THE OTHER HALF
SEASON 1 - THE LEGEND OF ANABELLE
EPISODE 20
SIKU YA PILI
Ni sauti iliyofifia ikigugumia kwa uchungu ndio pekee ilikuwa inasikika kwa mbali sana katika ghala kubwa lenye kiza totoro ambalo lilikuwa na taa moja tu ambayo ilikuwa inajitahidi kuangaza.
Japokuwa giza lilikuwa ni kubwa mno huku kukiwa na mwanga hafifu tu ndani ya ghala, lakini pua zilikuwa na uwezo kabisa wa kusikia harufu ya damu. Damu ambayo ilikuwa imetuama chini sakafuni na kutengeneza kidimbwi kidogo kama vile kisima kilichojaa mchanga na kufanya maji yabaki juu juu tu pekee.
Harufu ya damu haikuwa inaogofya kama ambavyo ilikuwa inaogofya sauti hii hafifu ya kugugumia kwa uchungu.
Haikuwa dhahiri sana ni nini hasa ambacho sauti hii hafifu iliyokuwa inalalama kwa uchungu ilikuwa inatamka. Maneno pekee ambayo labda yalikuwa yanaweza kusikia yalikuwa ni "…natalie…", ambayo yalikuwa yanasikika yakitamkwa na sauti hii hafifu kana kwamba yanatamkwa na mtu aliyeshikwa na kwikwi.
" na…ta…li..e"
Sauti iligugumia kwa uchungu huku ikirudia tena na tena ilichokuwa ikitamka.
Harufu ya damu mbichi ilikuwa imetapakaa kwenye ghala hili kubwa kiasi kwamba mtu ungeliweza kufikiria labda alikuwa ndani ya mto au kisima kinachotiririsha mifereji ya damu mbichi ya binadamu.
Katikati kabisa ya ghala hili kubwa ambapo ndipo taa ndogo ya 'balbu' ilikuwa inawaka kwa mwanga hafifu wa njano, kulikuwa na mnyororo uliofungwa kutoka juu ya paa la ghala kwa kuning'inizwa.
Mnyororo huu uliokuwa unaning'inia haukuning'inizwa hivi hivo tu, bali kuna binadamu aliyefungwa na mnyororo huu.
Mtu huyu alikuwa amefungwa katika namna ambayo alikuwa amesimama na mnyororo umefungwa mikononi mwake na mikono kuvutwa juu ya kichwa. Namna ambayo alikuwa amesimamishwa ilikuwa ni kusimama kwa maumivu makubwa kwa sababu ule myororo aliofungwa mikononi ulikuwa umekazwa kwa kuvutwa juu mpaka kufikia hatua ambayo alikuwa kama amesimama kwa kuchechemea na vidole. Yawezekana labda ni kucha tu ndizo ambazo zilikuwa zimegusa sakafu, lakini mwili wote ulikuwa unaning'inia kwa nyororo iliyofungwa mikononi na kuning'inia angani.
Mwili wake mweupe wa kizungu ulikuwa umechoka kwa maumivu na ngozi ilikuwa imebadilika na kuwa nyekundu kabisa kana kwamba alikuwa amewekwa juani kutwa nzima. Kutokana na kuning'inizwa vile angani kwa muda mrefu huku kucha tu zikiwa vimegusa sakafuni, mikono yote ilikuwa imekufa ganzi na hakuwa anahisi chochote kile kuanzia mabegani kuelekea mikononi, ilikuwa ni kana kwamba mikono imekatika tayari.
Tumboni na kifuani alikuwa na vidonda vikubwa ambavyo viliambatana na michirizi mikubwa ya damu.
Kichwa chake ambacho alikuwa amekiinamisha kama amelala kilifanya majeraha aliyonayo mdomoni yasionekane vyema lakini ikisababisha damu nyingi kuvuja kutoka mdomoni.
Damu ilionekana kwamba ilikuwa imevuja kwa muda mrefu mpaka kufikia hatua kwamba ilianza kutoka damu nzito iliyokuwa inanata kama udenda. Hii ilifanya mdomoni kwake kuwe na kama 'uzi' mwekundu wa damu unaoning'ninia.
Mwili wake haukuwa na hata kipande kimoja cha nguo, alikuwa uchi wa mnyama kama alivyozaliwa na hii ilifanya majeraha yaliyopo mgongoni mwake, kifuani na tumboni yaonekane vyema na kuogofya zaidi hata kuyatazama.
Pamoja na mtu huyu aliyeninginizwa hivi na majeraha mwili mzima ndani ya ghala hili, pembeni yake kulikuwa na mtu mwingine, mzee aliyevalia suti nyeusi tii kabisa na akiwa amenyoa upara ambaye alikuwa kwenye kiti cha chuma anavuta kiko huku anatazama mwenzake aliyening'inizwa kana kwamba anafurahia kumuona katika hali hii.
Lakini si mzee huyu tu pekee aliyekuwemo kwenye ghala hili. Bali pia kulikuwa na kijana ambaye yeye alikuwa amesimama mikono yake imeloa damu, naye alikuwa amevaa suti nyeusi huku kichwani amenyoa upara naye kama yule mzee pembeni yake aliyekaa kwenye kiti anavuta kiko.
KAMA KAWAIDA NAOMBA TWENDE KWENYE TOVUTI ILI KUSOMA EPISODE 20...
TAZAMA JUU PALE KABISA KWENYE "TRENDING" AU NENDA CHINI KABISA KWENYE CATEGORY YA "SHORT STORIES"
jamiiforums.com