Msamiati
R I P
- Mar 6, 2011
- 1,063
- 700
Akiwa amepitiwa na usingizi ndani ya nondo za gereza Tarick anasikia nyayo za mtu zikimsogelea Taratibu. Huku akiwa hoi kutokana na uchovu wa kipigo kizito alichopewa na kikosi cha usalama wa taifa kitengo cha upelelezi Tarick anajivuta taratibu na kugeuka nyuma ili kumtizama mtu aliyekuwa akimsogelea, Baada ya kufumbua macho kwa shida Tariki anamtambua msichana mrembo Brenda akiwa mbele yake, Akiwa mtu mwenye majonzi Brenda anachuhumaa pale alipokuwa Tarick na kudondosha machozi huku miguno ya kilio cha uchungu ikisikika.
Kilio hicho kina mfanya Tarick Kuinua sura yake na kumtizama Brenda. Huku akitoa sauti kwa shida na uchungu Tarick anasema "Naona umeamua kuja kunisanisanifu, na kuibariki safari yangu ya kuelekea akhera……. Mlichokuwa mmedhamilia kimeshatimia nini unataka tena…….! " maneno hayoo yanampa simanzi nzito Brenda na kumfanya kububujikwa na machozi yanayoambatana na sauti nyepesi ya kilio, Kwa uchungu Brenda anasema,"Please Tarick usiseme hivyo….. I Love You Tarick , and I promise to be With you until the End". Huku akububujikwakwa na machozi Tariki anamkatisha Brenda na kusema,"What Kind of Love is this?........... Eeh! Nilishakwambia toka mwanzo kwamba ukweli wa mapemzi yako kwangu ni kuachana na mimi, Hatuwezi kulazimisha mapenzi ikiwa hatuendani kwa hali wala Mali. Huu ndio ulikuwa mpango wako Brenda……… Haisaidii kitu kuendelea kunikashifu kuwa unanipenda wakati nimesha hukumiwa kifo……… Haisaidii kitu kiniambia utakuwa na mimi mpaka mwisho wakati nitanyongwa pekeyangu…… Umekuja kunikejeli Brenda……! Mungu awabariki ……" maneno hayo yanazidi kumtia simanzi na kummaliza nguvu kabisa Brenda. Brenda anafuta mchozi na kusema,"Usiseme hivyo Tafadhari,……… ". Kabla hajanyanyua kinywa kusema kauli yoyote Askari anampa taarifa Brenda kuwa muda umeisha, Huku askari akiwa anamsindikiza Brenda kutoka nje alitoa sauti kwa uchungu akisema''sitakuacha Tarick……… Sitakuacha peke yako Tarick niamini Tafadhari………".
Akiwa amedondoka pale chini Tariki alionekana mtu aliye Ghubikwa na mawazo, huku fikra nyingi zikiwaza jinsi atavyo muacha mama yake ambaye katika kipindi hicho alikuwa akimtegemea yeye. Usiku kucha Tarick Hakuweza kupata usingizi, alikuwa mtu aliye jawa na mawazo.
Kesho yake alfajiri Tariki alishtushwa na maji ya baridi yaliyommwagikia na kumpa ukakasi mkubwa kwenye majeraja ya mateso yaliyomjaa mwili mzima.
Kunyanyua sura yake juu ili atizame ni nani iliye kuwa mbele yake, Tarick anamuona Profesa Rweyemam akiwa na wapambe wake, Kwa Dharau na nyodo anasema,"Upumbumbavu wako umekugharimu sana…… Nasikitika sina cha kukusaidia," Profesa Rweyemam ananyamaza kidogo na kuendelea,"ungetumia weledi wako kidooogo… ungekuokoa usiingie katika dhahma kubwa kiasi hiki mpaka inakugharimu uhai wako". Maneno hayo yanampa ghadhabu Tarick anajivuta taratibu kwa kutumia nondo za gereza na kusimama, kisha huku akionesha kutokuwa na hofu hata kidogo Tarick anamjibu,"Nilishawahi kukwambia kuwa elimu yako bado haijakutoa kwenye ujinga……… hapa hakuna cha muhimu unachofanya zaidi ya kudhihirisha wasifu wa ujinga na upumbavu wako unadhani pesa na wadhifa wako unaweza kukufanya uishi milele? unajidanganya wewe ..." . Maneno hayo yanamtia hasira Professa Rweyemam Anamkatisha Tarick kwa Ghadhabu, "Shenzi wewe…… hukumu ya kifo imekupendeza… ". Rweyemamu anaondoka mahali hapo kwa Hasira.
Mpenzi msomaji, Professa Rweyemamu ni mwanasheria mkuu wa serikali na mototo wa aliyekuwa mwanasiasa maarufu nchini. Kutokana na wivu wa mapenzi huyu ndie aliyetengeneza chezo mzima ambao umemtia kijana Taric kwenye Hatia ya kuhusika na tukio la kigaidi jijini Arusha. Hii ni siku ya tatu kabla ya Tarick kupelekwa kwenye hukumu Mjini Dododoma ambako atahukumiwa kunyongwa. Je nini Kitaendelea? Na msichana aliyeanzisha kizungumkuti Hiki Ni hatua gani atakayochukua baada ya kuhusika kwa asilimia mia moja kwenye kasheshe hili.
Fanya nijue kama Tamthilia hii inastahili kuendelea au ipigwe chini fanya hivyo kwa kubonyeza like au Kucomment, Episode 2 inasuburi like 50. Kama umevutiwa na Riwaya Hii Tafadhari bonyeza LIKE.
I dedicate this to you (msamiati) queenkami