TIBA ASILIA WAIPINGA SERIKALI

wembeee

JF-Expert Member
Jan 16, 2015
2,708
1,353
Shirikisho la vyama vya tiba asili Tanzania limesema kuwa halikubaliani na tamko lililotolewa na wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia,wazee na watoto la kukataza matangazo yao.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam mwenyekiti wa Taifa wa shirikisho la vyama vya tiba asili Tanzania Abdulrahman Lutenga amesema kuwa hali hiyo ni kudhalilisha taaluma yao na hivyo bado hawajapata sababu ya kutosha ya serikali kukataza matangazo yao na hawaelewi sababu zilizotolewa.
 
Ni bahati mbaya sana kuwa wanatumia Tv na redio kujaribu kufundisha. Nilisikitika sana kumwona mmoja akifundisha jinsi ini na figo zinavyofanya kazi nikaona ni majanga matupu. Nikajiuliza kwanini hawa wanaruhusiwa kufundisha vitu wasivyovijua??
 
Wengi ni washirikina na wanatumia mazingaombwe kutibu. Naunga mkono serikali.
 
Yaani ndani ya nchi yangu kuna mvurugano Na mwingiliano wa sauti, mawimbi hayako sawa kabisa, nawashauri viongozi tuombe msaada marekani waje watusaidie kuweka sawa, kusudi tupate kuelewana ili kila mmoja ajue nafasi yake Na jinsi ya kuitumia
 
Viongozi wa matabibu wa Tiba Mbadala na Tiba Asili haitawasaidia kutoa matamko kwenye vyombo vya habari waende wizara ya afya wakazungumze na viongozi wa Serikali kupata muafaka kinachotakiwa kufanywa.
 
Hii nchi sa ivi ni mvurugano watu hatuelewani kila mmoja hajui majukumu yake tumebaki sha majungu ubishi na matamko yasiyo na positive feedback
 
Ukweli ni kuwa kuna mambo mengi yanaendeshwa kiholela hebu turudi kwenye kufata sheria zinasemaje watz kuna tatizo hatufati sheria.
 
Wengi hawajui madhara ya dawa wanazozitoa. Ni utaratibu bora wa kisayansi unapofanya utafiti kujua madhara ya dawa yaani side effects. Unaanzia na wanyama hadi kwa binadamu. Lakini hawa jamaa kazi yao kusema tu dawa zao hazina madhara wakati ni uongo. Vitu kama LDL havijabainishwa wala kutafitiwa.
 
Yaani ndani ya nchi yangu kuna mvurugano Na mwingiliano wa sauti, mawimbi hayako sawa kabisa, nawashauri viongozi tuombe msaada marekani waje watusaidie kuweka sawa, kusudi tupate kuelewana ili kila mmoja ajue nafasi yake Na jinsi ya kuitumia
umenena mkuu yawezekana aliyoyasema mkosamali tunahitaji consultant yametimia tusubiri tuone itakuwaje, lakini si nzuri kabisa muda unasogea na hatua nazo ni ngumu kupiga Mungu atunusuru na wimbi hili.
 
Back
Top Bottom