Threads zilizoharibu saikolojia yangu

Threads zilizoharibu saikolojia yangu

honey bee

Senior Member
Joined
Nov 23, 2021
Posts
139
Reaction score
236
Habari wana jamii forums,
Hivi ulishawahi kupambana na thread za mtu fulani zinazohusu mambo ya kiroho na miujiza!
Mfano:
•kutoka nje ya mwili
•kuondoa hofu kiroho
•kutengeneza ndoto za Lucid
•kumuona mke mtarajiwa kwenye kioo
•kufanya tahajudi

Mchezo wa kufanya jaribio la kutoka nje ya mwili lilisababisha kuamsha nafsi yangu kutoka kitandani kwa kasi zaidi pasipo kutumia nguvu bali kutumia mawazo yangu mimi mwenyewe, ingawaje nilivyopaa kufika mbele kidogo nikageuka nyuma, mwili sikuuona!! Wala ile Silver cord sikuiona pia! Baada ya kuligundua hilo, nilijiona kama mtu ambaye alishakufa zamani, nilijawa hofu sana kufikia hatua ya kushtuka nikiwa kitandani na jasho la kufa mtu!! Hali hiyo iliniharibu saikolojia yangu sana, ilifikia hatua ninawaza kufa tu! Sikutamani kuishi tena!

Mchezo wa kufanya jaribio la kutengeneza ndoto za Lucid ulisababisha kujihisi niko katika ndoto muda wote, hasa hasa nyakati za usiku nilipokuwa nikifikiri jambo, kisha nikazubaa tu, lilitokea! Niliposhtuka lilipotea! Kuna wakati nilipokuwa ninaamka usiku nilikuta baadhi ya vitu ambavyo havikuwepo kabla ya mimi kulala vimeongezwa ama vimepangwa tofauti, mfano foronya langu nililikuta miguuni badala ya kichwani, nilipojaribu kulirudusha, kumbu kumbu ilipotea ghafla na nisielewe nafanya nini! Ndipo niliamua kulala na asubuhi nilipoamka nilikuta vitu viko sawa tu!

Jaribio la kioo, kitana na apple usiku wa manane lilisababisha nikaona kiza kwenye kioo pale tu nilipozubaa!! Ghafla macho yangu kwenye kioo yalionekana mekundu, kisha taswira za ajabu zingeanza kupita kwenye kioo!!

Pindi nilipokuwa kwenye lucid dreaming halisi, nilizifurahia sana, make nilikuwa mtengenezaji wa character ambao nilihitaji kuwaona kwenye huo ulimwengu! Nilifanya chochote ninachojiskia, sikuweza kuona taswira yangu kwenye vioo!!

Ndoto ya mwisho ya lucid kunitokea, niliigundua mapema zaidi, make niliota nimeelekea shule niliyosoma advance kuchukua cheti, ila cheti hicho kilikuwa na picha ya cheti cha form four, nilipokitazama kwa umakini, niliona profile picture yangu ya facebook iko kwenye cheti! Nilipokitazama kwa ukaribu nilikutana na wall paper ya simu yangu iki pale, ndipo nilipotokeza kwenye voluntary mind, nilihisi raha ya ajabu ya kuwa kwenye austral plane kiasi kwamba sikutamani hata kidogo kuamka kutoka usingizini! Nilitamani nilale milele! Ndipo nilipojikuta nafumbua macho! Na Saikolojia yangu iliyokuwa imevurugwa ilirudi kuanzia pale, nikajihisi amani! Nilikuwa nikisumbuliwa na kichwa, kipanda usi! Lakini niliweza kujiambia kichwa pona, nikiwa ndani ya lucid, kichwa kikapona, hata nilipoamka hakikuuma tena!

Na mengi ya kuwaeleza,
Ila tu kama huna kifua cha kumudu mambo hayo, bora uachane nayo, yanawezekana kwa 100% na kila mtu unaweza fanya, ila inahitaji moyo!

Make kipindi naanza kufanya jaribio la kutoka nje ya mwili, kuna muda nilisinzia ingali najielewa! Ila naskia kabisa kuwa nimelala, hata kumeza mate nilishindwa! Niliziskia sauti za majirani wakipiga story japo kwa mbali!

Na hata nilipojaribu kuamka, niliweza kufumbua macho tu, mwili wote ukapigwa ganzi! Ni hatari wakuu!
Ngoja niishie hapa!!
 
Mi hizo zote bado hazijanishawishi kama kutoka nje ya mwili, ingekuwa ukifanya hivyo unaweza kwenda kuzurura nje na kuona matukio yanayoendelea kwa wakati huo ningefanya hivyo kwani ingependeza sana, ila kama ni kuunda tu fikra zako mwenyewe mi sio mtu wa drama sana na nipo real kinyama so ntashindwa kujiongopea, hiyo ya kitana nayo the same, ila huwa nafuatilia hizi mambo ipo siku ntajaribu nikikutana na ile ambayo itanipa life experience na kitu flani worth doing

Naendelea kufatilia madini wanayoshusha wakina Rakims na wengineo, leteni na nyingine zaidi.
 
Mkuu unaruhusiwa kufanya hivyo vitu wakati uko higher (umepiga cha Arusha au cha kimbiji)?
Siku zote hakuna jambo la kitofauti ambalo huwa linanipita bila ya kulifanyia jaribio!! Ideas za kuyafanya haya yote nilizitoa kwa watu fulani! Na ilikusudi hufanikishe haya yote, unahitaji utulivu wa hali ya juu!! Binafsi sidhani kama mtu ambaye yuko hallucinated kuwa anaweza kufanya haya, ni vigumu, ni utulivu wa hali ya juu!! Ila yatakapoanza kukutokea puani hapo hata knowledge ya utulivu sidhani kama itatumika tena, make nafsi yako itakuwa inajiendesha huku unaona!

Make kuna wakati unaweza ukawa unaona unaishi, ghafla ukapitiwa na gari kiasi cha kupata ajali mbaya, kumbe ni ndoto! Lakini ilikuwa inacheza kwenye uhalisia!! Kuna wakati unapoitazama saa yako ya mkononi utaona ina mshale mmoja, tena wenyewe unaelekea kushoto!!

Labda jaribu kwa kutumia binaurial beats!!
 
Mm kwakweli napenda kufanya imaginations na kuvuta vitu kifikra hasa kwenye mahusianoyangu huwa inajibu na Mara nyingi huwa napata majibu mazuri sababu nafanya imagination za furaha Sana hayo ya kutoka nje ya mwili aisee yanipite tu
 
MKUU UNATOKA NJE YA MWILI WAKO??? YANI UNATOKA NJE YA MWILI WAKO MWENYEWE?? WEWE NI NANI??? HUO MWILI UNAHUSIANA VIPI NA WEWE?? JE NI SEHEMU YA WEWE AU??
 
MKUU UNATOKA NJE YA MWILI WAKO??? YANI UNATOKA NJE YA MWILI WAKO MWENYEWE?? WEWE NI NANI??? HUO MWILI UNAHUSIANA VIPI NA WEWE?? JE NI SEHEMU YA WEWE AU??
Ndio mkuu,
Unaudanganya mwili kuwa umesinzia,
Baada ya muda, ubongo wako unakupiga ganzi ili ndoto zikikuanza, matukio ya ndoto yasijitokeze yakauvuruga mwili wako! Mfano kuna wale wanaota wanaongea, na kweli anakuwa anaongea akiwa usingizini! Watu hawa bongo zao huwa haziruhusu kupigwa ganzi ya kutosha!

Sasa ukishapigwa ganzi! Unakuwa unajitambua kabisa, na unakuwa unahisi umensizia, hata kama wewe ni mtu wa kukoroma, unakuwa unajisikia unavyokoroma!

Baada ya hapo, unapata kitu inaitwa out of body experience, ambayo huwa wanapata watu wanaoelekea kufa dk chache mbele, kama ushawahi jiuliza, mtu anajuaje kuwa anaenda kufa hadi kufikia hatua ya kutoa wosia? Pia hali hii huwatokea watu wakati wanafanyiwa operation za vital organs yaani zinazohusu kupasuliwa tumbo au kichwa!! (Waulizie kama uko nao karibu watakupa mwongozo)

Hapo unaweza kujiamsha kwa kujicontrol mwenyewe kwa kufanya imagination, ukiishaamka tu, unaachana na imagination unakuwa nafsi, unauona mwili wako pembeni!
Inatisha mkuu!
 
MKUU UNATOKA NJE YA MWILI WAKO??? YANI UNATOKA NJE YA MWILI WAKO MWENYEWE?? WEWE NI NANI??? HUO MWILI UNAHUSIANA VIPI NA WEWE?? JE NI SEHEMU YA WEWE AU??
Mtu ni roho!
Mwili ni km mimba tu!

Lkn siafiki mambo haya ya kutoka nje ya mwili, yanatumia nguvu(power) ss nguvu gani ndo hapo!
Mambo ya giza tu!
ndo maana zimeharibu saikolojia yake,sio vitu vya kawaida
 
Mtu ni roho!
Mwili ni km mimba tu!

Lkn siafiki mambo haya ya kutoka nje ya mwili, yanatumia nguvu(power) ss nguvu gani ndo hapo!
Mambo ya giza tu!
Hapana mkuu,
Mimi sio mganga, sio mchawi
Ni binadamu tu tena mkristu dhehebu X
Niliweza kufanya hivi vitu kwa mamlaka yangu binafsi!
Kama ukiweza kujiunganisha mawasiliano na uhai wako (pumzi yako) unaweza kabisaaaa!
Mwanzoni sikuamini, nilipoyasikia haya kwa Rakims niliamua kuanza majaribio mara moja, nina moyo mgumu kama jiwe ila ilifikia hatua nikawa natetemeka sana!
Sasa kama mimi nilikuwa naweza kuona viumbe vya ajabu bwenini na nilikuwa naona ni vya kawaida, sasa hii issue ilinitisha kiasi hiki!
Je, wewe ambaye matukio unayasikia kwenye bomba, unaweza vumilia haya?
 
Leo ndio nimegundua Kiswahili cha Threads ni Nyuzi hii lugha ya malkia hii....Samahani mtoa mada!
 
Back
Top Bottom