The way I met my wife today (Jinsi nilivyokutana na msichana, ambaye ni mke wangu leo)

Ushirombo

JF-Expert Member
Jan 22, 2013
3,557
2,692
Habari zenu. Niwatakie maandalizi mema ya uchaguzi mkuu hiyo siku. Mungu akatupatie viongozi bora.

Mada: Niliugua sana na dalili zote ilikuwa ni maralia, ila sikutaka kwenda dispensary kupima kwani naogopa sana kale kasindano ka kutolewa sampuli, ilikuwa ni third yr wakuu nahesabu baso mwaka mmoja nitoke chuoni, basi kulikuwa na ndugu yangu alikuwa anasoma IFM the same yr 3rd, akaniletea dawa nimeze maisha yaendelee, zilikuwa ni (fansida) mwaka huo ilikuwa 2010

Basi kidume nikazitupia bila kupima wala nini, nikanunua panadol zile za kupima kijiko, ok tulikuwa tumepanga maeneo ya njiapanda ya chuo huko ndani ndani unavuka kamto fulani, bana eeh night ake hali ikabadirlka kinyama dogo nikaanza kupata kila hali mbaya unayoijua mwilini yaani unaona pumzi inakata kabissaaaa, vitu kibao sana.

Asubuhi yake niko hoi natapika tu full time, mi nikiugua sitapika kabisa, hali ilivyozidi kuwa mbaya, rafiki yangu akasema hizo dawa hebu tuzisome, akatafuta pakiti lah haulah dawa ime expire like one yr ago.

Sasa hofu ya kufa ikanikaba, huku mitihani imekaribia. Ikanilazimu kwenda dispensary. Ile natembea toward it, na kidada kiko mbele yangu mara nainama najisikia vomits lakini hakuna nasonga, tukafika kama wote sawa ndo wagonjwa wa kwanza kabisa, tukapewa vikadi kwa nurse, ye wa kwanza mi wa pili, basi akaitwa kwa daktari, akaniambia nenda wewe unaumwa sana, aaaah nikasema no just go dada, akakataa tukabishana kidogo mi nikaenda.

Nikamwelezea daktari hali yote akasema nikapime damu nikakataa nikamuomba any other means else, basi akasema ok kakojoehumu, nikatoka na kichupa.

Dada akaingia, nimetoka tu nikaanza kutapika nje kidogo...
......

2.
Basi alipotoka kumbe na yeye katumwa mkojo pia, akanikuta karibu na choo akanipa pole nikaitikia akatoa sample yake akasepa, mi vivyo hivyo.


Nikajaribu kwenda class vitu haviendi unaona dunia kama gunia la mavi tu yaani kulala huwezi wala kukaa huwezi basi yaani ilimradi tu upo, nikasema let me go for breakfast muda some minutes before majority hawajatoka, nikaenda nichukua bagia na chai yenye tangawizi, nikawa naenda kukaa nikamuona jamaa flan hakuwa class anapiga tea, amekaa na mdada , mdada kainama hivi, nimefika tu jamaa nikamueleza the way ninavyoumwa jamaa akanipa pole na akasema kamaliza tea so anawahi class, yule dada akainua kichwa polepole doooh ni yule wa dispensary.

Yaani pamoja na ugonjwa wangu pale nikaleta kistory story nikamweleza nilivyotupia xpired dawa, akanionea huruma na kunipa pole, nikaanza kuuona uzuri wake kitoto cha Arusha cheupeee nikajua yule classmate wanafahamiana.

Basi nae akachukua tea tukaagana, baadae mchana nafuata majibu wakat i narudi nakutana naye, naye anafuata, tukasalimiana tu, hapo tushajuana majina.
emoji8.png
emoji8.png
emoji8.png


Tukaendelea endelea tukawa tunaonana tu hasa cafteria namuita Ja nae ananiita, hapo nilishamuuliza yule jamaa kama vp ile pisi akasema ye pia alimkuta pale so hata hamjui weraaaaaaaaah muoga nikaanza mdogo mdogo yeye anaishi chuo mi kitaa, nikaanza kumkaribisha mahome huku naogopa kila mara anasema atakuja hakuja ng'ooo 3rd yr ikaisha, 4th yr vile vile, ila uzuri alikuwa ukimuita tu anakuja mkiwa chuo, so sometimes i was delaying purposely so that the dark can hide my shy, namuita anakuja pisi ananukia mafuta safiiii, wakati mjuba mie nimeoga kwa wana na kupaka vaseline tu, akija unapata muda lau wa kutomasa kisela sana kwa uoga wa kiwango cha lami.

Basi uoga ulipozidi kupungukiwa nguvu, courage ilianza kushika hatamu lakini wakati huo mi jua machweo yaani naenda kumaliza chuo, one day akaja geto uuuuh
emoji7.png
emoji7.png
emoji7.png
emoji7.png
emoji7.png
cha ajabu my attempt failed, basi ikawa na mawasiliano tu, mara ipite wiki sometimes miezi hivyo yaani.

Muda wote huo man Ushirombo sikuwa na pisi anywhere unaishi kigumu kama jiwe tu, basi chuo kikasalimu amri kikaniachia nikiwa na mabawa nikaanza kupaa, mara paaaaap ajira ya 1 homeland, kanda ya nyonyo, ila si mkoani kwetu basi nikaanza kukomaa sometimes nikimkumbuka mrembo wangu wa Kaloleni i.e niliemuacha chuo namcheki, imeeeeenda tukapotezana.

Nikaanza kupata pata vinoti aisee nikaagiza ka motorcar nikawa nami kidogo nipo.
Like 1.5yr tulipotezana, sasa one day kwenye huo mkoa na wilaya hiyo kuna mama alifahamika sana kwa kuuza misosi yaan people with titles lazima wakutane pale, unajua tena watu wa halmashauri unakuta wale wakuu wa idara, DED au madiwani yaani naongelea level hizo, kwa bush bush hao ndo madon, basi Mr Ushirombo nikiwa nasaidia kusanifu miradi ya Serikali siku hiyo tukawa na kikao,

Tukamaliza tukaenda kupiga supu, tulipomaliza tukaondoka kurudi halmashauri, oooh muda kidogo kumbe nilisahau simu baada ya kulewa supu, siku hizo kigari changu nilikiacha geto, nikaazima gari jamaa diwani fulani akanipa key akasema ile pale, prado tx haaaaah haaaah nikalivuta vuuuuuuuuuuh nafika pale nashuka mawazo yote kwenye simu tena ya wasap miaka hiyo duh, mara paaaap macho kwa macho na toto nilomuacha chuo, kapendezaaa watu wote wanamuangalia yeye na vile kanda yetu na rangi ya mtume mmmmh bila ajizi akanirukia nikamkumbatia kwa mapenzi yote na extra.

Kila mtu anatabasamu hadi moyoni hatuamini kama tumekutana huku mbali na Dar about 12000km away jamani, yaani mshumaa wa mapenzi ukawaka tena sasa muda huo nikasema nitautunza usizime.

Basi nikamweleza why nipo huko bush naye akanieleza wapo wanafanya maping survey ya REA ili umeme vijijini uanze aisee alikaa pale town siku 2 lakini uoga wangu ulishinda mechi akaondondoka untouched though outing za kula kuku si mnajua bush huko kuku mzima sijui elfu 4 tu.
 
Ninawasiwasi kwa mujibu wa uandishi wako utakua muhanga wa jipu la vyeti feki. Hufanani na aliepoteza miaka minene to the so called Yunivesite
unataka uandishi mzuri...?
Nenda jukwaa la siasa or kasome akina Takadini😎😎😎😎😎😎
 
Hiyo hadithi yako yaisha lini wanichosha na vipande vipande
 
acheni kumzingua mshikaji, kama mnajua kuandika kianachuo kikuu si muanzishe nyuzi zenu!!?
 
Mkuu,hii mada itaendelea au ndio imeisha! Dah,nimeisoma nikawa najihisi kama vile natizama movie fulani hivi!
Big up Brother.
 
We mtoa UZI yaan una bahati sijui israel alikuwa busy na shughuli gan siku iyo una kunywa dawa ime expire...
 
kama umeoa huyu dem lazima utakua unachapiwa...sio kwa ukunguru huo...unakaa na dem anakuja kutembelea humgongi kwani dadako huyo?
 
Back
Top Bottom