Pole sana! Umeshaoa ama bado bado unamaumivu? Iko hivi katika maisha haya tunayoishi ujue kuna kuzaliwa, kuishi,na kufa. Kupenda na kutokupendwa kupo pia. Usikubali kuishi maisha ya kufikiria yaliyopita. Songa mbele na Mungu akupe imani iliyokuu.
Kama hujaoa Fanya mpango uoe kabisa na mzae chap chap ili usiwe unakumbuka yaliyopita ya Janeth.
Mtu akifa haijawahi tokea akarudi. Nilikuwa nampenda mama yangu hujawah ona alivyofariki nilipoteza kabisa uelekeo hadi shule sikuweza kusoma maana yeye ndo alikuwa ananilipia kila kitu, baada ya miaka 3 mbele sijui nini kilitokea nikanyanyua na kuanza upya safari ya maisha wanaonifahamu huwa hawaamini km ni mimi, na mpaka leo kifo kikitokea nitasikitika wakati huo baada ya siku mbili tatu hakika nasonga mbele kwa speed.
Mtu akishafariki harudi. Usikubali kubakia huko kwa Janeth songa mbele katika mahusiano.