The story of Abidon

wazanaki

JF-Expert Member
Mar 20, 2020
1,092
804
Abidon ni mtu mmoja aliekua mwema na mwaminifu na akiamini kwamba kila mmoja ni muaminifu kama yeye.

Siku moja Abidon alienda dukani kununua kiatu. Alipofika dukani akaona kiatu kizuri sana. Lakini kwa bahati mbaya kiatu kilikua hakijawekwa bei.

Kwa sababu abidon alikua mtu wa imani akamuuliza muuza kiatu "kiatu bei gani". Muuza kiatu akamwambia kiatu hicho ni 100,000/=. Abidon kwa sababu alikipenda kiatu na alikua mtu wa kuamini watu akatoa 100,000 akanunua kile kiatu.

Baada ya Abidon kutoka na kutamba mtaani kuhusu kile kiatu kwa rafiki zake. Rafiki zake wakamwambia. Kiatu hiko umekitoa duka gani. Basi abidon akawaambia. Wale rafiki zake wakamwambia umeibiwa, hicho kiatu juzi tu tumetoka kukiulizia kilikua kinauzwa 20,000/=. Abidon akarudi kwa muuza duka kudai pesa yake.

Muuza duka akamkataa, akamwambia "sikukulazimisha ununue kiatu" umenunua mwenyewe. So imeisha hiyo.

Abidon akaenda mahakamani, kwa kua hakua na ushahidi na ilikua ni agreement ya mdomo. Basi napo hakupata haki akabaki analia na kugalagala. Abidon masikini alikosa haki hivi hivi.

MAUDHUI
Story ya Abidon. Haina utofauti na mikataba inayofanywa Africa baina ya Europeans and Africans on African resources.

Swali: Je, ni nini tatizo kwa viongozi wa Afrika na agreement wanazoingia na Europeans?

Toa maoni yako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom