The Lesson Africa can learn from China!

Masanja,
Nimependa points zako, Afrika itakombolewa na waafrika wenyewe na adua mkubwa wa Afrika ni sisi wenyewe waafrika.....China ni beast anayekwenda out of control!!!!!!!. Hao mabwana walikuwa masikini na sasa wanajua utamu wa mali, dhamira zao ni mbaya na wana ile attitude ya "by any means neccesary." China si mfano mzuri wa kufuatwa hasa na nchi zetu za kiafrika!!!
Wanacho fanya China ktk Afrika ni kuchukua chochote kinachowafaa na kumwaga uchafu wao wa bidhaa duni ktk masoko yetu. China wana-loose manufacturing jobs ktk kasi ya kuzidi USA in the last two years.......hivo basi china ni lazima i-expand markets zake kuweza ku-sustain the labor force back home!!!. Kwa kifupi hamna anayetutakia mazuri kama sisi wenyewe hatujitakii mazuri, toka lini ukataka kuchukua mfano kwa nchi yenye citizens wake wanaoitwa immigrant laborers within its own border??. Kama unatoka Tibet kwenda kutafuta kazi mashariki ya China lazima uwe na kibali cha kufanyakazi na kuishi, la sivyo ni illegal na utanyanyasika kama "wanyola" ndani ya USA..........huo kama si muujiza ni nini?.
China ni HATARI in capital letters!!!!!!!!.
 
Wasee,
Legacy ya Nyerere ipo wazi na ni polarizing, mie nimekulia Daslam ya Duka la Kaya, suruali za midabwada, nilikuwa na vaa raba mtoni na degriz(jeans) utotoni toka ulaya kwasababu my step father alikuwa Captain wa P&C. Maisha yalikuwa magumu sana in the 80s, kuna pesa lakini hakuna vitu madukani.........kipindi cha mikingamo kilikuwa ni majungu matupu!!!. mazungumzo baada ya habari ni disaster na sumu miongoni mwa bongo za watu, daladala kwa foleni, safari ya Tanga kwa basi la kamata inachukua hadi siku tano kama una bahati mbaya na inabidi uwe na mwamvuli in case mvua ikinyesha.
Mie nimekulia kwenye nyumba ambayo Nyerere alikuwa anapigwa madongo kula kukicha na nilikuwa namwona mtu mbaya sana. Lakini sasa nikiangalia nyuma kuna mabaya yake na mazuri yake kwani nimekuwa na si tena bibi yangu anayenijaza blanks zangu kichwani. Tanzania viongozi wetu toka uhuru wote ni evil doers, lakini Nyerere labda naweza kusema alikuwa na dhamira nzuri, iliyokuwa complicated, bila watendaji waaminifu na ika-fell miserably....it was sad to watch!!!!!!!!!. Sidhani kama leo hii ndani ya 'Daslam' kuna mambo ya jiko limenuna ati kwasababu tu kwenye duka la mchaga au mpemba mchele wa mdundiko umekwisha, hata 'msasa' ilikuwa ni ishu....ukikamatwa na bunda la mineli ati wewe nawe ni muhujumu wa uchumi. Tanzania ni complicated sana..........!!
Achaneni na Nyerere, tusonge mbele kwani yaliyopita si ndwele tugange yaliyopo na yajayo.
 
China si mfano mzuri wa kufuatwa hasa na nchi zetu za kiafrika!!!

Mkuu Y,

Hao wa-China, wanapiga risasi hadharani viongozi wezi, huo ni mfano wa kuigwa mkuu, can you imagine Karamagi, akuwekwa shaba pale monument kwa mkataba wake mbuzi, unafikiri viongozi wetu wataiba tena? Subutu!,

Binafsi sizimii sana na wa-China, maana ninajua kuwa wao ni wahuni mno kuliko wazungu, lakini angalau wao wanajua kula na kipofu, angalau wanakupa kitu cha kuonyesha kwa wananchi wako kama uwanja mpya wa mpira wa taifa!

Ni kweli enzi za Mwalimu, waya ulikuwa mkali, lakini tuliweza kubanana humo humo, sasa mkuu tunajaribu hata kujikunja humo humo lakini damn! mambo ni mazito mkuu unajua bei ya petroli sasa mkuu?


jana mkuu mmoja aliniambia "..Sikiliza kijana tatizo sio mikataba ya Buzwagi, tatizo ni maisha yamekuwa magumu mno.."
 
Field Marshall Es,
Kama nimekuelewa vizuri mada hii inatusihi kujifunza toka China na sio kuikumbatia China kama ndiye rafiki yetu. Sasa imekuwaje hoja zimefikia ktk kutafiti uchaguzi wa Zimwi lenye unafuu?...(West against the East)
nadhani mengi yapo tunatakiwa kujifunza toka hawa jamaa na tuyafanye sisi sio kuwaita wao ama wageni wengine wowote kuja shirikiana nasi ktk ujenzi wa Tanzania.
China wameona thamani ya nchi yao, watu wake na viongozi wake kisha wakizijengea siasa bora ya kiuchumi ambayo inalingana na mazingira yao.
Kama hatutaweza kuthamini kile tulichokuwa nacho kwanza kisha tukajenga misingi ya kiuchumi ambayo italinda kwa madhumuni ya kuendelea uchumi wa nchi yetu hatuwezi kamwe kupiga hatua yeyote zaidi ya kujiburuta kwa tumbo. Kuiga mikakati ya nchi kama China haina maana tumegeuka kuwa Malaya wa China kwa sababu hata hii mikakati ya kiuchumi tunayoipokea tokea IMF inatengenezwa kwa kila nchi duniani maskini na sijawahi kusikia mtu akisema sisi ni watumwa wa hawa IMF.
Nina imani kubwa kwamba kuna mengi ya kujifunza toka kwa hawa jamaa kwa sababu sote tulikuwa ktk siasa za Kijamaa. Mapungufu yote yaliyotokana na Ujamaa wenzetu wamefanikiwa kuyapatia tiba na wakaendeleza yale yaliyokuwa mazuri.
Sisi Upande mwingine tumetupa kila kitu kinachohusiana na Ujamaa na kujenga mfumo mpya wa Kibepari - Kila mtu na mzigo wake!.
 


Mzee ES,
Samahani mzee usinicheke, lakini nimesikia kwamba TIPPER haipo tena!!!. Sasa hilo tatizo la bei ya petroli kuwa kubwa si wao ndio wameileta.......ndio maana mie nilisema maisha bongo na system kwa ujumla ni complicated sana. Hatuwezi kujifunza toka kwa yeyote, ila ni sisi wenyewe kuja na formula yetu ya kujinasua toka hapa tulipo.
 
Kama Tipper haipo tena basi sasa naanza kuamini niliyowahi kuyasikia. Inasemekana mke mdogo wa JK atamiliki shirika litakalochukua mamlaka hayo, share na jamaa wa Quatar!
Hizi ni tuhuma zinazotembea mjini!
 
Mkandara,
Hayo hapo chini si maelezo yangu,bali ni ya mtu aliye 'daslam' na mwenye hasira juu ya kinachoendelea........hiyo ni nukuu fupi ya maelezo marefu ktk mazungumzo yetu. Hapo ndipo nilipostuka, alaaa kumbe Tipper ni marhumu? ndio maana nikamuuliza ES,kama hiki kitu kipo au ni yengele lingine la mtaani.

"Bei ya mafuta ndiyo chanzo cha mlipuko huu wa bei tunao uona, lakini misomi ujinga hii tuliyonayo hata mara moja haisemi ukweli juu ya hili.Bei ya mafuta inapanda kutokana na manunuzi ya mafuta hufanyika kwa $ na ukiilinganisha na Tsh, $ inapanda kila siku hivyo kufanya bei ya mafuta kupanda siku hadi siku, nani aliyeleta soko huria? ni kikwete aliyeondoa TPDC na hatimaye kukifunga kiwanda cha TIPPER!? ili kuruhusu wafanyabiashara walete wenyewe mafuta ndipo wawauzie wananchi pamoja na serikali yenyewe kwa lengo la kunufaisha Umason wao!. TPDC ilikuwa inanunua mafuta kwa mkopo toka nchi za kiarabu{MWINYI'S ERA} Kisha hupeleka TIPPER kuyasafisha na kuuzia makampuni ya mafuta kama vile BP, SHELL, nk na kiasi kingine tulikuwa tunauza ZAMBIA, ZAIRE,BURUNDI,RWANDA,UGANDA,na MALAWI. TIPPER ilikuwa inamilikiwa na serikali ya TZ 51% ITALY 49%. Jiulize kwa nini tulivunja TPDC na kufunga TIPPER? hivi vyote huyu njemba anavifufua na kuendelea kuwa chini ya serikali na si wawekezaji wa kimason."

Mwisho....kama umeelewa jamaa anatupa lawama kwa awamu ya tatu na kutoa credit kwa awamu ya nne, mie sina shule kabisa ya hali halisi mtaani mjini daslam na Tanzania kwa ujumla. lakini kutokana na maelezo hayo hapo juu Tipper na cousin wake TPDC wote ni mahayati.
 
By Steve Schifferes
Globalisation reporter, BBC News

China's rapid economic growth has created huge companies, but most of them are owned by the state.

Now the Communist Party is embracing businessmen in its drive to modernise the country - but it faces growing accusations of corruption.

In the provincial town of Liuzhou, 1,200 miles south-west of Shanghai near the Vietnamese border, town officials held a banquet for GM executives and journalists to celebrate GM's investment in a new engine plant at formerly state-owned Wuling, China's leading maker of small minivans.

Leading the toasts was Liuzhou's most important official, who hailed GM's investment and hoped that more multinationals would invest in Guangxi Province to help boost people's standard of living.

That toastmaster, however, was the head of the province's Communist Party, who is in a battle to gain a growing share of China's booming car industry.

In September, he won a significant victory, when the government named Liuzhou as one of four "designated secondary centres" for the production of auto spare parts - a fast-growing segment of the Chinese auto industry.

State-directed capitalism

The auto industry encapsulates all the strengths and weaknesses of China's state-directed capitalism.

Car production in China is growing so rapidly that it is set to overtake the US within a decade as the world's largest market, and multinationals are flooding in to invest.

But all foreign multinationals must find a Chinese joint-venture company, which takes a majority stake in the business, and nearly all these Chinese companies are state-owned.

In Shanghai, GM was lucky to find Shanghai Automotive (SAIC), China's largest car company, as its partner.

As SAIC was owned by the Shanghai municipal government, it found no difficulty in finding new sites to expand its business in the new Pudong district.

And it had no problems getting suppliers - as the government even owned its own parts company.

The Shanghai government was also instrumental in helping the other early investor in Shanghai Automotive, Volkswagen, with its markets. All 20,000 municipal taxis in Shanghai are Volkswagens and made locally.

In return for its help, the government requires foreign car companies to share their modern technology with the state companies, thus helping them modernise both the production line and introduce new equipment in the cars.

GM has no regrets about its relationship with a state-run, party-controlled business.

GM boss Rick Wagoner says the Chinese managers have a "very professional" approach and that GM has benefited from party backing in smoothing the way for it to produce in China.

Uncontrolled expansion

The symbiotic relationship between foreign multinationals and local party officials also applies even more to overseas Chinese businessmen, who are being enticed to invest back in the mainland.

Much of Shanghai's property boom has been fuelled by Hong Kong Chinese investors, who have built many of the huge shopping malls and skyscrapers that have transformed the city.

And as the Chinese government owns all the land in the city, property developers are sold mere leases, which are auctioned off to the highest bidder.

The profits from the sales go to the municipal government, which has used the money to build the vast new infrastructure of roads, ports, airports and 12 underground lines which has transformed the city.

Until recently, it was relatively easy for the government to clear the land it wanted for development, relocating thousands of Shanghai residents to new housing on the outskirts of the municipal region.

And its control of the planning system meant that there was no conflict, and no delay, over planning permission.

It was in the interest of the government - bent on the expansion of Shanghai - to get the maximum value out of each site's land value, by building high-rise apartments for the rich or commercial office blocks.

Crackdown

But the system also encouraged corruption.

Businessmen were encouraged to join the party, while insider deals were common.

Last September, the secretary of the Shanghai municipal committee of the Communist Party, Chen Liangyu, was sacked from his post for corruption.

He has been accused of diverting money from Shanghai's $1.2bn pension fund to help finance building projects through dummy companies controlled by him and his business allies.


Mr Chen was also implicated in a real estate scandal in 2003 that led to the imprisonment of leading property developer Zhou Zhengyi, once named China's 11th wealthiest individual.

The dismissal and trial of Mr Chen is part of a broader campaign by the Chinese government to stamp out the perception of widespread corruption among party officials.

Revelations have included the denunciation of corrupt officials who kept mistresses while indulging in expensive foreign goods and trips abroad.


CORRUPT COMRADES
1998: Beijing mayor Chen Xitong jailed for corruption
2000: Scores of officials implicated in smuggling scandal in Xiamen
2001: Mayor of Shenyang and his deputy sentenced to death for land deals
2003: Shanghai property tycoon Zhou Zhengyi jailed for corruption
2006: Shanghai party boss Chen Liangyu sacked for diverting pension fund money into property deals

The party fears that corruption will undermine the legitimacy of the party, at a time when - despite economic growth - many people are suffering from rapid economic change.

The gap between rich and poor is growing, while state provision of health care and pensions is declining.

But the prosecution is closely linked to a power struggle within the party. As a politburo member, Mr Chen is allied to former leader Jiang Zemin, who strongly backed Shanghai's headlong dash for economic growth.

Unbalanced growth

Beyond the corruption scandals, there is a bigger problem for China's state-directed capitalism.

That is the competition between regions for economic growth and - ironically - the inability of the central government to prevent overexpansion.

Shanghai's premier state-owned company had traditionally been Baosteel, now the world's fifth-largest steelmaker, which also supplies the Shanghai car industry with its basic raw material.

Baosteel has been on an aggressive expansion programme - as have other Chinese steel companies, buying up other companies and listing some of its shares on the Hong Kong market.

It has plans to double steel production again, buying iron ore companies in Brazil and building a huge new plant in Shenzhen, the booming province near Hong Kong.

And those plans were strongly backed by the Shanghai party, which had close ties to Baosteel's boss, also a party member.

But the virtual doubling of steel production by China has led to a glut of steel on the world market, as well as questions as to whether the breakneck expansion can continue.

For now, China's booming economy is absorbing all the steel it can produce, despite the attempts by central government to slow growth by raising interest rates.

But if growth were to slow, the damage to Baosteel's balance sheet and its workforce could be severe.

And then, the competence of the party to run the economy - even with the advice of businessmen - could come under fire.

This article is part of a special BBC News series on 'Ruling China'.

Story from BBC NEWS:
http://news.bbc.co.uk/go/pr/fr/-/2/hi/business/7044541.stm

Published: 2007/10/15 22:26:09 GMT
 
Icadon,
Thx kwa story hiyo ya BBC, kwani ime-paint picha nzuri ya China!!. Kitu kizuri ktk system ya China kama ilivyoonyeshwa ktk story ni kwamba muwekezaji wa kigeni lazima awe na partner wa kichina......tunaweza kuiga hiyo toka China. Vinginevyo tutafute formula yetu wenyewe,........
 
Uchina ni nchi iliyotoka mbali na inao ustaarabu wa 'kale'kabla hata ya kumbukumbu za kimagharibi kuanza kuwekwa. wazungu walijaribu kuiangamiza uchina kupitia bangi na madawa ya kulevya...ikapelekea kwenye vita inayojulikana kama 'opium war. halafu wajapani wakaivamia uchina na kuunda taifa linaloitwa 'republic of manchukuo'. at that time wamarekani through the League of Nations wlinyamaza kimya....hadi ple Wajapani walipovamia Pearl Harbour.

Wachina waliungana na wamarekani kuwatimua wajapani, ambao kwa hakika walifanya unyama mkubwa sana huko uchina as demontstrated by the Rape of Nanking. Huwezi kuamini kwamba Menyekiti Mao na Wamarekani walikuwa damu damu kwa vile adui yao alikuwa mmoja: Mjapani.

Vita ilivyokuwa inaisha wamarekani wakataka kukabidhi nchi kwa Chiang Kaishek...ndipo Warusi (Stalin) akawaunga mkono kundi la Mao (Wakomunisti) ambao walmtimua Chiang ..aliyekimbilia kisiwa cha Taiwan na kuanzisha Republic of China.

Kusema kweli Mao hakuwa binadamu wa kawaida. very intelligent, katili, mfuska, mpenda kusoma vitabu mbavyo amepiga marufuku wengine wasisome. akaanzisha mapinduzi ya kilimo..yaliyosababisha njaa kubwa iliyoua wachina wengi kuliko waliokufa kwenye vita zote mbili za dunia! hakuishia hapo, akaanzisha 'mapinduzi ya utamaduni ' which was basically a purge against internal opposition. watu wengi waluuawa na kuteswa hata na watoto wao wa kuzaa wenyewe.

Ukomunisti wa china na ule wa urusi ulikuwa sawa na mapacha wa kike na kiume! actually there was a big schism because the soviet union wanted to treat china as a junior parter in 'spreading the seeds of communism around the word, something which chairman Mao did not agree with.Anyway walisaidia sana ukombozi wa bara la afrika, pia tusisahau reli ya uhuru.

Anyway watanzania tukaanza kuiga siasa za wachina kuanzia villagization, azimio la arusha hata cultural revolution. madhambi na maovu yaliyowakumba maelfu kwa mamia ya watanzania katika 'operesheni vijiji' yanasimuliwa hadi leo na kamwe hayatasahaulika. tukawaiga wachiina hadi kwenye mavazi...'kimao ama kimau' likawa ndio vazi la viongozi wa taifa! utashangaa ukienda china sasa hivi kila kiongozi amekuvalia suti 'armani style'. hapa bongo ni mzee kingunge na malechela ndio wamebaki na vimao!

UCHINA ilibadilika sana baada ya kifo cha mao. mtakumbuka kwamba mke wa mao na 'genge' lake la wazandiki waliwekwa ndani na mzee Deng Xiaoping ambaye ndiye anaaminika kuwa muasisi wa sasa wa 'Chinese economic miracle'. 'Free market socialism' imeleta maendeleo makubwa na ya haraka sana uchina ndani ya kipindi cha miaka ishirini tu! wachina sasa wanarusha sateleiti, wachina sasa ndio wakopeshaji wakubwa wa serikali ya marekani ( the value of US Treasury bills in chinese hands exceed 1trillion dollars. now that is very serious money!).

maendeleo ya kiuchumi yameleta kujiamini..china can now 'throw its wait around the world' na sio tena taifa la kusukumwa na kudharauliwa. one area where i have tremendous respect for china is the way they fight corruption.kosa la kula rushwa na ubadhirifu uchina..adhabu yake ni kunyongwa! we have seen the party boss in shangai executed, we have seen the head of the drug administration excecuted! HAYA NDIO YA KUJIFUNZA KUTOKA CHINA.
Naweza kuendelea kuandika mengi kuhusu china...ila inabidi watu wajue uchina ilikotoka.
 
kosa la kula rushwa na ubadhirifu uchina..adhabu yake ni kunyongwa! we have seen the party boss in shangai executed, we have seen the head of the drug administration excecuted! HAYA NDIO YA KUJIFUNZA KUTOKA CHINA.

Tunahitaji mfano wa kiongozi mmoja tu pale Monument, wallahi itakuwa mwanzo na mwisho wa haka ka-mchezo ka-Buzwagi!

Ahsante mkuu, Prince, maneno mazito!
 

Wakulima husema jembe likivunjika Mpini, usitupe jembe lenyewe!
Tanzania baada ya kuukosoa Ujamaa tulitupa hata jembe lenyewe wakati hatuna ujanja wa kufua chuma! matokeo yake ndio haya.
Ujamaa bado haujafa kabisa...China ni mfano bora - Free market socialism! ndio silaha kubwa ya mchina kiasi kwamba Mmarekani ameshindwa kuelewa hiyo nidhamu ya Mchina kwa nchi yake na Wachina kwa Ujumla.
Soon kuna uwezekana Korea ya kusini na kaskazini wakafunga ndoa....Heee heee mtakoma. Korea kusini wana technologia, North wana Population.. kazi ipo - far east will be the next economic power house!
 
China!
Watu wengi wanaitazama china kwa muono wa mbali na sio wa karibu. China imeanza harakati za mapinduzi kwa muda mrefu sana. Kwanza let see where is China coming from before we jump and shot the gun.

China began experiment with central planning economy in 1949, when communist defeated the nationalists in a long and bloody civil war. Leo viongozi wa China wanaiuta uchumi wao " Socialism with Chinese characteristics". Honest there is no country posible on earth that has done more for its people economically over the past two decades than China.

Kuanzia miaka ya 1949 mpaka kuanzishwa kwa reforms mwishoni mwa miaka ya 1970s, China ilikuwa mfumo wa kiuchumi wa kipekee. Uzalishaji wa katika sector ya Kilimo ulifanywa kwa makundi makundi ya wanchi which formed production brigades and production units. Wanakijiji walikuwa ndio responsible kuandaa nini kilimwe kwa chakula na kwa biashara.

Mwaka 1979 government ya China ilianzisha agricalture reforms ambayo iliongeza working incentives in this sector. Then kulianzishwa vitu kama township and Village enterprises (TVEs, hii organization iliweza kuajiri meneja ambao walitoa strategy. manaja wa TVE alikuwa responsible kwa faida na hasara.

One thing China have and its not in Africa is patience. So, unaweza kuona china imeanzia mbali, haija amka tuu asubuhi na kuwa China of today.

I know alot of you believe china is socialism, this is not true at all. In 2002 China allow wafanyabiasha matajiri kujoin Cummunist party, na many reform has been done kuvutia wawekezaji, this include laws concern private property. Kingine kilicho sababisha China kufika hapa ni kujiunga na Hong Kong mwaka 1997. Kuanzishwa kwa WTO which remove alot of trade barriers between countries which boost china economy kwa percent kubwa sana.

Foreign Direct Investment kutoka makampuni makubwa ya US, sababu China has low political and culture risks, many companies from US move to china in ealry 1990, this was due to high incentives from Chinese goverments. Chines government own a large shipping agent in China, this attract many investors. So, all in all there is alot of features that are found in China and they are not in Africa.
 

Na bado Kuna sehemu haruhusiwi kuwekeza hata kama watakuwa na mzawa badala yake wazawa ndiyo wanaruhusiwa na serikali inatoa mikopo kwenye hilo,Hii ni kwa maslahi ya Taifa!
 
China's vice-president loses post



Zeng Qinghong was appointed vice-president in March 2003

Who are tipped to take over? New generation leaders.
 










...Wakuu darasa mlilotoa hapa nawavulia kofia.

-Je, suluhisho la haraka ni nini ili kumkomboa MWANANCHI WA TANZANIA haraka iwezekanavyo kunusuru maliasili zetu, kuboresha kilimo, na kukuza uchumi wetu ili kuelekea kwenye ahueni ya maisha kwa vizazi vyetu vijavyo kabla historia haijatuhukumu?

-Je, kupiga kura pekee kutatosha, au foundation inabidi inazie sasa kwenye shule za msingi mpaka kwenye structure za Tanzania political parties?

-Je, CCM ki vipi inaweza kujisafisha 'kikweli kweli' na na kuchagua kiongozi mkweli na mwadilifu atayeweza kutukomboa? na vyama vya Upinzani vijiandae vipi kuleta ushindani wa kweli katika chaguzi zijazo?

-hatua gani za dharura zinafaa zichukuliwe ili wapiga kura wasijerudia makosa ya kumchagua Rais na wabunge kwakuwa tu 'ana mtandao' unaomlinda kuweza kuchukua madaraka?
 
china wanachama kimoja cha kikommmunist hawana vyama vingi jee hili ni la kuwafata? maana wao wanaamini chama chao kimoja ndio chachu za maendeleo yao.
 
Mchongoma,
Kwanza shukran kwa uwezo wako wa kukusanya data zote zilizotangulia na kuziweka ktk mtililiko wenye picha kamili. Nadhani kinachotakiwa kufanywa na CCM ni kufuata hatua kwa hatua maelekezo ya mapungufu ambayo tumeyaorodhesha.
Ikiwa kilimo ndicho uti wa mgongo basi wananchi kwa ardhi zao wapewe zana, mbegu na mbolea kwa mikopo ama ku-lease na vifaa hivyo vinaweza kuwa miliki ya Halmashauri. Ni vugumu kuweza kumpata dealer wa vifaa vya kilimo ikiwa ni asilimia 0.001 ya wananchi kijijini wenye uwezo wa kununua zana hizo. Mashirika ya kusafirisha mazao (finished product) nje yawe na contact moja kwa moja na wakulima wakiwekesha viwanda vyao ndani nchini, hii itasaidia kuongeza ajira kwa wananchi.
Katika maswala ya miundombinu, ubinafsishaji wake uwe ktk mfumo wa contract pamoja na kwamba tumesha uza mali yote! Malighafi zetu zisiruhusiwe kusafirishwa nje kama kuna uwezekano wa kufungua kiwanda cha kinachozalisha finished product. Mpango wa kina walanguzi kina Mohammed Enterprice kwenda badilishana na wakulima unga wa mahindi ulokuwa expired kwa Korosho ufe kabisa.
Wawekeshaji wapewe motisha ktk uwekeshaji wa viwanda vinavyoweza ku deal na mali ghafi yetu. Majaribio ya kilimo cha mazao yenye thamani kama vile Pamba ya Misri, kahawa ya Colombia na kadhalika yafanyiwe uchunguzi mkubwa ktk baadhi vitongoji kabla hayajapewa umuhimu wa kitaifa. Tukumbuke tu siku zote tutavuna tulichopanda, hata siku moja tusifikirie kwamba Utajiri hutokana na mirathi bali hujengwa hata Utalii hautokani na urithi alotuachia wa ardhi na wanyama alotupa mwenyezi Mungu. Utalii pia hujengwa kama tunavyoona ktk visiwa vya Bahamas, Miji kama Las Vegas, Atlantic City, Florida na hata Mombasa.

Mtu wa pwani,
kama unakumbuka hata mwl. alisema kuwa siasa yetu ya Tanzania ilikuwa ni ya Demokrasia ikiwa na maana kuwa mrengo wa nchi nzima ni mmoja isipokuwa demokrasia ipo ktk uchaguzi wa watu. Hapo tulipewa mifano ya NYUMBA na JEMBE tofauti na demokrasia ya nchi za magharibi ambayo kuwepo kwa vyama vingi ndiko kunakoashiria demokrasia..
Kwa hiyo ni muhimu kwetu kujiuliza hasa demokrasia yetu ni kitu gani hasa kinachotakiwa kuwepo. Mathlan ukiniuliza mimi nitasema kwamba Tanzania hatuhitaji vyama vingi kwa sababu mazingira yetu hayafanani na yale ya nchi za magharibi. Mrengo wa kulia ama kushoto hauwezi kuwa na nafasi ktk taifa maskini hata kidogo. kwa hiyo uchaguzi wa watu kama demokrasia ni bora zaidi isipokuwa unatakiwa marekebisho makubwa ambayo viongozi wote watakuwa na nafasi sawa ktk teuzi mbali mbali.
Nitapenda kuona Salim A. Salim, Malecela, JK, Mbowe, Mrema na wengine wakiwa ktk fainali ya uchaguzi wa rais wa nchi yetu. jambo hili linawezekana tu ikiwa tutakuwa na chama kimoja kwani sera za vyama vyetu kitaifa havina mrengo.
What is the use kuwa na vyama vingi ikiwa sera za Chadema zinaweza chukuliwa na CCM ama CUF na tusione ubabaishaji wa mrengo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…