Kwangu mimi Nape Nnauye ni kama Zito Kabwe wote ni career Politicians, hakuna kingine wanajua isipokuwa Siasa, na ni Siasa za Majungu, Fitina na Mipasho, wanaishi hivyo, sasa sijui watu kama hawa unafanya nao nini?
Unajua mtu mwenye profession yake utasema umrudishe labda Chuoni akafundishe, au umkabidhi Chuo Kikuu aendeshe, lkn sasa Nape Nnauye unafanya naye nini?
Kwa maana kiumri kwa kiasi fulani bado ni mdogo, na kuacha kupiga Gitaa sijui ana ujuzi gani mwingine nje ya Siasa, na hiyo ndiyo kwangu The Nape question, what to do with him?
Binafsi si mfuasi wa Nape ila vijana twende vzr na wakubwa zetu. Tuwaheshimu.
Mm nadhani upo nae CHAMA kimoja.
Kupishana mawazo na mitizamo isiwe chanzo cha kejeli, dharau, matusi na kuvunjiana heshima.
Mm siyo muumini wa vyama bali mtu bora. Nape kapitia wakati mgumu sn CCM enzi za JK dhidi ya Lowassa, nk nadhani maisha yake yalikuwa hatarini sn. Ikifikia wakati watu kumuombea kifo. Ila Mungu kamlinda na kamuepusha na roho mbaya
Tuheshimiane kwa utu wetu na tutambue kila mtu ni wa mhimu kwa mchango wake.
Same people hao ......!!The Nape Question?????
Kingereza cha wapi hiki??
Si uandike kiswahili tu kwani ungepungukiwa nini?
Uvccm kumbe kuna akina bashite wengi namna hiyo!
Yah right ...... huwezi kuelewa mambo yaliyokuzidi. Hivi kwa akili ya kawaida tu, wewe unaona haya mambo ni ya kuishia nyuma ya pazia?Mimi siyo Mwanachama wa CCM nitakutana na Nape, wapi? Hii ndiyo sehemu pekee ambayo naweza kuandika nilichoandika, isitoshe kama kweli alistahili hizo sifa ulizompa alikuwa hana haja ya kwenda on air kumshutumu mtu ambaye wako Chama kimoja na ni waajiriwa wa Serikali moja, wangekutana huko na kuyamaliza au kutafuta msuluhishi, kwangu mimi nashindwa kuelewa!
Uvuvi!Mkuu tusaidie na Makonda nae utaalamu wake ni nini?.
Yah right ...... huwezi kuelewa mambo yaliyokuzidi. Hivi kwa akili ya kawaida tu, wewe unaona haya mambo ni ya kuishia nyuma ya pazia?
Huu mtandao unaotumia hapa yani JF, wanadai ofisi zao zilivamiwa. Huyo Nape wako alitoa tako?!! Aliunda tume kuchunguza?? Alienda kuwapa pole na kujua mkasa wote? Alijieleza masikitiko yake yale ya kuanza na KAMA WAZIRI MWENYE DHAMANA!!Hivi unawezaje kumlaumu Nape kwa hatua alizochukua juu ya Makonda......kweli ushabiki unatufanya tukubali upumbuvu uliifanywa na RC......
Ukweli KIswahili ni lugha yangu ya tatu, baada ya kiingereza na kifaransa. Comprenez-vous ?Kajifunze kuandika kwanza
Ww na mm siyo wageni humu. Nakufahamu vzr huenda umdanganye mwingine!!Mimi siyo Mwanachama wa CCM nitakutana na Nape, wapi? Hii ndiyo sehemu pekee ambayo naweza kuandika nilichoandika, isitoshe kama kweli alistahili hizo sifa ulizompa alikuwa hana haja ya kwenda on air kumshutumu mtu ambaye wako Chama kimoja na ni waajiriwa wa Serikali moja, wangekutana huko na kuyamaliza au kutafuta msuluhishi, kwangu mimi nashindwa kuelewa, kwani hata kwenye Kampuni binafsi kinachoamriwa na Mkuu wako wa kazi ndicho hicho na kama hukubaliani nacho basi unajiuzulu nafasi yako au unaacha kazi na sasa unaweza kupinga na kupaza sauti uwezavyo lkn siyo ukiwa bado muajiriwa, kwangu ni ngumu sana kuelewa!
Ww na mm siyo wageni humu. Nakufahamu vzr huenda umdanganye mwingine!!
Uzuri wa Nape hajatetea na wala hajapendelea upande wowote ule ila amesimamia ukweli tu. Acha ukweli uchukue sehemu yake!!
Unae mtetea huyo hana hata robo ya Utumisha ndani ya CCM ukimulinganisha na Nape. Hata in terms of achievement & performance hana!!
Tusiwe vijana wa hovyo ktk Taifa hili. Kama mtu kakosea akanywe au awajibishwe kwa mujibu wa sheria
No Nape anafanya kazi yake kwa mujibu wa cheo chake. Nape alitangaza kwenda Clouds a day before. Kama kulikuwa na tatizo kwa nini hakuzuiliwa!?Ndiyo, hasa linapokuja watu ambao mnafanya kazi kwa muajiri mmoja, kulikuwa na namna nyingi kwa maoni yangu ya kulishughulikia hili sasa picha iliyopo kwangu ni kwamba Nape anapingana na Serikali ambayo ndiyo imemuajiri kwa maana kauli ya Raisi ni kauli ya Serikali, ...
No Nape anafanya kazi yake kwa mujibu wa cheo chake. Nape alitangaza kwenda Clouds a day before. Kama kulikuwa na tatizo kwa nini hakuzuiliwa!?
Haiwezekani watu wapewe madaraka halafu wasifanye kazi zao mpaka wapewe maelekezo. Kama itafanyika hivyo basi huitaji competent persons kwenye hizo nafasi.
Nape kajaribu kufanya kazi independently inakuwa tatizo. Hivi kweli unategemea kesho atakuwa tena na courage ya kutoa maamuzi binafsi kwa mujibu wa sheria na cheo chake?
Kama ni kuyazungumza nyuma ya pazia, kwa nini Makonda au Mkuu hawakumpigia simu Nape pale alipodai hadharani kuwa atakwenda Clouds the following day? Off course sidhani kama kulikuwa na haja ya yeye kama Waziri kwenda Clouds. Angewaita wote ofisini kwake na ushahidi wao.
Hivi Nape anatatizo gani yaani kupinggana na kile kilicho sababishwa na mkuu wa mkoa leo mnamtolea kashfa kwa anayeona kakosea basi amfungulie mashitaka na siyo kumchafua, na wakati huo yeye yupo hapo kusimamia sheria labda nikuulize we mtoa mada hivi wewe ndiyo ungekuwa Nape kwa issue kama hii ungefanyaje kutatua huu mzozo
Kiingereza cha aina hiyo kipo, jaribu tu kujielimisha kuhusu Dunia siku moja labda utakutana nalo tu!