Mkuu yawezekana ni mjumbe huru lakini kwa staili yako ya majibu ni kuwa kuna zaidi ya mjumbe huru. Mi hoja yangu kubwa hapa ni kwa vipi kila mtu ang'ang'anie clouds media kwa ajili ya kutoka?
Suala lingine ni kuwa kama kuna aina nyingi ambazo wadau wameshindwa kuvaa uhusika, imewezekanaje clouds media kuvaa uhusika? Kama jazz haipendwi mdau atamlazimishaje mlaji kuipenda? Na kama wadau wameshindwa, wanamuziki wetu wamewezaje kuendesha tasnia yao hadi kupendwa? Hapa tunawazungumzia kina Kitime na Kinasha. Yako wapi mafanikio yao katika kuongoza tasnia yao kama si wadai kina Mawingu kufanikiwa japo kuufikisha muziki hapo ulipo?
Unazungumzia hip hop ya USA. Wale walikuwa wanaimbia maisha yao na ndio maana ikawa rahisi kwa muziki huo kuweza kukubalika. Umemzungumzia Jay z lakini hukumtaja co founder wa def jam- Russell. Unajuaje kama bila Russell Jay z angesimama? Hujamtaja Marion Suge knight. Huyu ni CEO wa Death Row. Hapa unajuaje kama Dr Dre angesimama bila Marion? Kwa hiyo ishu si mwanamuziki asimamie kazi zake bali lazima kuwepo na specialization. Kujua kuimba si kujua soko, na ndio maana 'wadau' wakawepo.
Nami nasema, haiwezekani kwa kuwa tu haiwezekani kila mmoja aimbe bongofleva, basi tuimbiwe na aina ya miziki ambayo haipenyi masikioni. Hao wanaotafuta hizo variatiea watapotezwa tu na soko! Muziki tunaoujua Tz ni dansi, taarab, gospel, mnanda, mchiriku, bongofleva...
20% yuko/alikuwa THT? Ben Pol, Diamond, ali Kiba, Prof J, Weusi... Hawa nao wako THT? ndio ujue pia kuwa kizuri kinajiuza. Nawe kwa kuijua tasnia ilivyo ni hatua zipi ulizochukua, mkuu kujaribu kuwasaidia hawa kina Temba?