Pierre, I doubt kama kweli unamsikiliza huyu jamaa unayemsifia. Usije ukachukua tu maneno ya mtaani ukaamini kasema Trump. Kwanza sijui hata kama anajua kama kuna Tanzania. Na hajawahi kuzungumzia Afrika. Najua hapa Bongo watu wanadai kasema hivi au vile. Lakini kama alivyosema Nyani Ngabu tena na tena, Trump hajasema hayo mambo. Na kwa Wabongo ni upuuzi kuanza kujihesabia kwamba Trump atakuwa mkombozi wa Afrika. Ni lini Waafrika tutaacha ukahaba wa kijinga wa kungojea mzungu fulani aje kutukomboa?