Tiba ya Babu: Nai-challenge serikali kutoa tamko hili

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Ni kitu kisichopingika kwamba serikali inaonekana kukubaliana na tiba ya Babu wa Loliondo kwa kuamua kumpa misaada ya magari, manesi na ulinzi, vitu vinavyogharamiwa na kodi za umma.

Kwa hali hii naipa changamoto serikali hiyo changamoto ya kutoa tamko -- bila kigugumizi kwamba wale wote wanaoishi na VVU na kutumia dawa za ARV, basi:

1. Waache mara moja kutumia dawa hiyo (ARV) baada ya kupata kikombe cha Babu.

AU

2. Waendelee kutumia ARV, pamoja na kupata kikombe cha Babu.

Serikali lazima iwe na msimamo unaoeleweka, siyo kujificha-ficha nyuma ya pazia la dawa ya "imani" kwani sasa hivi ni mapema mno kujua athari (au la) za tiba ya Babu. Sasa basi endapo hapo baadaye Watz waliopata tiba hiyo watadhurika, basi tujuwe kwamba hiyo ilitokana na maelekezo ya serikali yetu ambayo ndiyo pekee yenye dhamana kubwa ya kutoa huduma za afya kwa wananchi wake.

Pili, ingefaa serikali imlazimishe babu kuweka kumbukumbu za wagonjwa wanaokwenda kwake kupata tiba kwa kuwaorodhesha majina na anuawani zao kwa sababu endapo kutatokea mtu aliyepata kikombe hicho na kudhurika, basi aweze kufungua mashitaka mahakamani dhidi ya Babu.

Bila kumbukumbu itakuwa vigumu kwa babu kukubali kama kweli alimpa mtu huyo kikombe.
 
Keshasema sio busara kuacha dawa mara baada ya kupata kikombe. Someni magazeti jamani. Babu ameshauri hivyo na pia tusisahau kuwa kwa sasa serikali yetu iko kwenye mchakato wa kufuatilia wagonjwa 200 waliojitolea kupimwa afya zao baada ya kunywa kikombe. Let us give more time to our government.
 
Tamko la serikali/ TFDA limekaa kisiasa zaidi kuliko kisayansi! Wanaogopa kupingana na babu kwasababu wanaogopa kuwaudhi wananchi/ wanaimani wengi!

Keshasema sio busara kuacha dawa mara baada ya kupata kikombe. Someni magazeti jamani. Babu ameshauri hivyo na pia tusisahau kuwa kwa sasa serikali yetu iko kwenye mchakato wa kufuatilia wagonjwa 200 waliojitolea kupimwa afya zao baada ya kunywa kikombe. Let us give more time to our government.
 
Keshasema sio busara kuacha dawa mara baada ya kupata kikombe. Someni magazeti jamani. Babu ameshauri hivyo na pia tusisahau kuwa kwa sasa serikali yetu iko kwenye mchakato wa kufuatilia wagonjwa 200 waliojitolea kupimwa afya zao baada ya kunywa kikombe. Let us give more time to our government.

Tunasubiri na tamko la Mbeya na Tabora. Serikali ipeleke usaidizi kama Loliondo.
 
Back
Top Bottom