutoa ufafanuzi kwa kutoa waraka juu ya hii campaign ya elimu bure.

Coz inachanganya na wananchi hawataki changia chochote kile kisa tu elimu ni bure. So ni vyema mh Simbachawene akajaribu kulifanyia kazi kwa kuainisha majukumu ya mwananchi katika utolewaji wa elimu bure!!
 
Kwa tunaomfahamu huyu mama hatupati shida kwa hizo kelele zenu za kumuita mwizi.Uwezo wake ni mkubwa hakuna wa kupinga hilo!! Kikubwa ni siasa za maji taka ndio zilizotumia nguvu kubwa sana kumchafua huyu mama!!!

Hofu kubwa walihofia kwa Kasi na uwezo aliokuwa nao....akizidi kupaa juu kisiasa itakula kwao.Ila hakuna kinachoharibika hata kwa Mh Magufuri inaweza ikala kwao!!!

Mama kaza buti watakaotaka kujua nini unafanya wake MULEBA kusini baada ya miaka mitano wataweza kujua uwezo wako.Viva PROFF Tibaijuka.
 
Iko hivi
Tibaijuka mwizi, na sakata hili lilitokana na muamala wa tegeta escrow, maazimio ya bunge yalimtaka rais achukue hatua za kinidhamu dhidi yake ....na rais alifanya hivyo. Tibaijuka hakupelekwa mahakamani ni halali kuitwa mwizi.......sawa.

2007 katika sakata la mkataba tata wa Richmond, Lowassa alijiuzulu uwaziri mkuu kwa kulitia taifa hasara, bunge kama kawaida liliazimia kuwa lowasa aachie ngazi. Lowassa hakupelekwa mahakamani ila akiitwa mwizi, watu hawataki.

Jamani hii sio double standard?
 
Amekugawia hela ya mboga.
 
mimi naamini akihamia upinzani kama wale wengine anaweza kusikilizwa na hawata mzomea tena wala kusema ni mwizi tena....kwa sababu wapinzani wanamsikiliza mwizi kama huyo akishahamia kwao ila sio akiwa bado ccm
 
Tatizo letu Tz ni kuchanganya taaluma na siasa. Usomi unaofaa kuwa wa kisiasa uachiwe mkondo wake, na usomi unaostahili kufanya kazi za kitaaluma uendelezwe. Otherwise haya hayataisha hata kama Prof ana uwezo mkubwa wa Kitaaluma.
 
Iko hivi
Tibaijuka mwizi, na sakata hili lilitokana na muamala wa tegeta escrow, maazimio ya bunge yalimtaka rais achukue hatua za kinidhamu dhidi yake ....na rais alifanya hivyo. Tibaijuka hakupelekwa mahakamani ni halali kuitwa mwizi.......sawa.
2007 katika sakata la mkataba tata wa Richmond, Lowassa alijiuzulu uwaziri mkuu kwa kulitia taifa hasara, bunge kama kawaida liliazimia kuwa lowasa aachie ngazi. Lowassa hakupelekwa mahakamani ila akiitwa mwizi, watu hawataki.
Jamani hii sio double standard?
Lowassa kakanusha na akataja mwizi wa ile project, na wewe umemsikia. Sasa je, Tiba ametaja mwizi? Hauwezi kuwalinganisha. Basi kama wote wanakanusha kuwa sio wezi, wawataje wezi halisi, halafu uone nani atataja na nani hatataja!
 
Hoja yako nyepesi sana, huyo Mama zile pesa kasema ni za msaada kwa shule yake, na alipewa na Rugemalila na kwa hivyo sio mwizi ( je maneno hayo ni ushahidi tosha wa yeye kujisafisha)

Lowasa nae anasema hahusiki, Jk anasema Lowassa ndiye mhusika mkuu kwa kuwa alikiuka maagizo ya baraza la mawaziri na kujifanyia mambo vile ajuavyo yeye.
( kusema tu hahusiki kwa maneno ni ushahidi tosha?)

Kumbuka mwizi anaweza akakamatwa red handed na bado akakataa kuwa mwizi.

Tuache upendeleo.....kama Tiba mwizi, Lowassa nae mwizi
 
Misimamo ya kishabiki ya wabunge inazaa hoja tata ambazo haziwezi kuleta maendeleo kwa nchi.
Hakuna anayesalimika hapa. Ni dhahiri kuwa wabunge wote wangekuwa wa chama kimoja mfano ccm wasingetoa hoja wazitoazo leo. watu wengi huanza na maneno "Naipongeza serikali .. nampongeza rais .. waziri naunga mkono asilinmia 100" n.k.
kuna dalili ya unafiki na nia ya kutafuta vyeo au kuonekana tu kuwa ni watu wazuri kwa seriali na rais.
Rais amerundikiwa heshima na madaraka makubwa mno kwa imani na katiba hadi kila mtu anashawishika kujipendekeza kwake! hili ni tatizo ambalo wengi wanalijua lakini hawatakiri ukweli huu ama kwa woga au kwa kujipendekeza au kwa unafiki! Kama rais ana anapewa madaraka na heshima kiasi hiki kwa nini asiyatumie!
 
kama mhalifu anajisafisha kwenye chombo cha kutungia sheria na wengne wakiona sawa.. hapo utawala bora itakuwa ni ndoto.
 
Hoja yako nyepesi sana, huyo Mama zile pesa kasema ni za msaada kwa shule yake, na alipewa na Rugemalila na kwa hivyo sio mwizi ( je maneno hayo ni ushahidi tosha wa yeye kujisafisha)

Lowasa nae anasema hahusiki, Jk anasema Lowassa ndiye mhusika mkuu kwa kuwa alikiuka maagizo ya baraza la mawaziri na kujifanyia mambo vile ajuavyo yeye.
( kusema tu hahusiki kwa maneno ni ushahidi tosha?)

Kumbuka mwizi anaweza akakamatwa red handed na bado akakataa kuwa mwizi.

Tuache upendeleo.....kama Tiba mwizi, Lowassa nae mwizi
Hajasema tu, amemtaja hadi mwizi. Sasa kwa nini wasichukue ushahidi kwake kuhusu aliyemtaja?
 
Iko hivi
Tibaijuka mwizi, na sakata hili lilitokana na muamala wa tegeta escrow, maazimio ya bunge yalimtaka rais achukue hatua za kinidhamu dhidi yake ....na rais alifanya hivyo. Tibaijuka hakupelekwa mahakamani ni halali kuitwa mwizi.......sawa.

2007 katika sakata la mkataba tata wa Richmond, Lowassa alijiuzulu uwaziri mkuu kwa kulitia taifa hasara, bunge kama kawaida liliazimia kuwa lowasa aachie ngazi. Lowassa hakupelekwa mahakamani ila akiitwa mwizi, watu hawataki.

Jamani hii sio double standard?

Nani hataki Lowassa aitwe jina lake?
 
Hajasema tu, amemtaja hadi mwizi. Sasa kwa nini wasichukue ushahidi kwake kuhusu aliyemtaja?
Kwani yeye ni nani kiasi kwamba akisema na kutaja basi ni kweli?

Aliyeachia madaraka kwa kashfa hiyo ni Lowasa au huyo mwingine unayeshindwa kumtaja kwa jina?
 
Mwizi atabakia kua Mwizi tuuu hata iweje na kama huyo Lowasa upo ushahidi kua kaiibia Serikali ataitwa Mwizi tuuu sasa na Huyo Tibaijuka wenu kama ushaidi upo kua kaiba na ataitwa mwizi tuuu

Na ukweli usiopingika kua kweli Tanganyika inainyonya Zanzibar kwa mambo mengi tuuu wanaobisha wanabisha kwa kisiasa ila kwa ukweli utabakia ukweli hata iwejeeee
 
Back
Top Bottom