Theresa May ni Nani?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,790
Theresa Mary May alizaliwa 01 October 1956 ni mwanasiasa Mwingereza ambae ni Waziri Mkuu wa Umoja wa Umoja wa Kifalme (the United Kingdom) na pia ni Kiongozi wa chama cha Conservative. Alikuwa mmbunge wa jimbo la Maidenhead toka 1997.

Mtoto wa padre, May alikulia Oxfordshire. Kuanzia 1977 mpaka 1983 alifanya kazi katika Bank Kuu ya Uingereza, na kuanzia 1985 mpaka 1977 alifanya kazi katika Association for Payment Clearing Services pia alikua diwani wa London Borough of Merton's Durnsforrd Ward. Baada ya majaribio kadhaa ya kuwania ubunge mwaka 1992 na 1994, alichaguliwa kuwa Mbunge wa Meidenhead katika uchaguzi wa 1997.
b770ce52-a620-4971-b18f-d3cc756903c6.jpg

Theresa Brasier akiwa na wazazi wake miaka mapema miaka ya 1960.

May amelitumikia taifa katika nafasi tofauti akiwa waziri katika serikali kivuli ya William Hague, Ian Duncan Smith, Michael Howard na serikali ya David Cameron, miongoni mwa nafasi hizo ikiwemo kiongozi kivuli wa Bunge na Waziri Kivuli wa Kazi na Pensheni. Alikua pia Mwenyekiti wa Chama Cha Conservative kutoka 2002 mpaka 2003.

Katika Serikali ya Mseto baada ya uchaguzi wa 2010, May alichaguliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Waziri wa Wanawake na Usawa, aliiacha nafasi hii ya pili baadae mwaka 2012. Baada ya uchaguzi wa 2015 alichaguliwa tena kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na ameacha historia ya kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani aliyedumu muda mrefu zaidi tangia enzi za James Chuter Ede miaka 60 iliyopita. May ametoa maamuzi magumu kwenye maswala ya madawa ya kulevya na maswala ya uhamiaji.

Kufuatia kujiuzuli kwa David Cameron mnamo 24 June, 2016, May alitangaza kuwania nafasi hiyo ya juu katika chama cha Conservative na haraka alipendekezwa katika wachache watakaowania nafais hiyo. Alishinda kura za maoni na 5 July, 2016 aliungwa mkono na wabunge 199 wa chama chake na kuendelea kuongoza katika mbio za kuwania uongozi huo pamoja na Andrea Leadsom. Leadsom alijiengua baadae na 11 July 2016 Theresa May alitangazwa kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza.

2016-07-13-1468405452-1079265-Theresa_May.jpg

Alizaliwa 01 October 1956 mjini Eastbourne, Sussex, May ni mtoto wa pekee wa Zaidee Mary aliezaliwa 1928 na kufariki 1982 na Hubert Brasier aliezaliwa 1917 na kufariki 1981. Baba yake alikua padre wa Kanisa la Anglikana wa kanisa la hospitali ya Eastbourne. Baadae alikuwa padre wa Wheatley maili chache kutoka mashariki ya Oxford.

May alisoma katika shule za serikali lakini zilizokuwa chini ya uongozi wa kanisa Katoliki. Alisoma shule ya msingi Heythrop, ambayo ni shule ya serikali baadae alijiunga na shule ya wasichana ya Mtakatifu Juliana ambayo ilikuwa shule yakanisa Katoliki mjini Bedbroke ambayo ilifungwa mwaka 1984.

Akiwa na umri wa miaka 13, May alifaulu vizuri na kuweza kujiunga na shule ya wasichana wenye vipaji ya Wheatley. Wakati May yuko pale, mfumo wa elimu ulibadilishwa na shule ilitoka kuwa ya vipaji maalumu na kuwa sekondari ya kawaida. May alikwenda Chuo Kikuu cha Oxford baadaya ya hapo na kusoma Shahada ya Sanaa (Batchelor of Arts) katika geografia na kufanikiwa kumaliza na degree ya daraja la pili (second class) 1977.

May ni mke wa Philip May, mwanauchumi na ambae kwa sasa ameajiriwa na Capital International, ndoa yao ilikuwa 06 September 1980 na hawakujaliwa kupata mtoto. May ameeleza sababu za kiafya ndio zimepelekea ndoa yao kukosa watoto, alieleza " Unaangalia familia na kuona kuna kitu kimepungua".
b1af677d-f3a7-48ce-8677-253b92a069af.jpg

May anapenda kwenda na wakati katika mavazi, katika hotuba yake kali ndani ya chama chake mwaka 2002 alivaa viatu vyenye urembo wa ngozi ya chui, pia katika mkutana wa kujadili mambo ya pesa akiwa waziri wa mambo ya ndani 2016. Kwenye kipindi cha radio ya BBC kijulikanacho kama Desert Island Discs ambacho watu maarufu walihojiwa na kuulizwa wangependelea nini kama kitu cha fahari, May alisema nakala za gazeti la Vogue. Alishalalamika akisema vyombo vya habari vinazingatia mavazi yake kuliko mafanikio yake kisiasa. 01 November 2012 May aligundulika na kisukari inabidi apate sindano za insulin kila siku.
p-may-589862.jpg

Theresa na Philip May.
 
Theresa Mary May ni mwanasiasa Mwingereza ambae ni Waziri Mkuu wa Umoja wa Umoja wa Kifalme (the United Kingdom) na pia ni Kiongozi wa chama cha Conservative. Alikuwa mmbunge wa jimbo la Maidenhead toka 1997.

Mtoto wa padre, May alikulia Oxfordshire. Kuanzia 1977 mpaka 1983 alifanya kazi katika Bank Kuu ya Uingereza, na kuanzia 1985 mpaka 1977 alifanya kazi katika Association for Payment Clearing Services pia alikua diwani wa London Borough of Merton's Durnsforrd Ward. Baada ya majaribio kadhaa ya kuwania ubunge mwaka 1992 na 1994, alichaguliwa kuwa Mbunge wa Meidenhead katika uchaguzi wa 1997.

May amelitumikia taifa katika nafasi tofauti akiwa waziri katika serikali kivuli ya William Hague, Ian Duncan Smith, Michael Howard na serikali ya David Cameron, miongoni mwa nafasi hizo ikiwemo kiongozi kivuli wa Bunge na Waziri Kivuli wa Kazi na Pensheni. Alikua pia Mwenyekiti wa Chama Cha Conservative kutoka 2002 mpaka 2003.

Katika Serikali ya Mseto baada ya uchaguzi wa 2010, May alichaguliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Waziri wa Wanawake na Usawa, aliiacha nafasi hii ya pili baadae mwaka 2012. Baada ya uchaguzi wa 2015 alichaguliwa tena kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na ameacha historia ya kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani aliyedumu muda mrefu zaidi tangia enzi za James Chuter Ede miaka 60 iliyopita. May ametoa maamuzi magumu kwenye maswala ya madawa ya kulevya na maswala ya uhamiaji.

Kufuatia kujiuzuli kwa David Cameron mnamo 24 June, 2016, May alitangaza kuwania nafasi hiyo ya juu katika chama cha Conservative na haraka alipendekezwa katika wachache watakaowania nafais hiyo. Alishinda kura za maoni na 5 July, 2016 aliungwa mkono na wabunge 199 wa chama chake na kuendelea kuongoza katika mbio za kuwania uongozi huo pamoja na Andrea Leadsom. Leadsom alijiengua baadae na 11 July 2016 Theresa May alitangazwa kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza.

2016-07-13-1468405452-1079265-Theresa_May.jpg

Ni Myahudi!
 
Huyu Mama namuona na mtu wa msimamo na makini sana, na nimeangalia baadhi ya speech zake ni za kuvutia na kutia imani katika future ya uingereza.
Ila sina uhakika nini kitatokea hapo baadae kama viongozi wengine wasipo mpa suppote.
 
Hata hapa kwetu wakina mama wanaweza kama wakiwezeshwa kutoka kwenye ngazi ya kifamilia kwa kupewa elimu na kukuzwa vipaji vyao
 
I'll Never vote for a woman in Africa because they first need strong institutions kabla ya kuwaza kuwa viongozi wakubwa. Africa bado hatuna strong institutions za kiserikali.
 
Msiopenda utawala wa wanawake mwaka huu tumekaba mataifa yote yenye nguvu, kutoka Ujerumana, Uingereza na tunaelekea Marekani.
 
  • Thanks
Reactions: kui
Unamaan gani huna iman na wanawake Econometrician fafanua ww ndio hujui dunia inaendaje acha mambo yakizamani
 
Jamani mbona Rais wa Laiberia anafanya vizuri? Kweli anaumw hawabadiliki.......... Aibu
 
Back
Top Bottom