Tiba Gani Apatiwe Huyu Ex-girlfriend?

Tiba Gani Apatiwe Huyu Ex-girlfriend?

Langu

Member
Joined
Nov 20, 2011
Posts
37
Reaction score
9
Salam kwenu wana MMU,

Natumaini wote ni wazima wa afya na kama ni tofauti natoa pole.

Nahitaji ushauri kuhusu binti kama huyu anayenisumbua sana na sijui nifanyeje kwake aamini kwa sasa aniaamini siko nae tena?

Nilikua kwenye mahusiano na binti mmoja na nilimpenda ila baadae akaanza kunicheat na kuwa jeuri sana kwangu mpaka mda mwingine nilikawa najiuliza nifanyeje atulie.

Kutokana kwamba huyo binti nilimpenda nilitumia mda mwingi kumshauri ila akawa mgumu kubadilika.

Nilivoona imeshindikana ikabidi niachane nae na nikamwambia kabisa mimi na yeye basi na wala hakujali kauli yangu.

Kutona na hilo niliingia baadae kwenye mahusiano na binti mwingine na huyu sasa akaonekana ni mwenye heshima na mwaminifu sana kwangu, cha kushangaza baada ya kujua kuwa nimeingia kwenye mahusiano mengine alimtafuta huyo dada na kumpa vitisho kuwa aniache la sivyo atamwendea kwa kalumanzila.

Huyu binti wa sasa wala hakukata tamaa akaendelea kunipenda na kwa sasa nimemuoa, na ni mke halali wa ndoa.

Yule X alipata taarifa kuwa nimeoa sikujua alichukuliaje ila sikuona response yeyote, ingawa kabla mimi sijaoa ndo niko kwenye process huyo X akanitumia picha Facebook akiwa amemkumbatia mkaka na kuniambia ni mchumba wake na mwenzi wa kumi na mbili mwaka jana wanaoana, mi nikampa hongera na go ahead.

Cha kushangaza baada ya mimi kuoa amekua akisumbua sana, anatafuta namba yangu ya simu kwa rafiki zangu wa facebook, mara ananitumia sms za mapenzi facebook na kila hatua yake anayopitia anataka nami niwe updated, jambo ambalo naona sio zuri na litakuja niaribia usalama wa ndoa yangu.

Nifanyeje wana JF kuhusu huyu dada, na anamaanisha nini wakati alishanitumia picha ana boyfriend na mi pia nataka ndoa yangu hisiwe na migogoro?
 
Nimependa avatar yako, pole na matatizo
cc: Kaizer
 
Last edited by a moderator:
Vyungu vya zamani muda mwengine vinsumbua, wew fanya yako tu si alichezea bahati
 
Hapo inaonyesha bado anakupenda na hajapata kama unavyodhani,facebook aliweka picha kupunguza stress,hivyo basi shikamana na mkeo ,huyo kaa nae mbali kabisa maana unaweza kukuta unache[uka bila kutaka si unajua tena mtalaka hatongozwi kaka.Ila makungwi wanakuja subiri utapata majibu.....
 
Asanteni sana kwakweli, nitazingatia
 
Huko facebook umeshindwa kumblock?

Kwebye simu yako umeshindwa kumblock?
 
Block namba zake na ikiwezekana hata huko facebook m-block. Kama akikutumia meseji usijibu na akipiga usipokee. Tatizo litaisha.
 
Huyo anatafuta pa kujipozea baada ya kutendwa sana, kuwa na msimamo
 
atachoka tu hasa ukimpuuza. Hakikisha humfichi kitu mkeo ili uwe safe.
Akituma txt usimjibu mwenyewe atachoka
 
kaa mbali na wafariji wataabishaji, m-block huko fb hataona wala hutaona chake, akipiga pokea na acha simu hewan bila kuongea, baadae atachoka na atapotea mwenyewe
 
Huko facebook umeshindwa kumblock?

Kwebye simu yako umeshindwa kumblock?
Mtoa mada hili hapa suluhisho la tatizo lako.
Akitumia namba nyingine mwambie the next thing utamripoti kwenye kampuni ya simu. Alafu kumbuka ukicheka na nyani.......
 
Duh! Pole sana ndugu!,cha msingi akili na mawazo yako elekeza kwa mke wako kipenzi, hesabu kwamba hujawahi kuwa na huyo x,ziba kabisa mianya yote ya kucontact nae kwa namna yoyote ile ZAIDI SANA NIKUTAKIE KILA LILILO KHERI KTK NDOA YAKO!
 
Kwanini bado upo rafiki naye fb? Huyo ni wa kumblock ili apate message kuwa umemsahau. Wewe kuwa nae bado fb na hiyo tabia yake unaonyesha kuwa bado unataka kujua mambo yake.

Haya nenda kam block fb kama kweli hautaki akusumbue maishani mwako.
 
Asanteni, nimeblock and now i think nitakua na amani, maana hata sms ilikua ikiingia nahisi nimemkosea mke wangu
 
Back
Top Bottom