The Overstating of Understated? or Understating of Overstated? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The Overstating of Understated? or Understating of Overstated?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Aug 28, 2010.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Wataalamu,

  I am abit lost on something here. Kwenye Ilani ya CCM ya 2010-2015 kuna takwimu za mambo ya madini ambazo hazileti maana ukizingatia kuwa pato la Serikali kwa madini lilikuwa asilimia 3 (3%) kabla ya sheria mpya ya madini iliyopita mwaka huu (nadhani) na kuongeza pato kufikia asilimia 4 (4%).

  Sasa ukiangalia haya madai ya CCM kusema mapato ya Serikali kutoka sekta ya madini yalikuwa kiasi kadhaa na kisha kuonyesha mauzo kutoka sekta ya madini kuwa kiasi kadhaa, it makes you wonder nani muongo.

  Ukifanya exchange rate ili kupata mahesabu kwa sarafu moja, inaonyesha kuwa sisi kama Taifa tulipata kama mapato kwa Serikali takriban kati ya 52% hadi 65% ya mauzo ya madini. THen nani anatoa takwimu za kweli na kwa nini CCM itoe takwimu ambazo zinapingana na sera ya madini ya Tanzania kupata asilimia 3 (3%)?

  Je hii ni danganya toto ya kuhutubia takwimu kudhani awatu hatutahoji au kubaini kasoro?

  Mwenye takwimu za Ashanti Gold na Barrick Gold kwa mwaka 2005 hadi 2008 naomba anipe takwimu na majedwali ya mashirika haya kimapato kutokana na uchimbaji wao wa madini Tanzania.

  Nanukuu vipengele vya Ilani ya CCM.


   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Takwimu ni vigumu mno kuzipata, kwani makampuni haya yote yamejenga viwanja vidogo vya ndege ndani ya maeneo yao ya uchimbaji. Ndege huingia na kutoka na madini bila ukaguzi wowote, hivyo siyo rahisi kupata takwimu.
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Majimoto,

  Nikirudi kwenye Ilani ya CCM, kila kilichofanyika ki-Serikali, wanmejitwisha sifa kuwa ni matunda ya kazi zao, lakini yale mapungufu ya Serikali, wao ni rahisi kudai hili ni la Serikali!
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Aug 29, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev. Kihsoka,
  Mkuu wala sijakuelewa swali lako..kwa sababu nachoona hapa ni kwa miaka ya nyuma na viko wazi kabisa.

  5. Imeeleza wazi nini mchango wa madini ktk mfumo wa Taifa kuwa ni asilimia 2. 6 (2008).
  6. imeeleza ongezeko la Pato la serilkali ktk sekta hiyo kwa miaka mitatu. na
  7. Imeeleza wazi ongezeko la sales nje kwa mwaka uliofuata..
   
 5. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,993
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  Mkuu Rev Kishoka,
  Kuna vitu viwili umechanganya hapa,Pato la taifa lina tokana na Utalii,Uvuvi,Kilimo(6.25%), madini, n.k. Sasa hiyo 3% au 4% ni kiasi ambacho madini yanachangia kwenye hilo pato.

  52% hadi 65% ni mahesabu kati yetu na kampuni za madini,Mfano kama tulipata 52% inamaanisha kampuni za madini zilipata 48%.Sasa hizo 52% ukizingiza kwenye pato la taifa ndiyo unapata asilimia 3 au 4.
   
 6. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  haya mambo ya percentage si mazuri hata kidogo... hebu hao ccm watuambie hiyo dhahabu imechimba tani ngapi na nintani ngapi zimeuzwa na wao wamegawiwa kiasi gani maana katika bei ya lei kwenye soko la dunia... an ounce of gold ilinauzwa kati ya us dolaar $1237.90 na $1244.20 source Gold Market Report - gold price quotes and news.

  hawa wachimbaji wamenufaika sana na sijui ni kwanini tusichimbe wenyewe.. najua kuna wale watako sema kwamba vifaa au machine za kuchimbia ni ghali sana.. ni bora tununue vifaa hivyo ghali na pia ni bora tukubali watanzania wachache wanaufaike na tuchimbe wenyewe madini hayo na tuyauze wenyewe kwenye soko la dunia.. hao watz wataonufaika kwa namna moja au nyingine ni bota tukakabana nao mbele kwa mbele lakini kwa mtindo huu .. tutaendela kula hasara mpaka lyamba...
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mapato ya Taifa kutoka kwa watu wa madini kama kodi na si jumuiko kuu la mapato ya nchi kutokana na mauzo ni 3%. Ukiangalia hayo mahesabu ya mauzo ya madini na kilichopata Serikali kutokana na mauzo hayo i zaidi ya 3%!

  On second note, mauzo ya madini ni makubwa ukizungumzia mauzo kama exports kusema ni 3% ya uchumi mzima!
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev. Kishoka,

  Labda mimi nisema nilichokielewa..Na kama nimekosea au sikuelewa vizuri naomba kusahihishwa..

  v) Mchango wa Sekta ya Madini kwenye pato la Taifa umeongezeka
  kutoka asilimia 2.4 mwaka 2005 hadi asilimia 2.6 mwaka 2008.

  - Hapa wakiwa na maana kati ya pato zima la mfuko wa Taifa kutoka makusanyo yote (revenues), sekta ya madini ilichangia asilimia 2.6 (ONLY) ya pato hilo. Hii haihusiani kabisa ile asilimia 3 ya ruzuku isipokuwa ni makusanyo ya kodi zote zinazohusiana na madini ukilinganisha na total revenue tulokusanya kwa asilimia ya mchango wake.

  (vi) Mapato ya Serikali kutokana na uchimbaji mkubwa yameongezeka
  kutoka Sh. 457.4 bilioni mwaka 2005 hadi Sh. 840.0 bilioni mwaka
  2008.

  - Hapa serikali inazungumzia pato (revenue) lililotakana na Uchimbaji mkubwa wa madini ulivyoongezeka.. hii haina maana ndio asilimia 3 ya mchango wa madini ktk mfuko wa taifa isipokuwa ni ongezeko la pato ktk sehemu moja ya sekta ya madini.

  (vii) Thamani ya madini yanayouzwa nje imeongezeka kutoka dola za
  Marekani 727.45 milioni mwaka 2005 hadi dola 1,075.9 milionimwaka 2008.

  - Hii ndio thamani ya madini yaliyouzwa nje (Total sales) kwa ujumla wake kulingana na record ya serikali. Haya ni madini yote ambayo sii lazima yanahusiana na ile asilimia 3 ya ruzuku moja kwa moja kwa sababu wapo wachimbaji wadogo wadogo (wazawa) na kadhalika..
  Kilichokosekana hapa ni maelezo ya kina ni kiasi gani haya mashrika makubwa yaliuza nje na sisi tulikatiwa ngapi toka hiyo asilimia 3 ya ruzuku kisha nasi kumpa Sinclair panga lake la asilimia 1.9 tukibakiwa na asilimia 1.1

  Hadi hivi sasa ningependa sana kujua ni kiasi gani Taifa letu humkatia Sinclair
   
Loading...