TIBAIGANA hapo ajwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TIBAIGANA hapo ajwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 29, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,184
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  MGONGANO wa maamuzi kati ya kamati za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umeendelea, ambapo Kamati ya Nidhamu ya shirikisho hilo imetengua adhabu za kufungiwa maisha kwa mwamuzi Osman Kazi.

  Kamati ya Nidhamu iliyokuwa chini ya Kamanda wa zamani wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana ilifikia uamuzi huo na kutangaza jana mbele ya wanahabari, ikiwa ni mara nyingine tena ikitengua ama kupunguza adhabu zinazotolewa na Kamati ya Mashindano.

  Kazi pamoja na waamuzi wenzake wasaidizi watatu ambao ni Omari Miyala, Omari Mfaume na Kamwanga Tambwe walifungiwa kuchezesha soka maisha na TFF wakihusishwa na rushwa kutokana na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Mtibwa Sugar na Majimaji.

  Hata hivyo katika uamuzi huo wa Tibaigana ni Kazi pekee aliyepunguziwa hadi miezi mitatu, wakati wenzake watatumikia adhabu ya miaka mitatu.

  Klabu ya Majimaji ambayo ndio ilituhumiwa kutoa rushwa hiyo kwa waamuzi na kupigwa faini y ash. Milioni kumi na TFF imefutiwa adhabu hiyo ya faini na kamati ya Tibaigana.

  Licha ya kutengua adhabu hizo, pia kamati hiyo ilitengua adhabu nyingine iliyotolewa ya kufungiwa kwa miaka mitano iliyotolewa kwa Katibu wa Chama cha Waamuzi Mkoa wa Ruvuma , Rashid Lwena na Katibu wa Kamati ya Waamuzi ya mkoa huo, Juma Gaudi.
  Tibaigana alisema jana kuwa, warufani hao waliokuwa wanapinga uamuzi wa Kamati ya Mashindano dhidi ya adhabu zao walidai kuwa kamati hiyo ilikuwa haina mamlaka ya kulitolea uamuzi suala lilokuwa linawakabili na kamati yake imetengua maamuzi yote yaliyopitishwa baada ya kuona utetezi huo ulikuwa sahihi baada ya kupitia kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa)


  Tibaigana aliongeza kuwa kamati yake ilichukua uamuzi huo kwa muibu wa kanauni za Fifa, ambao unabainisha kuwa kamati yake na ile ya rufaa ndizo pekee zenye mamlaka ya kushughulika masuala yanayohusu tuhumu zinazohusiana na rushwa..

  Kwa mujibu Ofisa huyo mstaafu wa polisi , kamati yake pia ilipitia upya kesi hiyo ya tuhuma za rushwa na kubaini kwamba ilikuwa ni kweli kuwa watu wawili ambao hawakutambulika walitoa fedha Sh. 200,000 kwa waamuzi na waliikubali na kuipokea.


  Hatahivyo kamati hiyo ilishawishika kukubali kuwa pamoja na waamuzi walifanya kosa hilo, kwa kukubali kupokea fedha hizo , mazingira yaliyozunguka tuhuma hizo yalithibitisha kuwa walichukua fedha bila ya kuwa na nia mbaya na walichezesha mechi kihalali wakifuata sheria 17 za mchezo wa soka .

  “Ni waamuzi hao ndio waliripoti suala hilo kwa mamlaka husika na hata tuhuma ambazo ziliibuka bada ya kurejesha fedha walizopewa kwa mamlaka (TFF) , Hakukuwepo na malalamiko yoyote kutoka kwa timu ya Mtibwa ama Majimaji kuhusiana na mechi yao ambayo waamuzi hao walichezesha, ” alisema.


  Lakini pamoja na hayo, alisema kamati hiyo imeamua kumwondoa kabisa Kazi kuwa miongoni mwa waamuzi watakaochezesha Ligi Kuu ya soka ya Tanzania Bara katika raundi ya pili kutokana na kushindwa kuripoti kesi hiyo ya rushwa polisi kwa wakati.

  Lakini Miyala, Mfaume na Tambwe adhabu yao itakuwa kufungiwa miaka mitatu badala ya maisha kutokana na kukana maelezo ya awali kwamba walipewa fedha.


  “Hawa watatu walidai walikuwa hawajui lolote kuhusiana na suala hilo la rushwa na kwamba hawakuhusika kabisa katika tuhuma hizo,” alisema Tibaigana.

  Aidha Tibaigana alisema Majimaji walikutwa hawana hatia, kwani watu wawili ambao walitoa rushwa hiyo kwa waamuzi hawakuweza kufahamika na kulikuwa hakuna ushahidi wa kuwahusisha watu hao na klabu ya Majimaji.

  Kwa upande wa maofisa wa waamuzi mkoa Ruvuma ambao pamoja na kutokatia rufa uamuzi wa Kamati ya Mashindano, pia nao wamefaidika na uamuzi wa kamati hiyo ya nidhamu kwa sababu kamati iliyotoa uamzui huo haikuwa na mamlaka na pia kulikuwa hakuna ushahidi kuwa wao ndio walipeleka fedha hizo kwa Kazi na wenzake.

  Hivi karibuni baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Mashindano walikaririwa na gazeti hili wakisema hawaridhishwi na namna kamati ya Tibaigana inavyopindua maamuzi yao mengi.

  Wajumbe hao walitishia kujiuzulu kama hali ikiendelea hivyo kwa vile inaonekana kana kwamba kuna kukomoana.

  Walitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Kamati ya Tibaigana kuwafungulia wachezaji wa Yanga, Mosses Odhiambo na Amir Maftah waliokuwa wamefungiwa kucheza mechi tatu wakidaiwa kumtukana mwamuzi.
  Pia kamati hiyo ya Nidhamu imepata kutengua mara mbili uamuzi wa Kamati ya Mashindano wa kumfungia kucheza soka kwa miezi mitatu kwa nyakati tofauti kiungo wa Yanga, Athumani Idd ‘Chuji’.

  Wakati huo huo, akizungumza jana, mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Mashindano alieleza kufadhaishwa na uamuzi huo wa Kamati ya Tibaigana.

  “Hata sijui ametumia kanuni zipi kwa sababu sisi pia tulitizama hizo kanuni za Fifa na kutoa adhabu hiyo, lakini wao wenzetu inakuwa kama tunashindana.

  “Binafsi nimechoka mambo haya, nafikiria kukaa pembeni sihitaji kudhalilishana,” alisema mmoja kati ya wajumbe wazito wa kamati hiyo.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,184
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Aiwezekani rushwa wale wote mmoja afungiwe mitatu wengine miezi mitatu acheni kujuana kwenye soka mtaaribu soka la tanzania wazee wetu...sheria iko wazi timu ikikutwa na rushwa unaishusha ligi na faini nyie mnaangalia jamani watu wa kusini watakosa timu na wachaga nao wakija na malalamiko ligi si itakuwa na timu 100
   
Loading...