Thanks
Bavaria.
Hizi project zipo tayari kwa badhii ya nchi zilizoendelea kama Japan, USA, Norway, Singapore etc.
Natoa mfano mmoja wa aina mpya ya upasuaji wa moyo.
Kwa mfano, ukifanya operesheni ya moyo Japan au USA, hamna tena kupasuliwa nchi 12 kifuani kama zamani (minimally invasive cardiac surgery- mics).
MICS wanakata inchi 3 baina ya mbavu, wanafanya kazi yao huku moyo unapiga kwa nguvu yake.
Hii endoscopic procedure inamfanya mgonjwa apone haraka, mwili haupati trauma sana, less bleeding and infections and cheaper.
Tokyo, kwa kuwa ardhi ni ndogo, kuna Tokyo mbili. Moja juu na nyingine imejengwa chini ya ardhi.
Kwenye station nyingine za treni, unaingia kwenye shimo kubwa sana. Huko kuna bar, hoteli, maduka na kadhalika.
Unaweza kutembea kilomita 10 ndani kwa ndani na kutokea sehemu nyingine ya mji.
Hata barabara unaweza kuamua kupita chini yake badala ya kusubiri magari na kuvuka pale Roppongi station. Siyo sehemu yote wamejenga hivyo, lakini mifano ipo mingi ya miji ya chini kwa chini iliyojengwa tayari hasa Tokyo.
Mabasi na magari mengi ni hybrid. Na karibu wataweza kuzalisha umeme katika hayo Mabasi na kutumia kuwasha taa za barabarani au shule.
View attachment 262373
Tokyo is a very futuristic city.