The most powerful business in the world (Biashara kubwa kupita zote duniani)

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
JIFUNZE KITU APA

The most powerful business in the world (Biashara kubwa kupita zote duniani)

Biashara hiyo ni "maneno"

Maneno ni bidhaa, umo utoka

Vitabu
audio dvd, CD nk
Tv,
whatsap, Instagram, Facebook, na Tweter


Njia hizo na zingine nyingi ni kwa ajili ya kusambaza maneno. Maneno ni bidhaa

Kiroho tunaambiwa kwa neno unaumba, hivyo kama hupendi jambo usiliongelee.

Kama unalipenda jambo liongelee sana ili lipate kufahamika na liwe dhahiri. Kwa mfano unakipenda chama chako kiongelee hicho kila wakati, tuma picha za viongozi wako, Serra za chama nk. Ongelea mambo hayo kwa sababu kwa kufanya hivyo unaumba lakini pia kibiashara unatangaza. Biashara matangazo.

Mtu flani kaondoka na sasa si mshirika kama unataka asivume usimpe nafasi ya kumwongelea hata kidogo kwa ubaya au kwa wema. Achana naye na endelea kutangaza habari za chama chako.

Ni kosa la kiufundi kuendelea kujadili habari za mtu aliyesarti popote kama wewe ni mwanachama kindakindaki. Leta jukwaani mjadala kuhusu sera mbadala za chama chako umachokipenda jadili, jadili mwelekeo wa uchaguzi kwa upande wako zaidi maana kwa kufanya hivyo unaumba lakini pia unatangaza. Kwa neno unaumba, biashara matangazo.

Acha kutumia muda wako kujadili bidhaa ya mwenzio, au kwa ubaya au kwa uzuri kwa kufanya hivyo unawapeleka wateja dukani kwa mshindani wako.

Nawaomba ninyi mlio magwiji wa kujadili mada ndani ya jukwaa hili, jitahidini kuliona hilo.

Biashara kuu duniani ni maneno.au utasema taarifa. Unakumbuka serkali sikivu ilivyompandisha Lissu kwa kumjibu majibu yasiyo sahihi? Nayeye anatumia udhaifu wao kujiimarisha kimataifa mpaka akaalikwa na vyombo vikubwa vya dunia kwenda kuuza bidhaa zake.

Hawakuishia hapo biashara ya maneno imezaa faida ya kumtoa mwanadiplomasia mahili katika nafasi yake na kumuuza kwenye sheria lakini mwanasheria kumuuza kwenye diplomasia. Yawezekana usione faida inayotokana na BIASHARA hii ya maneno lakini inalipa.

Nendeni serkali za mitaa mkiwa mmeuza bidhaa/SERA MBADARA hakikisha watu wote tunaielewa faida yake itakuwa kubwa kuzidi 2014.

*Uza bidhaa yako sasa* .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom