§ the returns of mwalimu nyerere §

kapolisi

Member
Jul 18, 2015
25
5
Ni miaka takribani 16 sasa tangu muasisi wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aage dunia...

Mwalimu alifanya kazi kubwa katika kujenga misingi ya nchi yetu.... Na kikubwa ni Imani yake juu ya Maendeleo..... Kuasisi mfumo wa Kijamaa Tanzania na...
Sana alikuwa akipigania na akihubiri maadui wakubwa watatu wa Taifa letu ...... UJINGA , UMASIKINI na MARADHI......

Wakati tunatafakari mema yake ili tuendelee kuyaenzi...... Leo hii zimebaki siku kumi kuelekea kwenye #UCHAGUZI MKUU - 2015#.... Kuna jambo limenigusa kuandika... Ni
#KURUDI KWA BABA WA TAIFA #

Moja ya Falsafa ya kiafrika inaamini.....
KUNA MAISHA BAADA YA KIFO...... FasilI..... Rahisi ya
Falsafa hii ni kuamini... Kuwa maisha ni #duara hivyo..... Kufa kwa mtu Ndio mwanzo wa maisha mapya ya mtu huyo.....
Msingi wa Falsafa ni Kuwa..... Daima
binadamu hatufi... Ila... Tunatimiliza mlinganyo wa maisha..
HIVYO KWANGU NAMUONA MWALIMU YUKO HAI KWA FALSAFA HII..... Kwa Kuwa bado tunaishi nae..... Licha ya Kuwa ni miaka 16 tangu afariki......

Kuna Falsafanyingine ya Jamii inaamini...

HERI KUFA NA MAWAZO YANAYOISHI.... KULIKO KUISHI NA MAWAZO YALIYOKUFA....
Ni dhahiri Kuwa hii ni Falsafa ya kimapinduzi... (inaweza tumiwa na Wana POSITIVISM SCHOOL OF THOUGH)
Na imesheheni... Dhana anuai Kuwa..... Ni vizuri katika maisha ya ulimwengu tuhakikishe pale tulipo... Tunafanya Kila tuwezalo..... Ili kuweka ALAMA..... Katika ulimwengu...... Alama inayorejelewa ni Alama chanya.... Si vinginevyo.... Yaani Wanaokuzunguka..... Watambue mchango WAKO si tu baada ya KIFO chako.....la hasha...... Hata wakati wa uhai WAKO....
MUHIMU...... Huwezi weka Alama katika ulimwengu..... Popote ulipo..... Usipojitambua..... Na kufahamu kwa nini uko hapo ulipo...... Na kutambua.....
Kuwa Kila kitu kina sababu.... HIVYO ZIPO SABABU ZA WEWE KUZALIWA..... Na kuwepo hapo..... Na zaidi upo hapo ulipo kwa kipindi flani tu...... Ndio uanuai wenyewe....
Umuhimu wa Mwalimu si tu umeonekana Leo.... HAPANA...... Ulionekana pia Hata wakati akiwa hai....... Akiwa kwenye madaraka...... Ndio maana..... Alipofariki wengi tuliwaza...... # Inawezekana maisha Bila Nyerere.....???


# NIRUDI KWENYE KIINI CHA MADA#

Hivi karibuni...... Tumesikia na kuona wagombea wakijinadi..... Kwa kueleza umma juu ya ilani zao na matamanio yao..... Wakipewa nafasi flani...... Ni dhahiri...... Yamesemwa mengi na kuzungumzwa mengi.....
Kikubwa kwangu ni...

a) Namna ambavyo wagombea wanatumia mawazo ya Mwalimu Nyerere katika kunadi sera zao.....

b) Wanavyotumia wasifu wa mwalimu Nyerere katika kujitengenezea mazingira ya kisiasa

c) Wanavyotumia nukuu za mwalimu Nyerere katika kufikia malengo kadhaa...... Nk....

YAPO mengi ya kusema hapo

UKICHUNGUZA WAGOMBEA WOTE..... Vyote wamavyohubiri...... Havichezi mbali na Maadui watatu wa Taifa hili...... Aliowataja Mwalimu Kuwa ni
#UJINGA
#UMASIKINI
#MARADHI .......

Muhimu ni Kuwa....... Mwalimu ni mtu muhimu sana katika historia ya nchi yetu na umma wa watanzania kwa ujumla ..... Mwalimu bado tunaishi nae wengi wetu..... Hivyo
Ni vizuri wakati tunatafakari miaka 16 ya KIFO cha Mwalimu.. Huku tukielekea kwenye Sanduku la kura October 25..... Tukafanya yafuatayo
..
1. Tukayaenzi mema aliyotenda Mwalimu.. kwa vitendo..
2. Tukahuisha Falsafa za Mwalimu katika maisha ya dhamana tulizopewa/tutakazopewa.
3. Tukaamini tunaweza Kuwa Kina Nyerere wa Leo... Na kesho...
Endapo..... Tutabeba mizigo ya dhamana tulizopewa / tutakazopewa kwa dhamira za dhati za mioyo yetu .....
Ndio ujumbe wangu kwako.....


MUNGU IBARIKI #TANZANIA....
MUNGU BARIKI #UCHAGUZI MKUU

( Ibrambeya@gmail.com )
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom