The Real Hidden World

KijanaHuru

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2017
Posts
1,822
Reaction score
2,329
Nianze kwa kusema nakumbuka nikiwa bado mdogo mdogo, nilikuwa na sifa moja kubwa sana mtaani kwetu ya ubishi.
Hata kama ulete fact za kiwango gani lakini niki-stickkatika msimamo wangu ni hapo hapo hamuwezi kunibandua hata mngekuwa mia.
Lakini kuna jambo moja aliligundua mzee mmoja siji kumsahau katika maisha yangu yote ningali bado mdogo kabisa miaka 8.
Aliniita na kuniambia
""Nikiamua kuwa na maarifa naweza kuwa nayo, nakuambia hivi si kwamba nimekuona unamaarifa bali nimegundua unaweza kujaza maarifa ukitaka, sasa nakupa kazi jifunze ulimwengu uliofichika ulivyo hautapata nafasi ya kubishana na wengine kamwe'''
Mzee nilimuelewa japo kwa ufupi sana, labda kutokana na umri wangu ulivyokuwa na kuambiwa jambo lililokuwa juu ya uwezo wa frikra zangu.
Nikiwa na miaka 14 ndipo mzee aliweza kunipa kitabu kilichokuwa na Tittle Hii
"Comfort That Kills" Nikitabu chenye page 36 tu lakini ndicho kikabadili ukurasa wangu wa maisha na kunipa hamu zaidi ya kuujua ulimwengu uliofichika.
Nilikisoma kwa kufanya mirejeo mingi sana katika kamusi ya kufasiri maneno ya Kiingereza kwenda kiswahili,
kwanza kilikuwa na maneno mengi ya kiingereza cha zamani sana, kilinipa shida kidogo lakini niliweza kukielewa na kufunguliwa ukurasa mpya wa kusoma Maandishi.
Si kwamba sikuwa msomaji toka mwanzo ila nikwamba usomaji wangu uliegemea sana katika kusoma hadithi za nadharia zaidi zilizoandikwa na waandishi mbalimbali mahiri.
Sasa hapo ndipo nikaaznza kuufukunyua ulimwengu uliofichika kwa fujo zote.
Sio katika Upande wa Dini au Historia tu, bali niliweza kuyajua mabo mengi sanakwa muda mfupi.
Na kadri nilivyozidi kusoma ndivyo nilivyozidi kujua na kutambua ya kuwa katika asilimia 100% huenda nimeijaza asilimia 0.001%(Kwa wasomaji wavitabu wananielewa vizuri hapa maana kadri unavyosoma ndivyo unaona hauna kitu na unahitaji kujaza vitu)

Nilikuwa napitia Thread Za mtu mmoja humu(jina kapuni)
Niligundua jambo moja wengi wanaompinga katika thread zake ni wale wanaoangalia muvi na video za youtube juu ya uhalisia wa ulimwengu tunaoishi, lakini hawezi kuwa na mrejesho hata mmoja juu ya maandishi aliyoyasoma.
Huyu jamaa ameandika vitu vingi ambavyo huenda sikujua kama naweza kukutana na mtu kama huyo hapa, lakini ndipo nikajua kumbe JF ina watu wengi sana wa kila namna (Viva JF)
Sijaja Hapa kuueweka hadharani ulimwengu uliofichika ila ukihitaji kuujua unajulikana kabisa, tena kwa urahisi sana.

Labda unaweza ukakosa Mzii mahala pa kuanzia lakini nakupa kidogo jambo moja.
Jaribu kujifunza mambo kama haya hapa.

Kwa watu wa Imani hasa wakristo na waochimba masuala ya tulikotoka,kwanini iko hivi,kwanini iko vile,imekuwaje,ilikuwaje,jaribu kupitia mambo haya.
-Ni vitabu gani vilimeondolewa katika Biblia
Unaisoma Biblia Leo lakini inavitabu zaidi ya vitano havijawekwa humo
Tafuta kwanini havimo, vinafundisha nini, nk

-Ni nani alikuwa mmiliki wa kwanza wa America(Usiniambie wahindi wekundu nabaadhi ya maneno yaliyopo kajifunze ulimwengu uliofichika)

Naomba niishie hapo kwa Leo, lakini nikipata mda mzuri na nafasi nitaweza kuleta hoja mbalimbali juu ya ulimwengu uliofichika kwa kadiri ya jinsi nitakavyokuwa na muda.


Updates Ipo Page #30 Kitabu Chenye Utata (Kina Uwezo Wa Kujua Wakati Wako Ujao)

Updates Ipo Page Ya #95 Nguvu Za Asili Alizonazo Mwanadamu Kumshinda Mchawi


Updates Ipo Page Ya 128 Nguvu Za Asili Alizonazo Mwanadamu Kumshinda Mchawi Sehemu Ya Pili Na Mwisho
 
Mkuu mimi pia nimefurahi kukutana na mtu aliyeanza safari yake kitambo ya kutafuta yaliyo nyuma ya pazia.

Mimi sina mda mrefu ila najiona nikiendelea kuwa huru siku hadi siku.

Ila neno kufichwa kidogo linanipa shida,siamini kama kunakufichiana ila tu ni uwezo mdogo tulionao ndio unatufanya tusiuone ndio maana anayeuona anashangaa kweli jinsi mwengine asivyouona.

Nisaidie vitabu kadhaa ndugu niendelee kujifunza,maana safari bado changa sana japo mwakani nimedhamiria kupiga hatua ya KISHINDO.
 
Sawa mkuu wala usijar japo kwa internet unaweza pata material nyingi sana ila kwa zingine
unapaswa kuzunguka zunguka katika maktaba za nyumbani hasa za wazee wazee unaweza pata mambo mengi sana mkuu

Nikibahatika kupata vitabu muhimu soft cop nitaviweka hapa
siku nikiwa na wakat mzuri nitaviweka hewani (ambavyo ninavyo vya soft copy)
 
Ok ndugu nitakuwa nikisubiri.

Ila kitu kimoja nimejifunza kwamba sio wote watakaokuelewa mara nyingi kwa maana ni yule tu aliye tayari na anayetafuta ukweli ndio atakuelewa.

Pamoja
 
Vitabu vikwapi!?

Kwa maarifa kuyapata kwa urahisi anza na google unaweza kutana na soft copy nyingi tuu ambazo zaweza kukupa majibu yote zingne zikakupa majibu nusu lakini ndio unakuwa mwanzo wa kujua na jambo lingie la ziada na hatimaye badala ya kujua jambo moja unajikuta hadi unafikaushapitia mambo zaidi ya 50+.
so waweza kuanzia popote wahisi unaweza kupata details
 
Ok ndugu nitakuwa nikisubiri.

Ila kitu kimoja nimejifunza kwamba sio wote watakaokuelewa mara nyingi kwa maana ni yule tu aliye tayari na anayetafuta ukweli ndio atakuelewa.

Pamoja
Nihakika bro ukishaanza kujifunza jambo fulani unakuwa upo ulimwengu mwingine na hapo mtu kukuelewa ni vigumu mno hadi aamue nayeye kuingia katika ulimwengu wako.
Hapo unaweza kupingwa na wengi sana sometimes nilikuwa naambiwa naanza kuchanganyikiwa haswa ukimuuliza mtu asiye sahihi.
Kweli si wote wanaweza kukuelewa
 
mmiliki wa kwanza wa AMERICA ni black kutoka AFRICA na mwafrica alikuwepo sana AMERICA akifanya biashara mbalimbali na hadi kufikia kuweka makazi

usiniquote mimi
muulize
 
Nimesoma soma vitabu kisi chake nikaja gundua hadithi zote ni moja ila inaelezwa kwa jinsi tofauti tofauti-msingi wake mkuu unakuwa ni ridhiki-(kutafuta ridhiki). Hii sasa ndio inajichambua katika milengo mbalimbali kama siasa-hii inatoa matokeo kama vita,ujasusi n.k,uchumi hii inajifunua kwenye maswala km biashara ,ubunifu,usafiri,wizi n.k na mwisho wa siku kuna swala la imani-hii imefichika kidogo lakini ni ridhiki ya kiroho ni kama ustawi wa mtu unavyomfanya kuwa bora basi ndivyo pia ustawi wa kiroho unavyomfanya kuwa bora.kuna kipande kidogo ni kama kipo pembeni ila ni matokeo ya msingi mkuu ambao ni ridhikinamaanisha-Swala la mapenzi, huwa linatokea kama mrejesho(matokeo kabla au baada ya kupata ridhiki) tu kuwa nikiwa katika hali flan,au nikipata kitu flan basi nitaoa,nitakuwa na mpenzi ,nitaenda kutumia na malaya etc.
Sasa katika swala la imani sijisumbui kutafuta sana-kwa sababu ni imani- Yaani kusadiki kile ambacho hakipo kwamba kipona ni hakika,Kwa hiyo huwa sijisumbui sana kutafuta nisije nikapoteza kile nilicho nacho kwa kuwa ingawa kinaweza kuwa kidogo kinanitosha na kwa udogo wake huo huo kinanipa matokeo ambayo nayafurahia.
 
Haya I will try
 
Jaman msije kutuambia tunaenda uko kwa kulala usingizi alafu tukapotelea uko hata mimi natamani kwenda kuchungulia uko dunia inaonekana ina usili mkubwa sana.
 
Jaman msije kutuambia tunaenda uko kwa kulala usingizi alafu tukapotelea uko hata mimi natamani kwenda kuchungulia uko dunia inaonekana ina usili mkubwa sana.

Nikweli broo ni kitu fulani adimu sana
wachache wanajua, muhimu kuujua vyema ni mpaka ujitose uweze kwenda nao sambamba
mambo yake mengi tunayajua kama sumilizi za paukwa na pakawa ila ukweli wake
huenda mtu ukaogopa hata kutembea nje sometimes
ila madhara yake pia yapo inaweza kukufanya ukawa mwana dini sana
ama ndio ukaamua kukengeuka mazima.
sometimes unaweza ukawa kama mwehu maana unachokijua unataka kila mmoja ajua awe salama.
anything can happen
wengine huwafanya kuwa wapole sana na huongezeka busara zaidi na maarifa.
a lot of things utagundua.
but also humfanya mtu ajitambue kwa usahihi zaidi
 
Mkuu wewe baada ya kuupata ukweli uliofichika umekuwa mtu wa namna gan?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…