Threads zilizoharibu saikolojia yangu

Threads zilizoharibu saikolojia yangu

Hayo mambo ni sawa na kujiziba pumzi ili ufe ni ngumu inahitaji hisia na imani ya kiwango cha flyover
 
Nini hasa sababu ya kufanya yote hayo? Kwa faida gani?
 
Nini hasa sababu ya kufanya yote hayo? Kwa faida gani?
Ooh!!
Kuna faida ambazo nilielezewa mwanzo kabla ya kufanya vitendo hivi! Na pia hasara zake!
Nitaandaa uzi maalumu kuonesha yale niliyoyapitia katika vitendo vyote hivyo nikihusisha faida ambazo nimezishuhudia mimi kama mimi na hasara ambazo zilinikumba!!
 
Nakumbuka nilipokuwa nna miaka 11 kijana mdogo sana kuna babu yangu alikuwa anaumwaga na kuna siku wazee walituchukuwa watoto wote twende tukamsalimie babu yaani kumuona hospital..

Kufika tukaambiwa tumsalimie; babu kwa upande wangu sikuona mtu kitandani pale inaposemekana babu alipolala.. wenzangu wote walimsalimia kwa kumuamkia; mimi nilikuwa nawaona kama wanakisalimia kitanda mda ukafika bana akanambia msalimie babu yako nikamwambia mbona sioni kitu hapa.. uwezi amini Baba akunisemesha tena kwamba nimsalimie babu na katika watu hakuna mtu aliyesikia maongezi kati ya baba na mimi:: mama nahisi alisikia ila wale wenzangu wote walikuwa anakiangalia kitanda..

Binafsi sikujua chochote nini? Kilichokuwa kinaendelea ila wakubwa walikuwa wameelewa nini? Kinatokea katika ulimwengu mwingine .. kurudi home baba akawa ananisemesha kuwa kwanini? Nimekataa kumsalimia babu tulipokuwa hospital “ nikamwambia kuwa sikuwa naona mtu pale kitandani ... baada ya tukio akatafutwa mtu aje kuniombea nikaombewagwa.. safi

Baada ya hapo mimi mwenyewe nikawa naogopa kwendaga hospital kwa kukimbia kadhia hiyo ya kuulizwa ulizwa.. yaani ulikuwaga utoto tu na hofu nikisikia wanasema kesho tutaenda hospital.. ntatafuta michezo ya kucheza... nisiende hospital

Baada ya siku chache babu alifariki.. tena kwenye msiba.. karibia watoto wote walikuwa wanalia msibani lakini mimi nilikuwa ganzi hata lepe la chozi sikuwaga nalo.. tena baba akawa ananichunguza tena baada ya msiba wakawa wanasemezana na mama mwanao wenzake wote walikuwa wanalia lakini! Yeye alikuwa kimya sana .. kiukweli hata mimi sijui nini kilikuwa kinanitokea..

Kuhusu kuto muona babu kitandani wakati wa kwenda kumuangalia hospital; wengine wanasema pengine alikuwa ameshakufa au akili /hisia yangu zilikuwa zimeona kuwa amefariki sema sikuweza kusema moja kwa moja... kiufupi nilikuwa mbele ya mda.. na kuitiwa watu waje! Kuniombea sijui ilikuwa kwa nini! Nahisi kuziondosha zile nguvu labda waliofia sisije kunitawala..

Ila kwa sasa Sina hali kama izo
 
Honey bee yani upo very powerful,just dont lose focus.
 
Ooh!!
Kuna faida ambazo nilielezewa mwanzo kabla ya kufanya vitendo hivi! Na pia hasara zake!
Nitaandaa uzi maalumu kuonesha yale niliyoyapitia katika vitendo vyote hivyo nikihusisha faida ambazo nimezishuhudia mimi kama mimi na hasara ambazo zilinikumba!!
Hizo ungeweka hapa tu.. maana hata uliyoandika yamejadaliwa sana humu
 
Siku zote hakuna jambo la kitofauti ambalo huwa linanipita bila ya kulifanyia jaribio!! Ideas za kuyafanya haya yote nilizitoa kwa watu fulani! Na ilikusudi hufanikishe haya yote, unahitaji utulivu wa hali ya juu!! Binafsi sidhani kama mtu ambaye yuko hallucinated kuwa anaweza kufanya haya, ni vigumu, ni utulivu wa hali ya juu!! Ila yatakapoanza kukutokea puani hapo hata knowledge ya utulivu sidhani kama itatumika tena, make nafsi yako itakuwa inajiendesha huku unaona!

Make kuna wakati unaweza ukawa unaona unaishi, ghafla ukapitiwa na gari kiasi cha kupata ajali mbaya, kumbe ni ndoto! Lakini ilikuwa inacheza kwenye uhalisia!! Kuna wakati unapoitazama saa yako ya mkononi utaona ina mshale mmoja, tena wenyewe unaelekea kushoto!!

Labda jaribu kwa kutumia binaurial beats!!
Mkuu hapa kuna tofauti gani na mtu ambaye akili yake inamuendesha (aliyewehuka)??
 
Mkuu hapa kuna tofauti gani na mtu ambaye akili yake inamuendesha (aliyewehuka)??
Naweza sema utofauti upo,
Make kila tukio la tofauti linapopita, utakuwa excited lakini nafsi yako itatulizwa ghafla!

Mfano, ishawahi kukutokea kuwa uko unaongea na mtu fulani mko mahali fulani, halafu maneno unayoyazungumza au anayoyazungumza, unagundua kuwa ushawahi zungumza naye au ashawahi kuyazungumza, unastaajabu, kisha maisha yanaendelea! Unaweza kukuta hata mazingira mliopo ndo yaleyale! Waswahili husema ni kujirudia kwa matukio!

Nikikwambia kuwa tukio la mwanzo lilikuwa ni ndoto ambayo hukuwahi kuigundua unaweza kunielewa?

Hali hii inakuwa kama hivi, sema kwa aliye activate nafsi, haya mambo yanakuwa kwa frequency kubwa! Yapo mengi ya kueleza! Jamii forums ingelikuwa na system ya voice note! Mngefaham mengi zaidi niliyoyapitia!

Utofauti ni mkubwa!!
 
Nakubaliana nawe na nimekuelewa kiasi fulani,

Nikuulize kitu nje ya mada kidogo, hivi ndoto zinatengenezwa katika katika nyanja ipi ya mwili?
 
Nakubaliana nawe na nimekuelewa kiasi fulani,

Nikuulize kitu nje ya mada kidogo, hivi ndoto zinatengenezwa katika katika nyanja ipi ya mwili?
Ok, ngojea nirudi darasani, ntakujibu kwa haka ka uelewa kangu kadogo nilikonako!

Kwenye ubongo kuna sehemu inaitwa temporal lobe, inapatikana kwenye ubongo ikiigemea zaidi ubongo wa mbele, ambayo huhusika na taswira

Ili ndoto itokee, condition ya REM lazima iwepo yaani Rapid Eye Movement ambayo inakuwa katikati ya usingizi na ufahamu, na ubongo wako lazima uwe kwenye theta waves

Ajabu sio kuota tu, ila ni kwenye issue ya ndoto za lucid zinazotokea katika vibration za ubongo za Gamma, ambazo waweza tengeneza mwenyewe kwa binaurial beats! Hizi ndoto unaweza kuamua nani ashiriki, nani atoke, tukio gani lionekane, tukio gani lisitokee, pia unaweza kujitibu maumivu ndani ya lucid! Ni ndoto za ajabu sana na za kushangaza!!
 
Back
Top Bottom