Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 43,037
- 34,741
Muungano wa Shirika la Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika TLS, wamelaani vitendo vya mauaji na ukandamizaji wa raia wasio na hatia vilivyoshuhudiwa wakati wa maandamano ya uchaguzi.
Katika taarifa ya pamoja, mashirika hayo yamevitaka vyombo vya usalama kuheshimu haki za kiraia za kuandamana kwa amani na kushughulikia maandamano kwa weledi mkubwa ili kuzuia ghasia na uharibifu.
Taarifa ya pamoja imeelezea kuwa wakati wa maandamano kulikuwa na vitendo vya mauaji ya raia, ukiukwaji wa haki za binadamu, uharibifu wa mali, kuzimwa kwa mtandao wa Intaneti, ukamataji na vipigo.
Katika mapendekezo yao, mashirika hayo yamezihimiza familia zote ambazo zimepotelewa na jamaa kutoa ripoti kwa mamlaka au mashirika ya utetezi wa haki za binadamu.
Chanzo. DW Kiswahili