Hata ulimwengu uliumbwa kwa fikra ndugu. Na yawezekana hao wanaolalamikia muziki hawafikiri. Sasa, hao mapacha waliwabeba weusi kwa kipato kilichotokana na nini? Kama ni muziki mbona leo waanze kulia? Kama ni ishu zingine kwa nini leo walilie muziki? Sijui kama huwa unapata muda wa kujiuliza haya.
Kadhalika haimaanishi kuwa kila afanyaye kazi serikalini kipato chake kinamtosha. Hivyo haimaanishi kuwa kila afanyaye muziki basi aendeshe benzi, maana ndivyo unavyotaka tuamini.
Kingine ninachokiona hapa ni suala la kufuata mkumbo kwa hawa wasanii. Kisa tu fulani kaimba basi nami naweza. Ukiacha hilo kuna suala la kudhani muziki ni kimbilio baada ya kukosa kwingine, hasa kutokana na kukimbia umande. Bangi na malengo wapi na wapi?