The Magufuli's most daring projects in Tanzania

Maswa Yetu

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2023
Posts
1,399
Reaction score
2,601
1. Ujenzi wa bwawa la umeme.
Mradi wa ujenzi wa bwawa la umeme pale Rufiji ulikuwa unapata upinzani mkali tangu enzi ya baba wa taifa mwl Nyerere.

Wasomi wa ndani ya nchi na wasomi wa kimataifa walipinga mradi huo, wafadhili walipinga mradi huu. Mabeberu waligundua njia rahisi ya kuukatisha tamaa mradi huo ni kuwaambia watanzania kuwa ujenzi wa bwawa ni gharama kubwa sana na pia ni kuharibu mazingira kwani mradi huo ungefanyika ndani ya hifadhi ya Selous ambayo ni urithi wa dunia.

Mbunge wa Geita Mh Kasheku Musukuma anasema kabla mradi haujaanza walichukuliwa wabunge kadhaa akiwemo na yeye kwenda kutembezwa kwenye eneo utakapofanyika mradi huu, walikuta pori kubwa na Kimondo, wakiwa mule porini wanashangaa Magufuli aliwapigia simu na kuwaambia kuwa waheshimiwa wabunge aminini kuwa hapo kwenye kimondo tutajenga bwawa kubwa la umeme lenye uwezo wa kudhalisha megawatts 2115. Musukuma anasema wabunge waliguna kwa sababu hakuna aliyekuwa anaamini kama akisemacho Magufuli kitafanikiwa.

Mabeberu walitumia kila njia ikiwemo kuhonga baadhi ya watanzania kupinga mradi huo, pia mradi huu ulisababisha Tanzania inyimwe misaada kwa kisingizio kwamba inaharibu urithi wa dunia kwenye eneo la Selous.

Pamoja na vitisho vyote Magufuli alisema Tanzania inajenga bwawa la umeme liwalo na liwe.

2. Kuhamishia serikali yote Dodoma.
Huu mradi ulishindikana kwa miaka zaidi ya 40, na kushindikana kwake ni kwa sababu kuna baadhi ya viongozi wa serikali walikuwa wananufaika kwa kuipangishia serikali kwa gharama kubwa kwenye majengo yao.
Magufuli alilijua hilo na alipoingia alitangaza kuwa serikali inaenda Dodoma na kiongozi yoyote asiyekubalina na hilo aachie ngazi mara moja. Wizara zilianza kuhamia UDOM kama makazi yao ya muda kabla majengo ya wizara zao hayajakamilika.

3.Ujenzi wa Treni ya umeme.
Hayati Magufuli wakati anaingia madarakani alikuta Kenya wamejenga reli ya standard gauge inayotumia dizeli kwa gharama kubwa sana na walikuwa wanajivuna sana nayo.
Magufuli akatangaza kwamba Tanzania itajenga reli ya standard gauge inayotumia umeme na siyo dizeli kama ile ya kenya.

Watu wakajiuliza kama reli ya Kenya inatumia mafuta ya dizeli na ni gharama kubwa kiasi hiki je reli ya kutumia umeme itakuwaje gharama zake?

Hili lilimtisha hadi rais msitaafu Kikwete akahoji we Magufuli utauweza mradi wa Reli ya umeme?

Magufuli badala ya kwenda kwa wachina alienda kwa waturuki na ujenzi wa reli ya umeme ukaanza mara moja kwa gharama nafuu kuliko zile za wakenya. Yani reli ya umeme ikajengwa kwa gharama nafuu kuliko reli ya mafuta!!!
 
Lilikuwa na mapungufua yake lile jamaa, lakini huenda tungepiga hatua kadhaa kimaendeleo..

Huyu wa mi5 tena, hana la maana, miaka itaenda sisi tunarudi nyuma ama kusimama.. Ni kama gari inavyopishana na miti, tanzania ndio mti wenyewe na gari ndio miaka.
 
1. Ujenzi wa bwawa la umeme.
Mradi wa ujenzi wa bwawa la umeme pale Rufiji ulikuwa unapata upinzani mkali tangu enzi ya baba wa taifa mwl Nyerere.

Wasomi wa ndani ya nchi na wasomi wa kimataifa walipinga mradi huo, wafadhili walipinga mradi huu. Mabeberu waligundua njia rahisi ya kuukatisha tamaa mradi huo ni kuwaambia watanzania kuwa ujenzi wa bwawa ni gharama kubwa sana na pia ni kuharibu mazingira kwani mradi huo ungefanyika ndani ya hifadhi ya Selous ambayo ni urithi wa dunia.

Mbunge wa Geita Mh Kasheku Musukuma anasema kabla mradi haujaanza walichukuliwa wabunge kadhaa akiwemo na yeye kwenda kutembezwa kwenye eneo utakapofanyika mradi huu, walikuta pori kubwa na Kimondo, wakiwa mule porini wanashangaa Magufuli aliwapigia simu na kuwaambia kuwa waheshimiwa wabunge aminini kuwa hapo kwenye kimondo tutajenga bwawa kubwa la umeme lenye uwezo wa kudhalisha megawatts 2115. Musukuma anasema wabunge waliguna kwa sababu hakuna aliyekuwa anaamini kama akisemacho Magufuli kitafanikiwa.

Mabeberu walitumia kila njia ikiwemo kuhonga baadhi ya watanzania kupinga mradi huo, pia mradi huu ulisababisha Tanzania inyimwe misaada kwa kisingizio kwamba inaharibu urithi wa dunia kwenye eneo la Selous.

Pamoja na vitisho vyote Magufuli alisema Tanzania inajenga bwawa la umeme liwalo na liwe.

2. Kuhamishia serikali yote Dodoma.
Huu mradi ulishindikana kwa miaka zaidi ya 40, na kushindikana kwake ni kwa sababu kuna baadhi ya viongozi wa serikali walikuwa wananufaika kwa kuipangishia serikali kwa gharama kubwa kwenye majengo yao.
Magufuli alilijua hilo na alipoingia alitangaza kuwa serikali inaenda Dodoma na kiongozi yoyote asiyekubalina na hilo aachie ngazi mara moja. Wizara zilianza kuhamia UDOM kama makazi yao ya muda kabla majengo ya wizara zao hayajakamilika.

3.Ujenzi wa Treni ya umeme.
Hayati Magufuli wakati anaingia madarakani alikuta Kenya wamejenga reli ya standard gauge inayotumia dizeli kwa gharama kubwa sana na walikuwa wanajivuna sana nayo.
Magufuli akatangaza kwamba Tanzania itajenga reli ya standard gauge inayotumia umeme na siyo dizeli kama ile ya kenya.

Watu wakajiuliza kama reli ya Kenya inatumia mafuta ya dizeli na ni gharama kubwa kiasi hiki je reli ya kutumia umeme itakuwaje gharama zake?

Hili lilimtisha hadi rais msitaafu Kikwete akahoji we Magufuli utauweza mradi wa Reli ya umeme?

Magufuli badala ya kwenda kwa wachina alienda kwa waturuki na ujenzi wa reli ya umeme ukaanza mara moja kwa gharama nafuu kuliko zile za wakenya. Yani reli ya umeme ikajengwa kwa gharama nafuu kuliko reli ya mafuta!!!

Magufuli ametawala muda mfupi ila amefanya mambo mengi sana
 
Hata wasipokuja hapa lakini umeme wa bwawa wanatumia
Si ni pesa za wananchi zilizotumika na hata kama alikopa, bado wananchi watalipia kwa kodi au rasilimali za nchi kutumia kwa bei rahisi..

Magufuli alikuwa kiongozi mzuri kwenye physical infrastructures, hakuna wa kupinga hilo Ila huku kwingine hakuwa vizuri. Kwa hiyo kama kuna watu hawatompenda kwa sehemu alizopwaya na wewe ukampenda kwa maeneo aliyoweza

Nyote mpo sahihi
 
Kwani sasa hivi pesa za wananchi zimepotelea wapi
 
Kwani vinavyomalizia hiyo miradi ni pesa zimetokea mbinguni mkuu

Kila kizuri hakikosi kasoro zake na kila kibaya hakikosi uzuri wake. I hope wafuasi wa Magufuli na siasa mtaacha kapara watu wenye mitazamo tofauti na mnachokiamini 🙏🏽
 
Hivi huyu mama atakumbukwa kwa zuri lipi? Maana Kila nikilitafuta silioni.
 
Back
Top Bottom