TI: Vurugu zinatokana na ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TI: Vurugu zinatokana na ufisadi

Discussion in 'International Forum' started by EMT, Dec 1, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Shirika la kupambana na ufisadi, Transparency International, limesema ghasia ambazo zimeshuhudiwa kote duniani kwa kiwango fulani zimetokana na ufisadi. Katika uchunguzi wake kwa nchi 183 unaotolewa kila mwaka, Transparency International imesema nchi ambazo zimeshuhudia vurugu hizo ndizo ambazo zimefanya vibaya katika kukabiliana na ufisadi.

  Mwaka huu shirika hilo limegundua kuwa nchi zilizohusika na mapinduzi katika mataifa ya kiarabu kama vile Misri, Algeria, Libya na Syria zikiwa chini katika orodha hiyo ya mataifa yaliyo na ufisadi mkubwa zaidi. Uchuguzi wake aidha unaonyesha nchi nyingi zinazotumia sarafu ya Euro ambazo zinakabiliwa na wakati mgumu kiuchumi pia zinafanya vibaya katika kukabiliana na ufisadi.

  Uchunguzi huo unasema kushindwa kwa maafisa wa umma kukabiliana na rushwa na watu wanaokwepa kulipa kodi, ndio sababu kuu zinazochochea mzozo wa madeni katika mataifa hayo. Katika ripoti hiyo ya Transparency International nchi ya New Zealand imeorodheshwa ya kwanza kama nchi isiyokuwa na visa vingi vya ufisadi.

  Barani Afrika, Botswana inaongoza ikiwa nambari 39, kama nchi isiyokuwa na ufisadi wakati Somalia imeibuika ya mwisho kama nchi ambako ufisadi unashuhudiwa kwa kiwango kikubwa. Tanzania imeshika nafasi ya 100 wakati. Rwanda imepongezwa kwa kupiga hatua katika kukabiliana na ufisadi. Shirika la Transparency International linamalizia kwa kusema ''serikali fisadi ni serikali ambayo iko katika hatari ya kuangamia''.

  BBC Swahili - Habari - TI: Vurugu zinatokana na ufisadi
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kati ya 138 sie tumekuwa wa 100 basi tutajiona bingwa sana!

  Ufisadi ukikithiri, yatatokea machafuko. Sasa bado ndo kwanza mkoko
   
Loading...