Tiba ya mafua

The hammer

JF-Expert Member
May 17, 2011
2,381
1,760
Jamani wataalam wa afya au mwenye kufaham tiba ya mafua,nimesumbulwa na mafua kwa kipindi kirefu sana bila kupona,nimeenda hospitali mbalimbali bila mafanikio.Hivyo naomba mwenye kufaham tiba anijue niweze kupona
 
'konyagi'
 
KITUNGUU SOMU:

Kitunguu Somu ni kinga ya maradhi mengi mno, na pia ni dawa ambayo ndani yake kuna vitu vinavyojulikana kwa "ALLICINE" NA "GARLICINE" ambavyo vina nguvu kubwa ya kupigana na wadudu.

Meza tembe (chembe) moja ya Kitunguu Somu kila baada ya chakula na pia unywe juice ya kitunguu Somu iliyochanganywa na maji ya ndimu na pia unaweza kujifukiza mvuke wa Kitunguu Somu.

Inshallah natumai dawa hii itakusaidia ila nakuomba kitu kimoja uwache kula vitu vibaridi sana na vitu vikali sana. Hata hivo nitachangia kidogo juu ya madhara ya Kitunguu Somu, kitu chochote ambacho utatumia zaidi au utatumia bila mpango maalum basi lazima huleta madhara kwahivo kila kitu kitumiwe kwa kiwango fulani ili kujiepusha na madhara ya hicho kitu chenyewe The hammer
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom