Tatizo kubwa ilililonalo Marekani ni kwamba wao wanajiona kwamba ni Super nation na kwamba wanaweza kuwanyooshea vidole watu wengine, ukweli ni kwamba hakuna jamii Duniani ambapo watu wa aina fulani hawabaguliwi ila tatizo linapokuja fulani kujiona kwamba yeye ni mtakatifu wakati yeye mwenyewe hayuko kamili hiyo ndiyo shida aliyo nayo USA!
Ni mara ngapi Marekani inasema Urusi kuna Ubaguzi ingawaje hakuna wakulipinga hilo lkn Marekani anapata wapi uhalali wa kunyooshea Urusi au nchi nyingine yoyote Duniani khs Ubaguzi wakati mpaka leo hii asilimia zaidi 80 ya watu walio jela ni weusi wakati weusi ni asilimia 20 tu ya Wamarekani?
Kama kuna wageni wanakuwa attacked Urusi kwa ajili tu ya rangi yao ambapo ni kweli inatokea sana Urusi na sehemu nyingine lkn pia Marekani watu wanapigwa risasi kila siku kwa kuwa tu weusi ni hivi majuzi weusi wamepigwa risasi kanisani kwa sababu tu ni weusi ni mara ngapi tunasikia vijana weusi wanapigwa risasi na Polisi Marekani tena juzi mtoto wa miaka 12 alipigwa risasi na Polisi na uchunguzi unaonyesha walioufanya wenyewe Marekani kwamba ni rangi yake tu ndio iliyopelekea apigwe Risasi?
Hata Hollywood ni Wabaguzi akina Will Smith, Beyonce &Co. juzi kati hapa hata walisusia Oscar kwa sababu ya Ubaguzi wa mtu mweusi?
Hivyo nchi zote zina Ubaguzi na kila jamii ina mtu ambaye inamchukia na hakuna mwenye uhalali wa kumnyooshea mwingine kidole kwamba wewe ni mbaguzi zaidi, bali ni wote kama Binadamu tuungane na kujaribu kutatua tatizo na siyo kunyoosheana vidole na kutoa top ten sijui nani mbaguzi klk mwingine, huwo ndiyo ujumbe wangu!
Marekani, kama nilivyosema, ina matatizo yake ya ubaguzi.
Lakini, imeweza kuweka misingi imara ya kupinga ubaguzi. Misingi ambayo hata Tanzania hatuna.
Marekani wana sheria kali za kupinga ubaguzi, si wa rangi tu, mpaka age discrimination, gender discrimination etc.Kuanzia Civil Rights mpaka Equal Employment Opportunity Zaidi ya hapo, suala la kuwa mbaguzi wa rangi ni suala la aibu kijamii. Ukiwa mbaguzi Marekani una side na the wrong side of history, the losing side. Ndiyo maana hata wanaofanya ubaguzi hawawezi kufanya ubaguzi wa wazi.
Tanzania mtu anaweza kuweka tangazo kwenye gazeti kwamba anatafuta mtu wa kuuza dukani, lakini lazima awe anaongea Gujarat. Marekani that is a violation of the Equal Opportunity Employment Act. Sisi hata hatuna hilo. Licha ya hilo, juzi mbunge kafura katoa kauli za kibaguzi bungeni kusema mtu mwingine si Mtanzania on the basis of color of skin, lakini hata sikusikia kwamba imezua mjadala.
Wiki kama mbili zilizopita, nilishangaa kuona tangazo la kazi ya kawaida limeweka sharti la umri, nakumbuka ulikuwa miaka 25 kama sikosei. Kazi yenyewe ya kutumia akili wala huwezi kusema mtu Zaidi ya umri huo hataweza, nikashangaa sana kuona hii blatant age discrimination. Nikasema Marekani habari ya ubaguzi wa umri wa wazi kama huu mtu anakushtaki na kukutoa mamilioni ya dola.
Marekani ina tatizo la "American Exceptionalism/ Superpower status" kama ulivyosema. Hii inaweza ilikuwa kweli zamani, lakini muda unavyozidi kwenda inazidi kuwa hadithi ya wanasiasa kuliko ukweli wa mambo.
Tofauti ya sehemu kama Marekani na China kwa mfano -China nao wabaguzi sana tu- ni kwamba, wakati Marekani ina tatizo la kujidai ina exceptionalism, watu watalisema hilo kama ni tatizo na kuliandikia mpaka vitabu. Kuna kitabu kimoja kizuri sana kinaongelea hilo cha Nancy Sodenberg kinaitwa "The Superpower Myth: The Use and Misuse of American Might". Kitabu kinaponda Marekani kujitutumua u superpower lakini kimepata mpaka foreword ya Bill Clinton, mtu aliyekuwa rais wa Marekani.
Nitafutie kitabu kama hicho cha Mchina kinachoisema China kwa kukalia kwa nguvu visiwa vya South China Sea, ambacho kina foreword ya Deng Xiaoping kwa mfano.
I can guarantee you, hakuna! Ukitaka kuandika kitabu critical tu, Communist party inakufunga.
Hapo tunaona kitu kingine muhimu kuhusu Marekani. Marekani inathamini sana pluralism kiasi kwamba huwezi kusema Marekani iko hivi au vile. Kwa sababu ukisema kuna watu wanaonadi sana Marekani kuwa Superpower na kuingilia mambo pengine, kuna wengine pia hawataki kabisa Marekani ijiingize katika mambo ya nchi nyingine.
Ukisema kuna Donald Trump racist, wengine watakwambia kuna Jimmy Carter mchungaji asiyetaka racism so much mpaka Waisraeli wamemuona anajiweka na Wapalestina, kitu ambacho hakikutegemewa kwa mchungaji.
Kwa hiyo Marekani just defies these simplistic categorization because it is too complex, too diverse and too experimental to be fitted into any of the old world categorizations.