Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,786
Huu ndiyo ukweli, nimefika Kenya (Nairobi) mara kwa mara, na hivi juzi tu nilikuwa huko pia, nilichokiona ni kwamba Watoto wanaokuwa sasa hivi yaani kizazi cha leo hasa jijini Nairobi don't give a shit about Kikuyu, Jaluo sijui Kalenjil, wengi wao wanaongea Kiswahili tu kama lugha yao kwanza sheng to be specific, ukiwa mitaa ya Nairobi ni ngumu sana siku hizi kusikia mtu anaongea kilugha lugha na kama ukimuona basi ni wale wazee wa kizamani, lkn vijana wote leo hii wanaongea Kiswahili tu, ukienda Shuleni wkt wa break watoto wanaongea wao kwa wao kutumia lugha ya Kiswahili tu, hivyo baada ya hii generation ya sasa iliyojaa ubaguzi wa Ukabila kupita Kenya mpya itakuwa free of tribalism!