Tiba ya kunuka miguu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,456
Reaction score
872,092
Awali ya yote nichukue nafasi hii kuwapa pole sana wale wote wenye hili tatizo asilimia kubwa wakiwa ni wanaume.

Ni tatizo linalokera na kufedhehesha sana, hivyo kuwanyima wengi raha na kukosa kujiamini.

Hili tatizo lina viashiria na vyanzo vingi lakini ukiachana na lile tatizo linalowekwa kwenye kundi la magonjwa ya ngozi kutokana na maambukizi ya vimelea vya bakteria na fungus, kuna chanzo kingine kisichopewa kipaumbele na wengi! Nacho ni uchafu, jasho na kutosafisha vizuri miguu.

Wengi wetu ni mabingwa wa kuoga kwa kumwagia maji na kupaka sabuni na kujisuuza bila kujali sehemu muhimu za maungio na viungo vilikobanana. Maeneo haya ni muhimu kupewa usafi wa pekee ama wa ziada.

Kwa mfano vidole miguuni licha ya kuoga mwili lakini ni muhimu sana kumalizia kwa kusafisha kwa makini sehemu zote katikati ya vidole.

Kisha zingatia yafuatayo:-
1. Vaa soksi safi
2. Vaa soksi kavu
3. Usirudie soksi
4. Usivae soksi kavu lakini miguu ikiwa na unyevu
5. Epuka kuvaa viangu vya plastic ama ngozi bandia
6. Kumbuka kusafisha viatu kila mara
7. Epuka kuvaa viatu vyenye unyevu
8. Zingatia kuvaa viatu na soksi vinavyoruhusu hewa kupenya nknk

Kama tayari una hili tatizo ufanyeje?

Wengi wetu hukimbilia hospitali ama kutumia marashi kuua harufu lakini hapa unaongeza tatizo badala ya kutatua.

Fanya hivi:-
1. Hakikisha miguu yako inakuwa safi katikati ya vidole kabla ya kulala na hata baada ya kulala
2. Tumia mchanganyiko wa maji yenye ndimu na chumvi kusafisha miguu mara mbili kwa siku
3. Tumia mafuta ya nazi halisi kupaka katikati ya vidole mara mbili kwa siku..
4. Hakikisha muda wowote unapovaa viatu miguu vidoleni ni safi na mikavu, soksi ni safi na kavu na viatu ni visafi na vikavu...

Utakapofanya yote haya na bado tatizo liko palepale wahi hospitali kwa uchunguzi zaidi na tiba
 
Ukifanya hayo yote uliyoyaorodhesha hapo juu itachukuwa muda gani kumaliza tatizo??
 
Kwa kuongezea jaribu kuwa na pair zaidi ya moja ya viatu ili uweze kuvipumzisha na kupata hewa safi
 
Haha..hiyo itahusu jinsia zote
Yeah unajua wengi hawajui tofauti ya kuoga na kujisafisha.... Wengi ni mabingwa wa kuoga lakini sio kujisafisha
. kuvaa nguo za ndani hasa chupi ni tatizo
. kutojua namna ya kujisafisha vema hasa sehemu zenye uvungu, mipasuko na maungio
. kuacha nywele ziwe ndefu bila kuzihudumia vema hasa maeneo ya mipasuko, uvungu na maungio
. kutokausha na kuacha unyevunyevu sehemu tajwa hapo juu....
. Kuvaa nguo za ndani zenye unyevu
 
Nasubiri huo Uzi mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…