Tiba ya Robin Van Parse Serbia kwa Placenta Fluid | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tiba ya Robin Van Parse Serbia kwa Placenta Fluid

Discussion in 'JF Doctor' started by IshaLubuva, Nov 19, 2009.

 1. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2009
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jana nilisoma habari kwenye mtandao zikielezea kuwa mshambuliaji chipikizi na nyota wa Arsenal na timu ya taifa ya Uholanzi Robin Van Parse atakwenda Serbia kwa ajili ya matibabu ya maumivu aliyoyapata kwenye kifundo cha mguu wake kwa mama mmoja wa Kiserbia aitwaye Mariana kwa kutumia Placenta Fluid. Inasemekana kuwa matibabu hayo yanaweza kuongeza kasi ya upanoji wake na kuchukua majuma machache takriban mawili au matatu tofauti ya majuma sita kama alivyoelezwa na madaktari wa kisanyansi (kama angetumia upasuaji).

  Wadau kuna mtaalamu anayejua zaidi maelezo ya matibabu haya na iwapo yanafanyika nchini Tanzania.

  Nilivyosoma habari hii nikakumbuka kuna jamaa walikuwa wanatupa stori wakati tukiwa sekondari kuwa kule Tanga kuna wataalamu ambao wanatoa tiba ya watu aliovunjika viungo vyao pasipo upasuaji wala kuweka mhogo (POP). Jamaa alituambia kuwa huna huyo mtaalamu wa Kitanga anachukua magamba ya migomba na kuyazungusha kwenye kipande cha mti cha mfano wa mguu, kama mtu huyo amevunjika mguu, halafu anaanza kufanya kama anaunyoosha vila. Wakati akifanya hivyo aliyevunjika mguu husikia maumivu makali na baada ya mduda anakwambia mambo tayari na kweli jamaa anaanza kutembea. Je wadau wenye asili ya Tanga hizi habari zina ukweli wotote?

  Nawasilisha
   
Loading...