Tiba ya asili ya matatizo ya ”Hormonal imbalance” kwa wanawake

Dinnah

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
803
1,000
Habari wanawake wenzangu,

Poleni na majukumu, leo nimependa niwaletee huu ujuzi kidogo ambao nina ushuhuda nao, niliona post sehemu nikajaribu na ikanipa majibu ndani ya siku 3.

Kuna wanawake wengi wanasumbuliwa na matatizo ya hormone kubalance, kitu kinachopelekea kutoona siku zao, au matumizi ya njia za uzazi wa mpango mfano sindano kuna baadhi wakitumia hawaoni kabisa siku zao.

Ukienda zahanati unashauriwa utumie vidonge vya uzazi wa mpango bila kujua vile navyo vina madhara yake kwa mtumiaji. Tuachane na madawa yenye kemikali kuna njia mbadala ambayo unaweza itumia ukiwa nyumbani ili kurejesha au kuona siku (bleed).

Mahitaji: Tangawizi mbichi na asali

Hatua:

- Tangawizi mbichi unakata vipande vidogovidgo unachemsha mpaka ibadili rangi. Unaipua unachuja kwa chujio au kitambaa safi unajaza kikombe cha chai.

- Ukishaichuja unafunika kuacha ipoe, ikishapoa unaweka kijiko kimoja cha asali mbichi kisha unakunywa kama chai.

- Unaweza tumia asubuhi na usiku matokeo yake ni ya haraka siku moja mpaka 3 unaona siku zako.

Jaribu utanipa mrejesho.

ice_2019-11-20-15-10-38-315.jpeg
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
1,900
2,000
Nje kidogo ya mada:

Mpenzi wangu wa pekee ana tatizo la MP. Anatoa damu nyingi kupitiliza alafu ni kwa siku sita na kujirudia baada ya siku 17 kama sikosei. Akimaliza MP mara kadhaa anapungukiwa damu. Madaktari wanampa madawa kibao alafu wanadai hormone hazijabalance sasa sijui shida nini.

Haya wanawake msaidieni wifi yenu maana jana usiku nilimwambia nitachukua hatua. Ningeanzisha uzi lakini sipendi maana si mwandishi mzuri, sitarajii mtu atadhihaki.
 
Mpe pole wifi yetu. Labda ningependa nijue historia ya wifi kidogo kuhusu matumizi ya njia yoyote ya uzazi wa mpango kama amewahi tumia mfano kijiti au kitanzi.

Mara nyingi njia hizi huleta kero hizo za kurudia rudia bleed. Je mmefanikiwa kupata mtoto? Na tatizo limeanza lini?
 
Dinnah

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
803
1,000
Hivi akishaona siku zake ndio itakuaje? Atanufaikaje?
Itakuwa vizuri sababu njia hii ni nzuri katika kusafisha mfuko wa uzazi, endapo haujableed miezi saba unadhani uchafu utatoka kwa njia gani?

Ananufaika kwa kuwa na amani, mwanamke kutokuona siku ni sawa na mwanaume kukosa kusimamisha stress zake nadhani utavutia picha.
 
Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
51,082

Mimi siku za nyuma nilikuwa napitiliza sana naweza kukata hata miezi mitatu au miwili ila nilikuwa nafurahia maana hakuna wakati huwa nalaani kuzaliwa mwanamke kama wakati wa hedhi. Sasa hivi zimekaa sawa ni miezi minne sasa mzunguko uko perfect.
 
Unafurahi kama hufanyi, usiombe ufanye alafu upitilize yote hiyo utamaliza UPT pharmacy. Kila kukicha unasikilizia sijui nitaanza kujisikia kichefuchefu unaona hola, unaweza anza kuhisi katoto kanacheza tumboni kwa uoga huku umepitiliza miezi 2 tu.
 
Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
51,082
2,000
Unafurahi kama hufanyi, usiombe ufanye alafu upitilize yote hiyo utamaliza UPT pharmacy. Kila kukicha unasikilizia sijui nitaanza kujisikia kichefuchefu unaona hola, unaweza anza kuhisi katoto kanacheza tumboni kwa woga huku umepitiliza miezi 2 tu.
Hahaha noma sana
 
Mr Miller

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
11,188
2,000
Nje kidogo ya mada:

Mpenzi wangu wa pekee ana tatizo la MP. Anatoa damu nyingi kupitiliza alafu ni kwa siku sita na kujirudia baada ya siku 17 kama sikosei. Akimaliza MP mara kadhaa anapungukiwa damu. Madaktari wanampa madawa kibao alafu wanadai hormone hazijabalance sasa sijui shida nini.

Haya wanawake msaidieni wifi yenu maana jana usiku nilimwambia nitachukua hatua. Ningeanzisha uzi lakini sipendi maana si mwandishi mzuri, sitarajii mtu atadhihaki.
- Amewahi kujifungua kwa njia ya kawaida?
- Amewahi kufanya njia yoyote ya kuzuia mimba?
- Ameshawahi kupata Miscarriage?
- Ni mtumiaji wa vilevi (pombe)?
- Ni tatizo la muda mrefu au limeanza hivi karibuni?
 
Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
16,547
2,000
Itakuwa vizuri sababu njia hii ni nzuri katika kusafisha mfuko wa uzazi, endapo haujableed miezi saba unadhani uchafu utatoka kwa njia gani?

Ananufaika kwa kuwa na amani, mwanamke kutokuona siku ni sawa na mwanaume kukosa kusimamisha stress zake nadhani utavutia picha.
Asante sana, sikujua hilo
 
Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
16,547
2,000
Mimi siku za nyuma nilikuwa napitiliza sana naweza kukata hata miezi mitatu au miwili ila nilikuwa nafurahia maana hakuna wakati huwa nalaani kuzaliwa mwanamke kama wakati wa hedhi. Sasa hivi zimekaa sawa ni miezi minne sasa mzunguko uko perfect.
Nakumbuka sana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom