The Toxic Lady mwanamke hatari

Military Genius

JF-Expert Member
Mar 3, 2019
760
1,445
View attachment 1487304


Gloria alizaliwa January 11,1963 na kufariki february 19, 1994 mjini California US akiwa na umri wa miaka 31, alikuwa ni mama wa nyumbani na alipewa majina ya 'The Toxic Lady' au 'The Toxic Woman' kwa maana ya ni hatari kumgusa kutokana na tatizo alilokuwa nalo.

Majina haya aliyopewa ni kutokana na kuwa na mwili waajabu pindi tuu akiumwa, Klkila aliyeugusa mwili wake au kuigusa damu yake pindi alipoumwa alikua anapata madhara kama kukosa kabisa pumzi na nguvu, misuli yote kukaza N.K.

Sio kumgusa tuu, hata ukipita hatua mbili toka alipo yeye ilikuwa ni hatari.

Baada ya kuzidiwa na homa February 19, 1994 kutokana na maradhi ya Cancer aliyokuwa nayo, Gloria aliwahishwa katika hospitali ya 'Riverside' kwaajili ya matibabu.

Ajabu ni kuwa manesi watano waliompokea walianza kuumwa ghafla kwa pumzi kukata, misuli kukaza na nguvu kuwaishia baada ya kuugusa tuu mwili wa Gloria!.

Mmoja wa manesi hao alipekekwa ICU kabisa na baadae watumishi wengine 34 wa hospitali hiyo ikabidi waanze kupatiwa matibabu ya haraka kwa kuwekewa mashine za kuwasaidia kupumua baada ya kukutwa na hali hiyo, kisa ni kuugusa tuu mwili wa Gloria.

Wataalamu walipofanya uchunguzi walibaini kuwa Cancer ya Gloria Ilikuwa ikimpa maumivu makali sana hivyo akawa anatumia kemikali aina ya 'Dimethyl Sulfoxide' (CH3)2SO kwaajili ya kupunguza maumivu, ilikuwa Inamfanya akizidiwa tuu mwili wake unakuwa Toxic.

Kemikali hii ni kali mno, Ilikuwa inamfanya mapigo ya moyo kwenda kasi na joto lake lilishuka hadi 18°C, joto la kawaida la mwili huwa 37°C.

Ikabidi Gloria aachwe tuu bila kuhudumiwa kwasababu ilikuwa ni hatari kumgusa, dakika 45 tuu baada ya kuachwa akafariki, inaelezwa kuwa wahudumu wengine 23 waliomgusa hospitalini hapo baada ya kufariki walipatwa na matatizo hayo.

Hata baada ya kufariki pia aliachwa tuu maana ilikuwa bado ni hatari kumgusa, klikuja kuzikwa miezi miwili baadae April 20, 1994 baada ya kemikali hizo kuisha mwilini mwake.
View attachment 1487307
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom