This election is not about Dr Slaa and Chadema is about us as Wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

This election is not about Dr Slaa and Chadema is about us as Wananchi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by George Maige Nhigula Jr., Sep 12, 2010.

 1. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #1
  Sep 12, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu watanzania naomba tukubaliane kitu kimoja uchaguzi wa tarehe 31st October 2010 tusisahau kamwe sio kwa ajili ya Dr Slaa na Chadema ni kwa ajili ya mmambo tunahitaji yabadilike ili na sisi tupate heshima kama wananchi tunao ishi kwenye nchi huru yenye neema tele ambazo mwenyezi mungu ametubariki kuwa na rasilimali nyingi kama vile madini chungu mzima, utalii, ardhi nzuri, bandari,mafuta, bahari, mito, maziwa, biashara na nguvu kazi yenye kiu kubwa ya kuchangia katika ujenzi wa taifa imara lenye uchumi imara.

  Hivyo basi kiu yetu kubwa ni kuwa na viongozi wenye maona chanya na uzalendo mkubwa wa kuweza kutusimamia na kutuongoza kuweza kuzitumia rasilimali zetu ili zitunufaishe kwa kuwa na maendeleo endelevu ambayo kila mtanzania atanufaika nayo bila kujali tabaka, rangi, dini, kabila na wasifu wake wa nje na ndani.

  Hivyo basi sote tumeshuhudia kuwa uwongozi wa chama tulichokipa dhamani kwa takribani miaka 50 kimeshindwa kutupa maono sahihi na uongozi makini kutuvusha katiba changamoto nyingi ambazo kila mtanzania anakabiliana nazo kila siku.

  Baada ya kupata Uhuru tuliweka ahadi na dhamira ya dhati kutokoomeza ujinga, kuwa na huduma bora za afya na kuondoa umaskini kwa wananchi wengi ili waweze kuishi maisha ambayo binadamu anastahili, lakini leo hii ni miaka hamsini takribani baada ya uhuru je tumeweza kutokomeza au kutatua matatizo hayo. nadhani kila mmoja anaweza kutumie dhamira yake binafsi na kujua kuwa hali halisi ya taifa letu katika nyanja hizo tatu ikoje?

  Ndugu watanzania wenzangu kama tumeshindwa kupata ufumbuzi wa matatizo hayo muhimu je tunahitaji kupoteza kizazi kingine cha watanzania kuendelea kuongelea matatizo yale yale miaka nenda miaka rudi? Je ni nini tatizo haswa la kushindwa kujitatulia matatiza haya yote kama kila rasilimali mungu ametujaria? nini hasa tatizo la kushindwa kujinasua kwenye matatizo hayo muhimu?

  Ndugu zangu tunayo mifano kemukemu ya nchi ambazo zilikuwa na hali duni ya kiuchumi na huduma za jamii duniani kuliko taifa letu, labda tukumbushane mifano michache tu, waliobahatika kutembelea au kosoma historia ya nchi kama SINGAPORE, MALAYSIA, SOUTH KOREA,CHINA, INDONESIA na HONG KONG, nchi hizo zilikuwa duni sana kiuchumi kuliko taifa letu tukufu la Tanzania miaka 50 iliyopita na nchi hizo zote hazina rasilimali kemukemu kama nchi yetu ilizobarikiwa na mwenyezi mungu lakini wamejitahidi kujikwamua kwa kuwa wamekuwa na uongozi wenye maono(vision) na dhamira thabiti ya kuweza kufanya mageuzi thabiti ya kiuchumi! na sote tunafahamu kuwa nchi hizo uchumi wao ni imara na mfano wa kuigwa duniani. uchumi wa nchi hizo umezipiku hata mataifa makubwa yaliyokwisha endelea mda mrefu kama ujerumani, uingereza na nyingine nyingi za magharibi, hivyo basi kama wao wameweza kufanikiwa bila ya rasilimali nyingi kama zetu, sasa kwanini sisi tushindwe na utajiri wetu wa asili mwingi tulionao?
  Nadhani watanzania wote tunajua kuwa tunaweza kuleta mageuzi hayo kama tutadhamiria.

  Hivyo basi tutakubaliano sote kuwa tatizo letu kubwa ni mfumo mbovu wa uongozi uliokosa maono (vision) baada ya kuongoza kwa mda mrefu na kila kitu kinafanyika kama desturi na mazoea ya kawaida. Sote tumeshuhudia mmomonyoko mkubwa wa maadili ya viongozi wetu, ambao wamekuwa wakituburuza kwenda mahali ambapo sipo, kila chaguzi zinakuja na kupita na matokeo yake tumekuwa na desturi ya kuwaabudu viongozi wetu kwa mtindo wa utawala, ambapo viongozi wetu wametusahau sisi wananchi kuwa ndo tunastahili kupata mwongozo thabiti ili tuweze kujiletea maendeleo yetu, lakini imekuwa juu chini, maslahi ya viongozi wetu yamekuwa mbele kuliko maslahi yetu wananchi na matokeo yake viongozi na tabaka la watu wachache(elite) wamefanikiwa kutufunga minyororo ya utumwa ndani ya nchi huru.

  Tunahangaika na hali ngumu tunalipa kodi, tunajitahidi kuwatafutia watoto wetu elimu bora na tumefanya kila kitu kama raia wema lakini juhudi zetu zimekuwa ni za bure, bila mafanikio ya kusisimua, sasa je swali la msingi sote tujiulize tutaendelea mpaka lini kuwa watumwa ndani ya nchi huru isiokuwa hata na mianzi au miale ya matumaini? kwani kila kukicha hali yetu inazidi kuwa mbaya zaidi! sasa inabidi tukae chini tufanye upembuzi yakinifu wapi tulipokosea na tutarekebisha vipi?

  Ndugu watanzania wenzangu, tumeshuhudia watawala wetu wamekuwa wabinafsi na wanafki wakubwa kila mara tunapoelekea kwenye chaguzi za kitaifa, wamekuwa wakifanya kila hila, udanganyifu, vitisho na mbinu mbalimbali ili kuendeleza tabaka lao utawala, huku kila mtawala akiwa na agenda yake ya siri ya kujineemesha yeye, familia yake na wapambe wake , Je what about us? Wananchi? kila mara tumekuwa tukipewa kila aina ya ahhadi na lugha tamu za kiuungwana lakini mwishu wa utawala mmoja tunambulia patupu! sasa ni wakati wa kuwahoji hicho chama tulichokuwa kira mara kikutusihi kuwapa dhamana ya kutuongoza kuwa 50YRS is Enough!

  Kuna tatizo kubwa hapa hawa watawala huwa hawatuelewi kama tutathubutu kuwapa miaka mingine mitano unafikiri kuna maajabu gani watafanya ndani ya miaaka mitano kama miaka 50 wameshindwa? hilo ni suala muhimu sana kuwahoji, na kama tukiwapa thamani tena watajenga kiburi kuwa tumelidhika na hali tuliyonayo hivyo wataendelea kutuchezea mchezo wa kisiasa na kizazi chetu kitapita na tutawalithisha watoto wetu taifa lisilo kuwa na mbela wa nyuma, wao hawana tatizo kwani ndo wanafaida kila matunda ya na neema za nchi yetu hivyo vizazi vyao vitaendelea kuneemeka milele na vizazi vyetu vitaendelea kupata mateso milele, sasa inatakiwa tune uhitaji wa lazima wa sasa wa kufanya mabadiliko ya ghafla(FIERCE URGENCY OF NOW)kama tunataka tuwe na kambi mbili za uongozi utakaoshindana kuliletea maendeleo yetu sisi wananchi taifa letu hatuna budi ya kuwakataa watawala wa sasa leo hii.

  Lakini tusipokuwa na ujasili wa kuthubutu, hatutapata maendeleo milele, ni kipindi kwa kuangalia upande mwingine wa uongozi na tuwapime tuone miaka mitano watafanya nini hawa wengine kwa maendeleo yetu sisi wananchi, hivyo basi uchaguzi huu sio kwa ajili ya Dr Slaa inabidi tupeleke ujumbe mkuu kuwa this election, this year is about us!

  This Election, This Year is about us! This Election! This Year is about us.
  This is not about Dr. Slaa is about us, This Is not about Chadema is about us, Lets all march forward and say 50yrs is enough, this time and this election is about us.
  If we stand together on October 31st we gonna change this country together as one people with common purpose!

  MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA WAFANYE UAMUZI SAHIHI
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Utahangaika san a mwaka huu
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Swadakta mkuu,

  Lakini unatakiwa kuzingatia jambo moja muhimu sana, ili kufanikisha hayo yote uliyoyaorodhesha unahitaji mtu makini,muadilifu, mchapakazi na chama makini. Kwa kuzingatia hilo na kwa kuangalia wagombea tulionao katika uchaguzi wa mwaka huu, lazima tumchague Dr. Slaa kuwa rais wa JMT na tukichague chadema kuiongoza nchi hii. Kwakuwa hao walioko madarakani kwa sasa wamethibitika pasipo shaka kwamba hawawezi kututoa katika lindi la umasikini!!
  Chagua Dr. Slaa, chagua chadema.
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Sijakuelewa kwa hiyo tujichague wenyewe hiyo Oktoba 31?
   
 5. M

  Masauni JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umesema vyema I wish kila mtu angekuwa na ideas kama zako, Tusingekuwa na watu wanaoshabikia CCM! UNAJUA KUSEMA UKWELI KUSHABIKIA ccm katika hali mbaya tuliyonayo mi naona is a selfish behaviour na lack of understanding ya baadhi ya watanzania
   
 6. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #6
  Sep 12, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  This election and this year is about issue we care about, kwa sababu tumekuwa tukichagua tabaka la watu wasiotujali kwa mda mrefu sasa inabidi tuwaambie 50yrs is enough we are looking on other direction this time! and see if the other party what has to offer to us, tukiwachaguwa watu wale wale watajenga kiburi kuwa we can not punish them kwa kutojali maslahi yetu miaka nenda rudi hivyo hawawezi kubadilika kutokana nakiburi tunachowapa kila chaguzi kwa kuwachaguwa watu wale wale, chama kile kile na ahadi zile zile na sera zile zile na mfumo ule ule, na ufisadi ule ule, na ubinafsi ule ule, hivyo basi tuwaadhibu hawa watu ili wakajibange vizuri waje na mikakati mingine mipya na hiyo itachochea ushindani wa vyama kutuletea maendeleo. kwani chama kikiboronga na raisi akiboronga tutakutana nae kwenye uchaguzi na tunamwadhibu hivyo ndivyo maendeleo hupatikana
   
Loading...